Mabadiriko makubwa Facebook, kuwa makini

Mabadiriko makubwa Facebook, kuwa makini

Kilongwe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2008
Posts
423
Reaction score
116
Facebook ikiwa ni nyumba ya online kwa mamilioni ya watu duniani, hivyo mabadiriko yanayotokea kwenye facebook ni dhahiri yanaathiri kwengi wetu. Katika siku za karibuni Facebook wamekuja na kitu kipya mbacho wenyewe wanakiitaTimeline , hii Timeline ni mpangilio mpya wa kurasa ya facebook ambao unamuwezesha mtumiaji kupanga picha,matukio nk kulingana na muda husika.
facebooktime.jpg
Picha inayoonesha muonekano wa timeline ndani ya Facebook.
Katika Timeline, utaweza kupanga taarifa zako kwa mtindo wa kipekee zaidi huku ikimpa nafasi mtembeleaji kuzipitia kwa haraka zaidi. Kama utaangalia picha ya hapo juu, utaona kwenye timeline yangu mtu akija mara ya kwanza ataona marafiki,picha na mengine meengi. Siyo hayo tu, kwa kutumia timeline mtu anaweza kuangalia matukio yako toka siku ya kwanza uliyojiunga na facebook.
Katika siku zilizopita Timeline ilikuwa ni kwa wanaohitaji, ila kuanzia tarehe moja mwezi wa pili timeline itakuwa ni lazima, utake usitake ni lazima utumie au kwa lugha ya kiufundi tunaweza iita de
miaka.jpg

fault. Hivyo usishangae kuona mabadiriko kwenye kurasa yako.

Kitu ambacho kimenivuta kuandika hii makala ni kuwa, ingawa timeline ni nzuri na ya kuvutia, ila Facebook inaonekana wanazidi kufanya mambo kuwa magumu,nidhahiri kuwa kufanikiwa kwa facebook kumekuja kutokana na urahisi wa utumiaji. Hivyo kufanya mambo kuwa magumu kutawafanya watu wengi kuikimbia au kushindwa kuifungua hususan wale walio kwenye mgao wa bandwith (internet zilizo taratibu mno). Kuna siku niliwahi kuona mpachiko wa rafiki yangu ambaye ni mtumiaji mzuri mno wa faceboo, yeye alikuwa akilalamika kwa kusema nani amesema tunataka hii timeline?


Kitu kingine kikubwa ambacho kinaniumiza kichwa ni privacy, facebook wenyewe mara kibao wamekiri kuwa privacy ni moja ya vitu vinavyowaumiza kichwa, kwenye facebook ya sasa mtu anaweza kuona matukio yako ndani ya wiki hadi mwezi,ila sasa kwenye hii timeline mtu anaona tukio tangu siku ya kwanza uliojiunga facebook, sasa huku si kuwaumbua watu? Chukulia mfano kwa wale wenzangu na mimi wazee wa kuongopa, huu si ndio mwanzo wa kukamatwa? Hivyo basi kwa kuweka timeline kuwa default kutawatatiza wengi. Habari njema ni kuwa kuanzia sasa unaweza kuanza kufuta matukio kadhaa usiyopenda kuwaonesha watu hadi hapo januari 31.
Je wewe unalionaje hili?

Souurce: Ughaibuni .com - Tekinolojia
 
Aaah sasa umeileta huku ndo facebook...ungewaandikia wenzio huko huko wangeiona tu.
 
sasa hili linahitaji matengenezo gani yakiufundi mpaka utuwekee hapa?
 
haha kuna wanafki watabeza as if hawapo facebook ... while ukienda group ya JF facebook wamejaa tele....
 
Wote tuliohumu na kwenye fb tupo tucmzingue jamaa kajipinda, bongo mbona twapenda kuangushana?!!
 
Aaah sasa umeileta huku ndo facebook...ungewaandikia wenzio huko huko wangeiona tu.

kama wewe ni mtumiaji wa internet, basi kati ya watu kumi kuna zaidi ya nane wanatumia Facebook, hata hapa unaposoma chini kuna twitter na juu kuna facebook. Mitandao jamii ni sehemu ya maisha katika dunia ya sasa. Kama unafuatilia, UN wamepitisha Internet kuwa moja kati ya human right na social network ni moja ya viongozi. So hakuna website itakayoenda bila social network.

Likwanda said:
Dah, Kichwa cha habari na miguu tofauti lol!

Mkuu, Nimesema vitu viwili, Mabadiriko makubwa, kuwa makini. Katika utendaji wa tovuti, kitu kinachobadirisha muongozo wake ni kitu kikubwa, Katika timeline sio tu wamebadirisha muongozo bali hata muonekano hivyo sio kitu kidogo. Pia kama ni mfuatiliaji utajua nini ninamaanisha. Hivyo bado natetea na ninastick na kichwa cha habari.

Dr Phone said:
sasa hili linahitaji matengenezo gani yakiufundi mpaka utuwekee hapa?

Tunapozungumzia technology haimaanishai kila siku ucheze na kodi au matengenezo. Katika miaka ya 80 kipindi technology inakuja wadau wengi walijikita zaidi kwenye technology na kuacha jamii, ndio maana enzi zile ukimkuta programmer hajui lolote zaidi ya code. Dunia ya sasa imebadirika na technology ya leo ni ile inayoingiliana na jamii.
Chukulia mfano, leo hii kaja kaka Mtazamaji simu yake imeharibika na wewe ndiye fundi, kama ingekuwa miaka ya 90, wewe ulikuwa na jibu moja tu, naweza kuitengeneza kwa mia moja. Ila kwa sasa kabla ya kujibu utaangalia upande wa biashara(Gain), jamii(Ethics) na faida zisizo za kipesa (Other business value) na jibu utakolotoa litakuwa ni lenye kujenga.
 
Nimeishaiona hii tayari kwa facebook page za watu wengine, sikuelewa ni nini hasa.Mdau umetufungua macho na hayo mambo yao ya time line. Itabidi tuwe makini, japo tunadonoa donoa kuingia huko, ila nadhani tunahitaji umakini zaidi sasa.
 
Nimeishaiona hii tayari kwa facebook page za watu wengine, sikuelewa ni nini hasa.Mdau umetufungua macho na hayo mambo yao ya time line. Itabidi tuwe makini, japo tunadonoa donoa kuingia huko, ila nadhani tunahitaji umakini zaidi sasa.
 
Nipo tayari kuyapokea MABADIRIKO unajau mabadiriko ni kitu kizuri sana hasa mabadiriko hayo yanapoenda na wakati kwahiyo sio fb tu hata sisi tunatakiwa tuwe na mabadiRIko.
 
Taarifa yako imenipa maarifa, nilikuwa sijui hata hiyo timeline. Asante sana ndugu, na ole wa wanafiki wanaobeza fb huku wakiwa na account huko.
 
lengo la fb ni kuwa na siri na mienendo yote ya watumiaji
 
Ningechangia lakini ninawiki mbili tangu ni delete my facebook acount permanently. nasubiri mwezi huishe taarifa na details zangu zote zifutwe milele.
 
Naona kuna memebr wao kila jukwaa kwao ni siasa za magamba na magwanda
 
mie siipendi hio timeline,kama wataweka lazima kwa kila member watanibore, i just dissaprove it,naona ina mambo mengi to the extent its confusing me....
 
Back
Top Bottom