Mabadiliko yatarajiwayo - Uongozi CHADEMA 2013

hivi chadema hakuna wanawake wanaofaa kuwa viongozi?
Duh! Yaani unataka na Chadema waanze kuchaguana kwa misingi ya jinsia? Kama walivyofanya CCM kwa kumtema Sitta kwa kudai kwamba safari hii wanataka spika mwanamke, matokeo yake unayaona hata wewe, kiuwezo Makinda hamfikii Sitta labda kwa jazba tu. CDM tunahitaji watu wenye uwezo na katika hili hakuna suala la uanamke au uanaume.
 
Ninauhakika hiyo POST imetoka LUMUMBA,ukiisoma ina maana moja tu ya kumtoa Dr slaa nje ya ulingo wa siasa wakati yeye ndiye anayeang'aa kuliko mwanasiasa mwingine yeyote wa upinzani na hata ndani ya chadema..Dr slaa anakubalika kuchukuwa cheo chochote ndani ya chadema na nchi.CCM bwana wanamuogopa sana Dr slaa kiukweli ukiangalia ndani ya ccm hakuna mtu yeyote atakaye mtoa Dr slaa kwenye mbio za kuingia Ikulu..ndiyo maana kila aina ya mbinu inatumika kumuweka Dr slaa mbali na mbiyo hizo za Ikulu.ngoja tuone ni mda tu utakao sema Dr slaa njia ya kuingia ikulu inaonekana kuwa wazi kwake,sababu ndani ya ccm kwakweli hakuna kiongozi yeyote anayeaminiwa na Watanzania wengi kulinganisha na Dr slaa.
Angalia mleta mada anakwambia ZZK haaminiki kwenye nafasi ya katibu mkuu lakini anaaminika kwenye nafasi ya N/katibu mkuu,why??? nawaombeni wanamageuzi wa kweli tukomae sana huku kwenye mitandao hawa jamaa wameshajua kuwa huku kuna nguvu kubwa ya ushawishi,wanabadilisha ID kila siku na kutuchanganyia habari.DR SLAA FOR PRESEDENT.

Umeona eeh? Hata shetani mara nyingi huja kama malaika wa nuru ili wasi mstukie mapema....Mafisadi wana haha kweli maana wanajua what will follow when Dr. enters the highest office....
 
Dr slaa lazma aendelee kuwa katibu mkuu coz ana msimamo usioyumba,ana akili na uwezo mkubwa wa kusimamia nidhamu,cha msingi abadilishiwe naibu,ZITO kapwaya,kakitenga chama yupo bze kusaka urais,nafasi yake apewe Heche au Lema,ama kwa hakika chama kitazd kuwa tishio
 
Ondoa uchuro hapa,

kwa hiyo mangula Na Yule mwizi Wa nyara za taifa ndio vijana!
 
hivi chadema hakuna wanawake wanaofaa kuwa viongozi?

Wapo wengi kwani wewe unaichukulia propaganda hii ya magamba kuwa ni msimamo wa chama? hata kama mkeo ni kamanda na anamudu mwambie asubiri muda ufike achukue fomu chama hakina hiana kinaangalia performance na sio sura au jinsia ya mtu!
 
Kwa maoni yangu ili CHADEMA ije kuwa tishio kwa CCm itabidi wakubali kufanya maamuzi magumu na kuingiza sura mpya katika nafasi za juu na hatimaye mgombea uraisi. Ushabiki kwa Dr Slaa au Mh. Zitto havitaleta ukombozi unaofikiriwa. Watafakari wasije kupigwa goli la kisigino kirahisi 2015.
 
Kwa hiyo unataka kusema kuwa Zitto anataka karibia kila nafasi ya uongozi hapo Chadema
 
kwa maoni yangu ili CHADEMA iweze kuwa tishio kwenye uchaguzi wa 2015, uchambuzi wa mambo ufanywe si kwa jazba au ushabiki kwa mtu au watu fulani fulani na pili watu waliokwishagombea uraisi wakashindwa wasirudie tena kugombea. Tupate sura mpya kabisa na ikiwezekana itakayokuwa imefuta muonekano kuwa chama cha wachaga au wametumwa na vatikani. Maneno ya jinsi hii ndio vitu vilivyotumika kirahisi sana kughilibu watu.:target:
 
Zitto anaendesha siasa za kuua chama ili binafsi afaidike. Hafai kwa nafasi yoyote.

A ha upuuzi we we akiua chama atafaidika vipi sasa? Hat a kama anataka uraisi anautaka kupitia chadema akiiua chadema ataupataje huo uraisi? Tumieni akili ktk kuchangia maada sio kukurupuka tu. Zito ameyafanya men I ndani ya chadema lab a nyie ndo mnaua chama kwa sababu cdm ndo uhai wa zito nae ni uhai wa chadema tangu amalize chuo hajatumikia kazi nyingine zaidi ya cdm hata kikombe chake ndani amenunua kwa pesa ya alizopata cdm. Acheni upuuzi nyie.
 
kwa maoni yangu ili CHADEMA iweze kuwa tishio kwenye uchaguzi wa 2015, uchambuzi wa mambo ufanywe si kwa jazba au ushabiki kwa mtu au watu fulani fulani na pili watu waliokwishagombea uraisi wakashindwa wasirudie tena kugombea. Tupate sura mpya kabisa na ikiwezekana itakayokuwa imefuta muonekano kuwa chama cha wachaga au wametumwa na vatikani. Maneno ya jinsi hii ndio vitu vilivyotumika kirahisi sana kughilibu watu.:target:
Madhara ya kubugia gongo kaabla ya kukaa kwenye keyboard ndiyo haya.
 
Ndugu wana jamvi, katika duru mbalimbali baada ya kikao cha kawaida cha kamati kuu ya CHADEMA, ishu inayozungumzwa zaidi ni uchaguzi na upangaji safu ya juu ya uongozi wa chama kwenye uchaguzi ujao wa chama 2013.

Nafasi ya Mwenyekiti>

1.Freeman Aikaeli Mbowe - katika duru mbalimbali bado anapewa nafasi kubwa kuendelea na nafasi yake. Kiumri, uzoefu, uongozi thabiti bado CHADEMA inamuhitaji KAMANDA wa Anga (kama wanavyoenda kumwita) aendelee kukongoza kwa miaka mingine mitano.
Tishio alikuwa ndugu Zitto Z. Kabwe mbye kw kutambua mchango wa Freeman Mbowe na athari za uamuzi wa kuamua kugombea safari hii ameamua hatagombea.

Nafasi ya Makamu Mwenyekiti.

Yapo Majina mengi yanatajwa kubwa upepo unavuma kwa kasi kwa Prof. Abdallah Jumbe Safari, mtu anayefahamika kwa misimamo yake thabiti, anaeichukia CCM kwa dhati. Yupo tayari kumkosoa yeyote kistaarabu bila kujali nafasi yake.
Tishio yaonekana bado Prof. Safari ni mgeni ndani ya siasa za CHADEMA.

Pongezi kwa mzee Arfi kuamua kupisha wengine.

Nafasi ya Katibu Mkuu.

wapenda mabadiliko ndani ya chama wanaona ni vyema Dr Wilbroad Peter Silaa yamfaa sasa kupumzika au kupisha damu mpya ili kuendeleza mapambano kwa kasi kubwa zaidi na Ndugu Silaa aende kuwa mwenyekiti wa baraza la wazee
majina yanayo tajwa sana ni
1. Zitto Zubeir Kabwe
2. Tundu Antiphas Mughwai Lissu.


Ndugu Zitto Zubeir Kabwe kutokana na aina ya siasa anazozifanya sasa inampa wakati mgumu kukikwaa cheo hiki kw kiasi fulani amepoteza imani kwa wanachama wenzake na anaonesha anasimamia zaidi malengo binafsi dhidi ya yale ya chama.

Ndugu Tundu Lissu - ni kiongozi mwenyew msimamo mkali anaonekana yupo tyari kusimamia nidhamu ndani ya chama bila upendeleo.

kwa vyovyote TUndu Lissu anaweza kukikwaa cheo hiki.


Naibu Katibu Mkuu

1.Bara (Tanganyika) - Ndugu Zitto Z. KAbwe anatajwa kuendelea katika nafasi yake.

2. Visiwani (Zanzibar) - zipo tuhuma za kupwaya kwa Naibu wa sasa Ndgu Yusuph Hamad japo mbadala wake haujaonekana kwa sasa,
Chadema ina kazi zaidi kujipanga Zanzibar.

kwa maoni zaidi ndugu John J Mnyika ameonesha kaimudu zaidi nafasi yake ya uenezi

Tutarajie mabadiliko ya 50/50 kwa sura za Kamati kuu na viongozi w mikoa potential kisiasa - Mwanza, Mbeya, Arusha, Kilimanjaro na Shinyanga.

Lengeri.
Unajua kuandika lakini huoni.
 
Kazi inayofanywa ni kumtenga Dr Slaa na siasa! Kuna watu na heshima zao wanajaribu hata kufikiria ushauri huu! CCM hawapambani na CDM tena bali Dr Slaa na mbaya zaidi wanasaidiwa na wana CDM wenyewe kwakujua au kutokujua.

Analysis kama hizi zimetoka CCM lakini wanasahau hii ni JF! Mwanzisha mada unataka kusema Dr Slaa amezeeka kiasi cha kuongoza baraza la wazee? akina Mtei? Alafu hapo hapo dhambi inakutafuna kwa kumjumuisha Prof Safari age mate wa Dr Slaa! wapi na wapi?

Msitufanye majuha CDM kinataratibu zake!

Copy Lengeri
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom