Mabadiliko yatarajiwayo - Uongozi CHADEMA 2013

kwani mbona mnatumia nguvu nyingi kunadi zito?chama chetu kina utaratibu mzuri wa kupata viongozi,kwa sasa DR hana mpinzani mwacheni ajenge chama .mda ukifika kama ataonekana kupwaya basi atapewa mwingine na inawezekana asiwa zito,kwani kila mwanachama ana nafasi ya kuwa kiongozi endapo atakidhi vigezo vya chama na sifa za kuwa kiongozi
 
Ndugu wana jamvi, katika duru mbalimbali baada ya kikao cha kawaida cha kamati kuu ya CHADEMA, ishu inayozungumzwa zaidi ni uchaguzi na upangaji safu ya juu ya uongozi wa chama kwenye uchaguzi ujao wa chama 2013.

Nafasi ya Mwenyekiti>

1.Freeman Aikaeli Mbowe - katika duru mbalimbali bado anapewa nafasi kubwa kuendelea na nafasi yake. Kiumri, uzoefu, uongozi thabiti bado CHADEMA inamuhitaji KAMANDA wa Anga (kama wanavyoenda kumwita) aendelee kukongoza kwa miaka mingine mitano.
Tishio alikuwa ndugu Zitto Z. Kabwe mbye kw kutambua mchango wa Freeman Mbowe na athari za uamuzi wa kuamua kugombea safari hii ameamua hatagombea.

Nafasi ya Makamu Mwenyekiti.

Yapo Majina mengi yanatajwa kubwa upepo unavuma kwa kasi kwa Prof. Abdallah Jumbe Safari, mtu anayefahamika kwa misimamo yake thabiti, anaeichukia CCM kwa dhati. Yupo tayari kumkosoa yeyote kistaarabu bila kujali nafasi yake.
Tishio yaonekana bado Prof. Safari ni mgeni ndani ya siasa za CHADEMA.

Pongezi kwa mzee Arfi kuamua kupisha wengine.

Nafasi ya Katibu Mkuu.

wapenda mabadiliko ndani ya chama wanaona ni vyema Dr Wilbroad Peter Silaa yamfaa sasa kupumzika au kupisha damu mpya ili kuendeleza mapambano kwa kasi kubwa zaidi na Ndugu Silaa aende kuwa mwenyekiti wa baraza la wazee
majina yanayo tajwa sana ni
1. Zitto Zubeir Kabwe
2. Tundu Antiphas Mughwai Lissu.


Ndugu Zitto Zubeir Kabwe kutokana na aina ya siasa anazozifanya sasa inampa wakati mgumu kukikwaa cheo hiki kw kiasi fulani amepoteza imani kwa wanachama wenzake na anaonesha anasimamia zaidi malengo binafsi dhidi ya yale ya chama.

Ndugu Tundu Lissu - ni kiongozi mwenyew msimamo mkali anaonekana yupo tyari kusimamia nidhamu ndani ya chama bila upendeleo.

kwa vyovyote TUndu Lissu anaweza kukikwaa cheo hiki.


Naibu Katibu Mkuu

1.Bara (Tanganyika) - Ndugu Zitto Z. KAbwe anatajwa kuendelea katika nafasi yake.

2. Visiwani (Zanzibar) - zipo tuhuma za kupwaya kwa Naibu wa sasa Ndgu Yusuph Hamad japo mbadala wake haujaonekana kwa sasa,
Chadema ina kazi zaidi kujipanga Zanzibar.

kwa maoni zaidi ndugu John J Mnyika ameonesha kaimudu zaidi nafasi yake ya uenezi

Tutarajie mabadiliko ya 50/50 kwa sura za Kamati kuu na viongozi w mikoa potential kisiasa - Mwanza, Mbeya, Arusha, Kilimanjaro na Shinyanga.

Lengeri.

Nafasi ya Makamu Mwenyekiti.


Esther Wasira


Naibu Katibu Mkuu

Halima Mdee

KATIBU MWENEZI

Ben Saanane


Naibu Katibu Mkuu

Godbless Lema
 
CCM wanapoteza muda badala ya kuwatumikia wananchi wanawahadaa ngoja wananchi wawagundue watawasusa mtaaibika kwelikeli.
 
Nahisi kama umebadiri ID hivi, siamini kama ni kweli we ni mgeni humu hata kidogo, hebu angalia hapa.

Join Date : 10th December 2012Posts : 119
Rep Power : 325
Likes Received24
Likes Given0
Sasa wewe kinachokupa wasiwasi hapo ni nini? Mimi ni member ambaye bado ni mgeni kama inavyoonekana katika profile yangu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom