Mabadiliko ya Wizara Mbili na UTEUZI, Februari 6, 2026

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
4,783
Reaction score
14,975




YAH: MABADILIKO YA MUUNDO WA WIZARA MBILI NA UTEUZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko ya muundo wa Ofisi ya Rais - Mipango na Uwekezaji na Wizara ya Nishati kwa Wizara hizo kuwa na Makatibu Wakuu wawili kwa kila Wizara, kuteua na kufanya uhamisho wa viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, viongozi walioteuliwa ni kama ifuatavyo:-

(a) Wakuu wa Mikoa

(i) Kanali Yahya Ramadhani Kido ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera akichukua nafasi ya Bi. Fatma Mwassa; na

(ii) Kanali Donald William Msengi ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara. Kanali Msengi anachukua nafasi ya Kanali Patrick Kenan Sawala ambaye atapangiwa majukumu mengine.

(b) Makatibu Wakuu

(i) Dkt. Tausi Mbaga Kida ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Mipango na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango;

(ii) Dkt. Fred Matola Msemwa ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Uwekezaji;

(iii) Balozi Waziri Rajab Salum ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda na Biashara. Balozi Salum anachukua nafasi ya Dkt. Hashil Twaib Abdallah ambaye atapangiwa majukumu mengine;

(iv) Dkt. James Peter Mataragio ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati anayeshughulikia masuala ya mafuta na gesi asilia. Aidha, Mhandisi Felchesmi Jossen Mramba atakuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati anayeshughulikia masuala ya umeme na nishati jadidifu;

(c) Makatibu Tawala wa Mikoa

(i)

(ii)Dkt. Toba Alnason Nguvila ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha. Dkt. Nguvila anachukua nafasi ya Bw. Missaile Musa ambaye amestaafu; na

Dkt. Stephen Justice Nindi ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe. Dkt. Nindi anachukua nafasi ya Bi. Judica Omary ambaye amestaafu.

(d) Naibu Makatibu Wakuu

(i) Bw. Nsubili Akomeligwe Kajela Joshua ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha anayeshughulikia huduma za hazina. Bw. Joshua anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bi. Jenifa Omolo ambaye aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Maendeleo ya Vijana;

(ii)Bw. Aristides Robert Mbwasi ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda na Biashara. Bw. Mbwasi anachukua nafasi ya Dkt. Suleiman Hassan Serera ambaye atapangiwa majukumu mengine;

(iii) Prof. Mohammed Sheikh ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia masuala ya uvuvi. Aidha, Dkt. Edwin Mhede aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara hiyo atapangiwa majukumu mengine;

(iv)Bi. Rose Zacharia Ambrose ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji;

(v)Bw. Emmanuel Tayari ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Afya anayeshughulikia masuala ya dawa na vifaa tiba;

(vi) Prof. Peter Lawrence Makenga Msoffe amehamishwa kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo anayeshughulikia masuala ya maendeleo ya mazao na usalama wa chakula, akichukua nafasi ya Dkt. Stephen Justice Nindi ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe;

(vii) Dkt. Fabian Magawa Madele ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia masuala ya mifugo; na

(viii) Balozi Baraka Haran Luvanda ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia masuala ya mazingira.

(e) Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango

(i)Bw. Sosthenes Laurent Kewe ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mtendaji, Tume ya Taifa ya Mipango anayeshughulikia masuala ya ufuatiliaji na tathmini. Bw. Kewe anachukua nafasi ya Dkt. Linda Ezekiel ambaye atapangiwa majukumu mengine.

(f) Balozi
(i)Meja Jenerali Marco Elisha Gaguti ameteuliwa kuwa Balozi na atapangiwa kituo.

(g) Mwenyekiti wa Bodi

(i)Dkt. Hassan Mahmoud Mshinda ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).

Aidha, uapisho wa viongozi wateule utafanyika kwa tarehe itakayopangwa baadaye.

Bakari S. Machumu
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu
 
Ana maana Gani sisi mkoa wa Kagera kutuletea mwanajeshi tena kanali, tena kutoka kobazi
 
Huyu mama Bi Fatma Mwassa aliyekiwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera kakosea wapi? Alikuwa mtu mzuribhasa kwa Kagera. Kwa hiyo ndo mama kam dump? Hajampeleka popote?🤔
 
Huyu mama Bi Fatma Mwassa aliyekiwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera kakosea wapi? Alikuwa mtu mzuribhasa kwa Kagera. Kwa hiyo ndo mama kam dump? Hajampeleka popote?🤔
Uzyri wa huyo mkuu wa mkoa ulikua kwenye nini? Kitu gani?
 
Walioonekana hawafai watafaa tu huko mbele ya safari.

Cc: Biteko&Jafo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…