SoC02 Mabadiliko ya mfumo wa Elimu kwa manufaa

Stories of Change - 2022 Competition

akyo

Member
May 6, 2017
38
25
UTANGULIZI

Mfumo wa elimu katika nchi yetu hauna mchango mkubwa sana kwa kuzingatia mahitaji ya ulimwengu wa sasa. Ulimwengu wa sasa unataka ubunifu,uwezo wa kutatua changamoto zilizo katika jamii zetu na utafiti katika stadi mbalimbali za maisha.

Chapisho hili litagusa maeneo matatu ambayo ni;
a)Elimu ya sasa na changamoto zake.
b)Mapendekezo
c)Matarajio

Katika maeneo haya,kila eneo tutajadili vipengele hivi;Umri wa kuanza shule, upimaji katika ujuzi/stadi za maisha,elimu katika teknolojia,elimu katika michezo & sanaa na utamaduni,ushindani elimu kimataifa na lugha ya kufundishia.


a)ELIMU YA SASA.

1.UMRI WA KUANZA NA KUMALIZA SHULE.

Umri wa kuanza shule kwa mtoto ni kuanzia miaka 6-8 kwa darasa la kwanza anamaliza la saba na miaka13-15 .Hivyo mtoto kumaliza kidato cha nne ni kati ya miaka 17-19.Kijana anamaliza kidato cha sita na miaka 19-21.Akiendelea chuo Ni miaka 20-24/25.

Changamoto katika umri
√Watoto wanamaliza shule wakiwa na umri mkubwa kwa kuzingatia mfumo wa elimu yetu.
√Madarasa ya kusoma ni mengi na hayapimi vizuri matakwa ya elimu kwa sasa.

2.UPIMAJI WA UJUZI NA STADI ZA MAISHA.
Watoto wa shule za msingi kwa mujibu wa "MTAALA WA ELIMU YA MSINGI" darasa la kwanza na la pili wanapimwa kujua " KKK" darasa la 3-7 wanapimwa kuwajengea ujuzi katika stadi za KKK na stadi nyingine za maisha.

Kwa upande wa sekondari ujuzi umejikita katika masomo wanayosoma kwa maana ya Masomo ya Sayansi,sanaa na biashara.
Vyuo vikuu ujuzi unapimwa katika kuendana na fani uliyoisomea.

Changamoto za upimaji ujuzi na stadi
√Wanafunzi wa shule za msingi hawapimwi vizuri ktk stadi nyingine za maisha pamoja na kuwepo kwa somo la stadi za kazi.
√Wahitimu wa vyuo vikuu hawewezi kujipima vizuri ktk ujuzi na stadi za maisha kwasababu mfumo wa elimu yetu ni wanadharia zaidi kuliko vitendo.
√Mitaala ya ngazi zote za elimu haizingatii matakwa ya ulimwengu wa sasa ndio maana wahitimu ni wengi na wanashindwa kuwa na ujuzi katika stadi za maisha na ujuzi.

3.ELIMU KATIKA SAYANSI NA TEKNOLOJIA.
Matakwa ya kisera kwa majibu wa MTAALA WA ELIMU YA MSINGI unasisitiza matumizi ya Sayansi na teknolojia katika utoaji wa elimu ngazi zote.Mfano kwa shule za msingi wameanzisha TEHAMA.Kwa upande wa vyuo Kuna baadhi wanasoma IT na baadhi ya ya vyuo vinahusika na Sayansi na teknolojia tu.Mfano,MUST na DIT.

Changamoto katkia Sayansi na teknolojia
√Uhaba wa vyuo vingi vinavyohusu Sayansi na teknolojia nchini.
√Uhaba wa wakufuzi wa kutosha katika vyuo kwa kuzingatia imuhimu wa Sayansi na teknolojia kwa ulimwengu wa sasa.
√ Vyuo vilivyopo havigusi mahitaji ya watanzania wengi hasa kwenye sekta ya kilimo na viwanda ndio maana tunakosa thamani ya malighafi zetu kuwa bidhaa.
√Utafiti haushirikishi sana mataifa mengine yaliyopiga hatua kwenye Sayansi na teknolojia ili japo tupate ujuzi kuotaka kwao.Hiyo ni kazi ya mabalozi wanaoiwakilisha nchi ktk mataifa mbalimbali.
√Kutowatambua na kuwashirikisha wagunduzi toka mtaani,mfano kuna mwaka kijana kutoka Tunduma alitengeneza helicopter,lakini hakuendelezwa na kusaidia ili kutoa hamasa ya ugunduzi kwa vijana wengine.

4.ELIMU KATIKA MICHEZO SANAA NA UTAMADUNI.
Kwasasa kuna mashindano ya UMTASHUMTA ambao unahusisha michezo mbalimbali kwa shule za msingi na UMISETA kwa shule za sekondari.
Kwa upande wa vyuo kuna mashindano ya michezo kwa vyuo vikuu Tanzania na Afrika Mashariki.

Changamoto katkia sanaa&utamaduni na michezo
√Vipaji vilivyopatikana kutoka katika UMISETA, UMTASHUMTA na Mashindano ya vyuo vikuu haviendelezwi.
√Uhaba wa shule zinazohusisha michezo na sanaa Kama masomo mengine.Zipo chache sana.
√Uhaba wa vyuo vya sanaa na michezo ambavyo tungepata wasanii,waigizaji na wachezaji mbalimbali.
√Ukosefu wa miundombinu ya kutosha Kama viwanja vizuri,mazingira rafiki kwa watoto,vifaa vya michezo na utamaduni n.k
√Wazazi kuchukulia sanaa,michezo na utamaduni Kama uhuni,hivyo kukosa kuwasaidia watoto kuviendeleza vipaji vyao.

5.USHINDANI WA ELIMU KIMATAIFA.
Tanzania inaendelea kushindana kimataifa hasa katika ngazi ya vyuo vikuu.Kwa mujibu wa" gazeti la mwananchi la November 3 mwaka 2021".Lilichapisha nafasi ya vyuo vikuu vya Tanzania barani Afrika Kama ifuatavyo;

UDSM( 42), SUA (51),MUHIMBILI ( 91), UDOM (174) Mzumbe (203) na SUZA (255).

Hata hivyo mwananchi linaeleza kishuka kwa nafasi za vyuo vikuu vya Tanzania kimataifa.Mwanchi linaeleza kuwa vigezo vilivyotumika kupima ni utendaji Kama; kusheheni machapisho ya kitaaluma,kazi za kibunifu na taarifa nyinginezo zinazohusu taaluma ngazi ya kimataifa.

Changamoto ya elimu kimataifa.
√Ukosefu wa machapisho mengi ya kitaaluma kwa vyuo vyetu.
√Uhaba wa tafiti na ubunifu wa katatua changamoto zinazoukabili ulimwengu kwa vyuo vyetu.
√Ushirikiano hafifu kati ya vyuo vyetu na vyuo kutoka sehemu mbalimbali duniani,hii anasababisha kutokupata mawazo mapya.
√Serekali kutokutenga bajeti ya kutosha kwenye elimu yetu ili iwe shindani kimataifa,bajeti itadaidi uwepo wa vitabu na vifaa vingine vinavyohitajika katika elimu.

6. LUGHA YA KUFUNDISHIA.
Lugha ya kufundishia katika ngazi ya shule za msingi za serikali ni Kiswahili huku nyingi za binafsi ni Kiingereza.Upande wa Sekondari na vyuo ni Kiingereza.

√Lugha inayotumika shule za msingi imetofautiana kwa kuwa shule za binafsi wanatumiia Kiingereza na serikali wanatunia Kiswahili,hivyo kutengeneza utofauti miongoni mwa wanafunzi
√Lugha yakufundishia kwa shule ya msingii haiendani na ushindani kwenye ulimwengu wa sasa.

7. ELIMU KATIKA BIASHARA
Kuna baadhi ya vyuo vya Biashara Kama CBE,IFM n.k.
Pia kwa shule za sekondari Kuna masomo ya Bookkeeping na Commerce.

Changamoto za elimu katika Biashara.
√Masomo yanayofundishwa hayajapewa mkazo,hakuna msisitizo ndio maana watoto hawependelei masomo ya biashara.

√Shule chache zinazosoma masomo ya biashara nchini.Hivyo kukosekana kwa wataalamu wa biashara.

√Masomo ya biashara hayafanywi kwa vitendo badala yake sehemu kubwa ni nadharia.

b). MAPENDEKEZO

1.UMRI WA KUANZA NA KUMALIZA SHULE

√Kupunguzwe madarasa kwa shule za msingi,lianze darasa la 1-6.Darasa la 1&2 yawe kwa lengo la kupima "KKK" na darasa la 3-6 masomo yajikite kupima stadi za maisha na ujuzi mwingine.

√Elimu ya sekondari O'level iishie kidato cha 3 watakafaulu divis 1 & div 2waende A'level,watakata div 3&4 waende vyuo vya ufundi,watajaopata 0 wapwewe elimu ya muda mfupi juu ya stadi za maisha.

√Umri wa kuanza shule uwe miaka 5-6 (darasa la kwanza)tu,ili kuwaanda vijana wangali wadogo ili vjana wawe na manufaa mapema kwa nchi yetu.

2.UPIMAJI WA UJUZI NA STADI ZA MAISHA
√Somo la stadi za kazi kea shule za msingi liwe la vitendo zaidi kuliko nadharia,kwenye mitihani somo hili lipimwe kwa vitendo kama mwanafunzi anaweza kusuka,kujenga,kushona,kucheza,kuimba n.k.
√Kuwepo na soma la lazima kwa sekondari litakolopima ubunifu wa mtoto katika nyanja mbalimbali ikiwemo ufundi n.k.

√Wahitimu wa vyuo vikuu wapewe kozi itakayosomwa kila mwaka kwa muda watakuwepo vyuoni inayohusu utendaji/ubunifu na kozi hiyo ifanyiwe mtihaini kwa vitendo.

√Serikali ijenge vyuo vya ufundi,kilimo na michezo kila Kanda ili kuandaa vijana kwaajili ya kujitegemea na kuendeleza sekta ya viwanda na kilimo.

3. ELIMU KATIKA SAYANSI NA TEKNOLOJIA
√Kujengwa vyuo vingi vya Sayansi na teknolojia ili kuendana na matakwa ya sasa.

√Kuimarisha miundombinu na kuongeza vifaa vya kujifunzia na kufundishia ktk shule na vyuo vyote nchini.

√Kutafuta walimu/wakufuzi toka nje ili kuwafundisha walimu wetu wa masomo ya Sayansi na teknolojia.

√Somo la IT ,computer yawe ya lazima kwa ngazi zote za elimu.

√Kuwepo na ushindani wa vyuo vya Sayansi ktk ubunifu,chuo kitakachoshindwa kipewe zawadi ya kubwa.

4. ELIMU KATIKA MICHEZO SANAA NA UTAMADUNI
√Kujenge vyuo rasmi vya michezo &sanaa kila Kanda.mfano chuo cha michezo kikijengwa mikoa ya kusini,chou cha sanaa kinajengwa mikoa ya kaskazini.

√Kutengwe shule rasmi za michezo na utamaduni kila mkoa.

√Wanafunzi waliochaguliwa kutoka kwenye UMTASHUMTA na UMISETA wapelekwe kwenye shule za michezo.

Baadhi ya topic zinazohusu utumwa ziondolwe kwenye somo la historia.
√Somo la sanaa na utamaduni liwekwe kwenye somo la historia na liwe kwa vitendo.

√Viwanja vizuri vijengwe kwenye kila chuo na shule za michezo.

√Wazazi waelimishwe imuhimu wa sanaa utamaduni na michezo kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

5. USHINDANI WA ELIMU KIMATAIFA.
√Vyuo vyetu vijikite katika tafiti mbalimbali ili kuongeza ubora wa vyuo na wahitimu.

√Mabalozi wanaoiwakilisha nchi waangalie namna ya kuisadia nchi katika suala la elimu kwa kuangalia nchi wanazofanyia kazi.

√Itelejensia ya nchi ihusike katika kuangalia teknolojia ya mataifa yaliyotuzidi ili wailete hapa nchini.

√Serikali iandae bajeti kwaajili ya kuboresha elimu na miundombinu ili iendane na matakwa ya kisasa.

√Vyuo vikuu viandae midahalo mbalimbali na kushindanisha tafiti zao hapa nchi na nje ya nchi ilituendane na ulimwengu wa sasa.

6. LUGHA YA KUFUNDISHIA.
√Kugha ya kufundishia iwe Kiingereza kwa shule za msingi na sekondari.

√Kiswahili kiendelee kuwa somo,na hakiwezi kupotea kwasababu kinatumika kwenye matumizi ya kawaida.

√Kuwepo na uwezekano wa kuongeza somo la lugha kwa baadhi ya shule,mfano kichina ili iwe rahisi kujifinza teknolojia kutoka kwao.

7. ELIMU NA BIASHARA
√Somo la Biashara liwepo ktk machuguzi mtu anapoenda A'level

√Kujengwe vyuo vya Biashara ambavyo vitahusisha vitendo zaidi kuliko nadharia.

√Mtihani wa mwisho ktk masomo ya Biashara upimwe kwa vitendo,mfano mtu ameanzisha biashara,je amafanikiwa vipi?

√Kuongezwe shule zinazofundishwa Masomo ya Biashara.

√Serikali iandae wataalamu watakaofundisha masomo ya biashara kwa nadharia na vitendo.

c).MATARAJIO
Endapo Mapendekezo niliyoyatoa hapo juu yatafanyiwa kazi tutarajie yafutayo;

√Kupungua kwa asilimia kubwa tatizo la ajira nchini kwasababu,vijana wengi watajiajiri kutokana na elimu kuwa ya vitendo zaidi kuliko nadharia.

√Maendeleo katika sekta ya kilimo na ufugaji kwa kwasababu ya elimu itakayotolewa vyuoni.

√Ushindani wa vyuo vyetu kimataifa, hivyo kuchangia hata wahitimu wa vyou vyetu kuhitajika nje ya nchi.

√Maendeleo katika sekta ya viwanda, kwasababu tutapata wataalamu wengi kutoka vyuoni na malighafi zitakuwa bora hii ni kutokana na wataalamu kutoka vyuoni ambao watawaelekeza wananchi uzalishaji wa kitaalamu wa mazao yao.

√Maendeleo katika Sayansi na teknolojia yatakuwa juu.Wataalamu tutawapata kutoka vyuoni, Tanzania itakuwa miongoni mwa nchi zenye teknolojia kubwa.

√Tafanikiwa vizuri katika michezo mbalimbali na kutangaza utamaduni wa nchi yetu,kwasababu tutapata wachezaji wazuri kwenye vyo na shule zetu.

MAREJEO
Mtaala wa Elimu ya msingi darasa 1-7.
Gazeti la mwananchi, November 3
2021.
UNESCO research 2021.
 
Umeandika vizuri ila kwe lugha ndipo kuna ukakasi mkubwa, kwamba kizungu kiendelee kutumika na kiswahili liwe somo tu la kawaida, anyway ni mawazo yako
 
Back
Top Bottom