Mabadiliko Tanzania, Nini Utata? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabadiliko Tanzania, Nini Utata?

Discussion in 'Great Thinkers' started by Hossam, May 31, 2012.

 1. Hossam

  Hossam JF-Expert Member

  #1
  May 31, 2012
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 2,363
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Ni Lini WatanzaniaTutaelewa Dhana ya Mabadiliko?

  NA GODFREY KASSANGA

  DHUMUNI kubwa la Tanganyika chiniya TANU, enzi zile za Mwl J K Nyerere, kudai uhuru kutoka kwa Wakoloni lilikuwani kuikomboa jamii ya Watanganyika na nchi kwa ujumla kutoka katika utawaladhalimu wa kikoloni ambao kwa wakati huo ulikuwa ukipora maliasili za nchi na kushindwa kabisa kuondoa ujinga, kuboresha huduma za afya katika kupambana namaradhi, na kupiga vita umaskini kwa kuleta maendeleo.

  Tafsiri sahihi ya mapambano yakudai uhuru ilikuwa ni Watanganyika kupinga kupuuzwa, kudharauliwa na kunyanyanyaswa katika kila jambo. Hali ya Watanganyika kuonekana hawana maana wala kauli mbeleya Wakoloni ilifanya kila Mwananchi aliyeelimishwa ubaya wa Mkoloni na kutawaliwa, na uzuri wa uhuru na maendeleokuelewa kwa urahisi harakati hizo na kuunga mkono kwa hali na mali.

  Sio lengo langu kujikita sana katika historia ya uhuru wa Tanganyika.Ikumbukwe kwambauongozi ni dhamana na sio haki ya kulazimisha ya mtu. Mwl J K Nyerere alilionyesha hili kwa vitendo pale alipojiuzuru wadhifa wake wa uwaziri mkuupindi tu Tanganyika ilipopata uhuru wake. Palikuwa na minong'ono kwa wale waliochukulia suala hilo kirahisi na wasiwena uwezo wa kuelewa maana ya Baba wa Taifa kujiuzuru. Leo hii katika taifa letuhii itabaki kuwa historia tu kwa vizazi vya sasa.

  Mwaka 1977 TANU iliunganana ASP na kuzaa CCM yaani Chama Cha Mapinduzi. Haieleweki hadi leo maana halisiya neno Chama Cha Mapinduzi, hii ni kutokana na ukweli kwamba Tanganyika haikupata uhuru wake kwa njia yoyote ile zaidi ya mazungumzo. Chama hiki, CCM, kikaaminiitikadi za TANU na ASP hasa zile za ‘Binaadam wote ni sawa', Nitapiga vitarushwa kwa nguvu zangu zote', Nitajitolea nafsi yangu kupiga vita umaskini,ujinga na maradhi', ‘Binadam wote ni ndugu zangu' na nyingine nyingi.

  Mfumo wa sasa waserikali yetu umefanya jamii ya Tanzania sasa haiamini katika falsafa ya ujamaaya kwamba binadam wote ni sawa. Misingi ile ya azimio la Arusha, ileiliyokiukwa mwaka 1992 ikaruhusu viongozi wa umma kumiliki mali, sasa inalitafuna taifa na tabaka la walio nacho na wale wasio nacho limekuwa kubwakiasi cha kutishia amani ya nchi.

  Ieleweke kwamba kauli mbiu ya sasa ya CCM ile isemayo ‘Maisha Bora kwa kila Mtanzania' niafadhali ingesomeka ‘maisha bora kwa kila kiongozi'. Maisha ya Watanzania sasayanaendelea kudidimia huku idadi ya wasiojua kusoma na kuandika ikiongezekasiku hadi siku, maradhi sasa yanazamisha mizizi chini zaidi kwa sababu yahuduma duni na mbovu katika vituo vyetu vya afya nchini. Bajeti ya serikali imekuwa ni finyu mno katika kushughulikia wale maadui watatu, ujinga maradhi naumaskini, na sasa tunae adui wa nne, ufisadi, ambaye mizizi yake ni mirefu na migumu na inatishia ustawi wa taifa.

  Chama kinapokujana kauli mbiu ya ‘maisha bora kwa kila Mtanzania', basi ni budi kikatafsiri dhana hii kwa vitendo. Vitu muhimu na vya lazima kwa maisha ya wananchi wa kawaida kama vile, sukari, maji safi ya kunywa, chakula, mavazi na malazi, ni lazima viwe kipimo cha kauli hii.

  Mifano mingi ipo inayoonyesha ama kauli hii haikufanikiwa ama ilishindwa hata kabla ya kuasisiwa. Hebu tupia jicho gharama ya vifaa vya ujenzi, ona jinsi beiya chakula cha kawaida kwa maana ya unga wa ugali na maharage inavyopanda kilauchao, tupia jicho gharama za mavazi, huduma za afya nazo hazieleweki kabisanchini ona jinsi akina mama wajawazito wanavyoshurutishwa kupeleka mipira ya hospitali (gloves) pindi waendapo kujifungua, na hata vitanda vya kulaza wagonjwa ni vibovu vichafu na havifai.

  Hapa je, hivi lile suala letu la‘maisha bora kwa kila mtanzania' linaleta muelewano wa kimantiki? Hii kwetu siosawa na pale Wakoloni waliposhindwa kuleta mabadiliko na Tanganyika ikaamua kudai uhuru wake ili ilete mabadiliko? Je kwa kuhoji haya ndio tutaonekana wachochezi wa uvunjifu wa amani nchini? Na sasa uzalendo utakuwa wapi kama tutakaa kimya kufumbia macho mambo yanayotesa jamii ya Kitanzania?

  Nchi maskini kama Tanzania inayaotegemea misaada na kuombaomba kila siku haikupaswa kusaga mabilioni ya shilingi za wavuja jasho maskini kabisa katika kusherehekea miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika huku mambo lukuki yakienda mrama. Na sasa zipo taarifa kwamba hata ule mwenge wa uhuru na bendera ya Taifa hazikufika kilelecha uhuru The Uhuru Peak kule mlima Kilimanjaro siku ile ya tarehe 8 December 2011 usiku japo imeripotiwa kwamba vilifika. Imekuwa ni usanii tu katika kila jambo. Ni aibu kwa shirika la utangazaji la taifa, TBC, kushindwa kurusha matangazo kutoka kilele hicho na kuishia kuumauma maneno. Hivi kwa miaka 50 hata teknolojia ya kurusha matangazo kutoka katika vilele virefu inakuwa kitendawili? Nchi hii ina visa.

  Hata kama serikali inasisitiza kwamba maendeleo ya Watanzania yataletwa na Watanzaniawenyewe, hilo ni sawa. Lakini hayo maendeleo yataletwa vipi? Hii mipango yamaendeleo inayoishia kwenye makaratasi ina faida gani leo? Tutaendeleakudanganywa hadi lini? Je ni sawa na kusema kila mtuatasafiri safari ya mbali kwenda kuyabeba maendeleo na kurudi nayo Tanzania?

  Hiyo si kweli. Nchi ni lazima iwe mstari wa mbele katika kusaidia shughuli za ujasiriamali. Serikali ikiweka mazingira rafiki katika uratibu wa kukopa mitaji, kuzuia uingizwaji horera wa bidhaa dhaifu za nje, kujenga mazingira safi ya kuunga mkono ujasiriamali wa wazawa, kusaidia utangazaji wa bidhaa zinazotengenezwa na wazawa na kutoa elimu nafuu ya ujasiriamali, nchi itapiga hatua mbele kimaendeleo na ukali wa maisha utapungua.

  Hebu tutafakariaibu ambayo CCM na kauli mbiu yake ya ‘maisha bora kwa kila mtanzania', na ileya ‘Tumethubutu, Tumeweza na Tunasonga Mbele' na vituko vya mwaka 2010. Hivi maisha gani bora ambayo CCM iliyahubiri kwa Watanzania wakati wa zile kampeni za uchaguzi mkuu na mwishowe baada ya uchaguzi CCM ikakataliwa sehemu nyingi nahatimaye ikawa kigugumizi kutangaza matokeo?

  Sintakosea nikisema wakati wa kutangaza matokeo, hasa yale ya ubunge, Tanzania ilikuwa kama uwanja wa vita katika karibu kilakituo. Polisi wakiwa na silaha za moto na baridi, wakiwa tayari kuwakabili baadhiya raia maskini walioamua mabadiliko, walivyoshupaza shingo zao. Ni imani yangu kwamba kila aliyetega sikio alisikia na kila aliyetazama aliona, suala lililobakia ilikuwa ni juu ya mtu kuelewa na kuamini nini kilikuwa kinaendelea.

  Hivi huu wimbowa mafisadi kutafuna nchi yetu tutauimba hata lini? Kuna sababu gani yakuendelea kuelimishana ubaya wa ufisadi ikiwa Wananchi wenyewe hatutaki kutumiahaki yetu kikatiba kuleta mabadiliko? Itoshe basi kuona watoto wetu wakifukuzwa hovyo vyuoni kwa kudai haki zao, itoshe sasa kuona wagonjwa wakisafirishwa umbali mrefu kufuata huduma za afya, ifike wakati iwe kawaida kuona Watanzania tukiishi kwenye vibanda vya udongo na nyasi huku maisha yakiwa dhaifu na duni hadi kushindwa hata kumudu mlo mmoja kila siku. Na hapa iwe kawaida kwetu kuona wanafunzi katika shule zetu za msingi vijijini wakikaa chini, wakitumia chumba kimoja duni kama darasa la pamoja, na ifike wakati sasa tuone ni sawa viongoziwetu kumiliki mali nyingi, kuishi maisha ya anasa na kukimbia Wananchi katika majimbo yao wakisubiri wakati wa uchaguzi mkuu kuja na maneno matamu, ahadi za hovyo tena zisizotekelezeka, na vijizawadi vya peremende na pilau.

  Ni ukweli usiopingika kwamba Watanzania walio wengi hatujui haki zetu na wajibu kikatiba,lakini swali linabaki palepale, je hii inatosha kwetu kuwa maskini hata wafikra? Kwa mfano ni rahisi kugundua kwamba kati ya Watanzania zaidi ya milioni40 ni wachache tu wanaoifahamu katiba ya nchi kwa ukamilifu. Hii inafanya Watanzania wawe wanyonge katika nchi yaona kuishi maisha ya bora liende. Wananchi wanaporwa madini yao na kuishia mirahabaisiyofaidisha wananachi, ardhi sasa inaporwa lakini kuhoji ni suala gumu kwa Mwananchi, wanafunzi wetu wanamaliza elimu ya sekondari, kidato cha nne nasita, lakini wanashindwa kuelezea elimu ya uraia kwa usahihi, na hali ikiwahivi hata wahitimu wa vyuo vikuu wale waliojikita katika elimu ya sheria punde watashindwa kuwa na tafsiri inayoeleweka ya sheria za nchi yao.

  Ukombozi wa Taifa letu, unafuu wa maisha na mabadiliko katika huduma za jamii ni utashi wa Wananchi wenyewe. Wananchi tunapaswa kuelewa kwamba sasa ni wakati wetu wa kuleta mabadiliko ya kweli na kufanya uamuzi sahihi, sasa ni wakati wetu wa kukataa kutawaliwa na mifumo dume, sasa ni wakati wetu wa kuihoji na kuikosoa serikali bila woga, sasa ni wakati wetu wa kupaza sauti na kusikika, na sasa ni wakatiwa kuchagua viongozi wanaoelewa kwamba uongozi ni dhamana. Kila mtu na awe balozi wa mabadiliko, tuamke na tutafute, kila tuendapo, njia sahihi na namna ya kuukataa umaskini na ukandamizaji ili hatimae tufaidi wote matunda ya uhuru wetu. Nguvu ya umma iwe ndio muongozo wa mwisho wa nchi yetu, na kila mtu awajibike pale alipo kwa faida yake, jamii na nchi kwa ujumla.

  Ile misingi iliyoliunda taifa letu inapaswa kuhubiriwa na kila mzalendo na mpenda maendeleo ili Tanzania ya leo iimbe ule wimbo wa matunda ya uhuru, nchi yetuinayotufaidisha wote bila kujali rangi, itikadi, dini wala kabila.

  0786546555
  godfrey120@hotmail.com

  SOURCE: DIRA January 5, 2012
   
Loading...