SoC03 Mabadiliko kuleta Utawala Bora

Stories of Change - 2023 Competition

Danwest

New Member
Jul 21, 2023
1
2
MABADILIKO KULETA UTAWALA BORA

Mabadiliko, ni hali ya kutoka hatua moja ya chini kwenda juu kuna aina nyingi za mabadiliko ila kuu ni mosi binafsi yaani mtu mmoja mmoja na pili mabadiliko kitaifa nchi kwa ujumla kutokana na hali ya kawaida kwenda kwenye hatua bora, mabadiliko mazuri ni ya kuletwa bila kuhusishwa na ufisadi, utapeli na unyonyaji wa watu na mali zao.

Utawala bora ni hali ya uongozi inayohusisha mabadiliko makubwa katika jamii kutokana na uongozi thabiti uliopo katika mtu binafsi na serikali.

Afrika ina mabadiliko makubwa katika miaka ya karibuni ikitokana na uwekezaji wa sekta binafsi haswa kutoka nchi za magharibi ambazo ni mabepari walio tawala katika enzi za ukoloni na ndio maana utaona waarabu na wazungu wakiwa watawala wa teknolojia na maendeleo badiliko.

Serikali zimesahau kutilia mkazo wa kuinua uchumi wa taifa na watu binafsi pia wametegemea serikali kuleta mabadiliko ikiwa wanawekeza katika chumi za nchi nje ya Afrika .

Shauri langu ni Afrika ikae na kuweka mfumo mmoja wa utawala kielimu unaweza kuinua uchumi wa Afrika kwakuuza vipaji na teknolojia mfano mpira , muziki na filamu kwakutumia mfumo wa miaka kumi na nane nje ya elimu kama ifuatavyo:

Awali iwe mwaka umri miaka 3

Darasa la 1 mpaka 4 elimu msingi -miaka 4 mpaka 8 elimu ya nadharia

Darasa la 4 mpaka 7- miaka 9 mpaka 11 ni elimu mpevuko ya vitendo na wote kuwa chini jeshi la halaiki au skauti yenye kubeba fani za kilimo ufugaji uvuvi misitu na maliasili misitu.

Elimu sekondari iwe miaka miwili Yenye kubeba vitendo vya teknolojia, ujenzi, sanaa yaani muziki, uchoraji fasihi na maigizo filamu, siasa uchumi, utawala na lugha za kigeni zote ili kufanya Afrika kuuzika duniani kote kwa lugha zote kuwa chini ya kiswahili -umri ni miaka 12 na 13.

Elimu ya juu iwe inatolewa kwenye vikosi vya jeshi la kujenga taifa JKT kwa miaka miwili yaani umri wa miaka 14 na 15.

Elimu ya chuo shahada ya kwanza miaka mitatu yaani umri wa miaka 16 mpaka 18.

Pia kwa wale wanafunzi watakao shindwa kufaulu mitihani ya darasa la saba kuto achiwa mitaani wachukuliwe na kuanzishwa jeshi la akiba lenye kuchukua wanafunzi hao na kufanya mafunzo jeshi kama ilivyo kwa mujibu wa sheria JKT hivyo hakutakuwa na mtu tegemezi asiye kuwa na wajibu.

Elimu ya watu wazima, wanafunzi wa kujitegemea itolewe peke yake kwa watu wazima walio nje ya mfumo uliopendekezwa ili kufuta uvivu na uendekezaji wa mimba za mapema utotoni na kupuuzia elimu maana kwa sasa Elimu ni bure ila wanaacha shule.

Jeshi la magereza liwe linatoa mafunzo kwa wakosaji walio fungwa ili kujenga uwanja wa taifa kuwa huru katika kuwahudumia wafungwa inabidi watumike kujenga miradi kama barabara,mashule, hospitali ili kupunguza idadi ya misaragambo kwa raia wa chini.

Hii inaleta taswira halisi ya maendeleo maana vijana imara katika nchi zetu watapatikana kutokea kwenye mafunzo ya kijeshi ambayo itaongeza uzalendo itakayopunguza rushwa na uovu binafsishwaji wa kujiuza, madawa ya kulevya na ushoga.

Daima tukumbuke ukoloni mamboleo ni adui wa Afrika hakuna wakuendeleza Afrika isipokuwa sisi Afrika wenyewe.
 
Back
Top Bottom