Ok, kwa leo nitakufundisha kupika tambi za nazi.
Kama hujui kukuna nazi, tumia hata nazi ya pakti ya Azam.Ila nazi yenyewe ya kukuna ndio nzuri zaidi.
Fuata step hizi:-
1. Katakata tambi zako size unayotaka, wengine hukata mara 2, 3 au werevaaa kisha ziweke pembeni.
2. Weka mafuta ya kula jikoni kwenye sufuria, yakichemka tia vitunguu maji, tia kitunguu saumu punje 3 au 4 zilizopondwa, tia iliki punje 3 zilizotwangwa, tia chumvi, kisha weka na ufuta au food color nusu kijiko cha chai. (ufuta na rangi si lazima ni katika kutia nakshi tu).
3. Endelea kukoroga mchanganyiko wako mpaka utakapoona umekolea na kila kitu kimewiva, kisha baada ya hapo tia sukari vijiko viwili na nusu.
4. Baada ya kutia sukari, sasa tia tambi zako ktk mchanganyiko wako na endelea kuzikoroga taratibu km dk 2-3.
5. Baada ya hapo tia tui la nazi, kama unatumia nazi ya Azam, chukua maji kiasi, tia nazi ya Azam yote, koroga kisha miminia jikoni kwenye tambi zako.
Kama unatumia nazi ya kukuna, tia tui la pili kidogo sana na acha ichemke.
6. Tambi zikianza kulegea, tia tui la kwanza la nazi ya kukuna, hapa wa nazi ya Azam ahusiki maana yeye keshatia kipakti chote awali.
7. Endelea kugeuza mpaka utakapoona tambi zako zimeanza kutoa udelele (urojo) ujue zimewiva.
Onja ili kujua kama sukari na chumvi vimekolea.
Hakikisha sukari na chumvi havizidiani, viwe na uwiano sawa.
8. Baada ya hapo, punguza moto ili zikauke.
Kisha epua na pakua tayari kwa kuliwa.
ANGALIZO:-
Kipimo cha chumvi na sukari inategemea na uwingi wa tambi zako.
Kama utatumia nazi ya Azam, koroga nazi yote na uiweke yote, ukianza kuweka maji halafu ndio tui, tambi zako hazitakolea nazi sawasawa
Tambi za kuliwa na nyama, samaki au mboga yenye asili ya nyama nyama, sukari haitakiwi kuizidi chumvi.
Ila tambi za kuliwa kavu au na chai, uwiano wa chumvi na sukari uwe sawa.
Tambi za kuliwa na uji, sukari isiizidi chumvi.
Tambi za kuliwa na chai yenye kahawa, sukari inatakiwa iizidi chumvi kidogo.
Epuka kukoroga koroga tambi zikiwa jikoni ili kuepuka tambi kurendemka (kurojeka).
Ukiona tambi zinashikana chini (kuungulia) punguza moto.
Naomba hiyo Saturday ukipika, ulete mrejesho, usi-google