Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Idadi kubwa ya vyuo mbalimbali vikiwemo vya ufundi na ualimu vimejengwa na kanisa. Hospitali mbalimbali na zahanati zinaendeshwa na maaskofu. Miradi mbalimbali ya umeme vijijini imeanzishwa na kuhudumiwa na maaskofu.
Viongozi wengi hapa nchini wamesoma katika shule na vyuo vilivyojengwa na kanisa.
Nashangaa leo CCM ikisema maaskofu wavue majoho maana yake wafunge shule, vyuo, hospitali, dispensary, nk
Maaskofu ni sehemu ya jamii, ni wapiga kura, na hivyo basi wanawajibu wa kukemea uovu, au jambo lolote lisilo la haki (kama vile Kuua waandamanaji wasio na silaha Arusha)kwenye jamii yetu. Historia inatuonyesha kwa mfano askofu Desmond Tutu wa Afrika Kusini enzi za apartheid regime alipinga na kukemea utawala dhalimu wa makaburu, ya kubagua, kudhalilisha, kuwafunga na hata kuwaua raia wenye asili ya Kiafrika.Hata kule Egypt wakati wa Farao ilifikia Mungu akamtuma Musa kuwakomboa wana wa Israeli toka kwenye utumwa wa zaidi ya miaka 400.Hivyo nahitimisha kwa kusema ni sahihi kabisa viongozi wa dini kuikosoa na hata kuikemea serikali pale inapokwenda kinyume na utaratibu unaokubalika kijamii.Anyayesema viongozi wa dini wakae pembeni kwenye masuala kama hayo ujue huyo anamatatizo ya uelewa (kufikiri) au anafanya makusudi kwa lengo la kuleta mkamganyiko kwenye jamii.
Hivi leo baraza la maaskofu waseme tunaiunga mkono cdm sababu inania ya kweli kukomboa nchi hii, kisha bakwata wasme sisi tunaiunga mkono ccm maana imeonyesha nia ya dhati kuleta maendeleo, wahindu nao kiongozi wao aseme wanaunga mkono dp kwa sababu zao.
As a great thinker what do you think would happen??
Viongozi wa kuongoza roho za watu. Roho haionekani, ila ni uzima wa kimungu ndani ya watu. Kwa hiyo viongozi wa kiroho huwaongoza watu walio na miili, na maana ya watu wenye miili wanahitaji huduma za msingi za kibinadamu. Viongozi wa kisiasa hushirikiana na viongozi wa kiroho katika kuhudumia hawa raia. Kama viongozi wa kisiana ni wahuni viongozi wa kidini ni wajibu wao kuwashuparia hawa waovu na kuwashinikiza wanasiasa kufuata misingi ya haki katika utendaji na uongozi.
Huwezi kuziongoza roho za watu bila kujali afya zao na maisha yao.
Maaskafu Sio Wananchi? Hao Maaskofu Walipo Kuwa Wanakwenda Ikulu na Sherehe za CCM, Haikua Uchanganyaji wa Siasa? CCM Msibabaishe Wananchi na Ujinga Wenu wa Kutaka Kufunga Midomo Maaskofu na Wapenda Imani Zao. JK Anataka Waislamu Wajione Kama Wakristo Hawampendi JK Kwa Sababu ya Imani Zao. Ujinga Mtupu, Nakumbuka JK Alikuwa Anapenda Sana Sifa za Maaskofu Leo Wamemgeuka kwa Wizi Wake na Sifa Mbaya za Uongozi, Anaanza Chuki Nao. Watanzania Hatuchagui Kiongozi kwa Kuangalia Dini Zao na JK Alipata Kura Nyingi Sana Hawamu ya Kwanza na Sasa Tume Mgundua ni "JK is One of the Corrupt Person in Tanzania and Has Very Very Poor Leadership Skills" It's Over CCM...
Haya umenena ni ukweli mtupu. Tuna safari ndefu sanaItachukua miaka takribani 45 Tanzania kukua kisiasa. Haya tuyaonayo sasa ni mpito tuu