Maaskofu wasiingilie mambo ya siasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maaskofu wasiingilie mambo ya siasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Jan 12, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jan 12, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Idadi kubwa ya vyuo mbalimbali vikiwemo vya ufundi na ualimu vimejengwa na kanisa. Hospitali mbalimbali na zahanati zinaendeshwa na maaskofu. Miradi mbalimbali ya umeme vijijini imeanzishwa na kuhudumiwa na maaskofu.
  Viongozi wengi hapa nchini wamesoma katika shule na vyuo vilivyojengwa na kanisa.

  Nashangaa leo CCM ikisema maaskofu wavue majoho maana yake wafunge shule, vyuo, hospitali, dispensary, nk
   
 2. n

  niweze JF-Expert Member

  #2
  Jan 12, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Maaskafu Sio Wananchi? Hao Maaskofu Walipo Kuwa Wanakwenda Ikulu na Sherehe za CCM, Haikua Uchanganyaji wa Siasa? CCM Msibabaishe Wananchi na Ujinga Wenu wa Kutaka Kufunga Midomo Maaskofu na Wapenda Imani Zao. JK Anataka Waislamu Wajione Kama Wakristo Hawampendi JK Kwa Sababu ya Imani Zao. Ujinga Mtupu, Nakumbuka JK Alikuwa Anapenda Sana Sifa za Maaskofu Leo Wamemgeuka kwa Wizi Wake na Sifa Mbaya za Uongozi, Anaanza Chuki Nao. Watanzania Hatuchagui Kiongozi kwa Kuangalia Dini Zao na JK Alipata Kura Nyingi Sana Hawamu ya Kwanza na Sasa Tume Mgundua ni "JK is One of the Corrupt Person in Tanzania and Has Very Very Poor Leadership Skills" It's Over CCM...
   
 3. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #3
  Jan 12, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Only one who devotes himself to a cause with his whole strength and soul can be a true master. For this reason mastery demands all of a person. Hakuna kurudi nyuma

   
 4. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #4
  Jan 12, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  mkuu uzi wako uko na utata.............

  sasa kwa mfano kama mimi nikiuliza: mashehe na maimamu wamejenga nini? utanijibu nini?
   
 5. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #5
  Jan 12, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,187
  Likes Received: 1,905
  Trophy Points: 280
  CCM $ Co iache ubaguzi kwa raia wa nchi hii ya kushiriki siasa ni Lazima pia haki yao ya msingi na kiraia kwa MAASKOFU Kushiriki siasa kama katiba ya nchi inavyo ainisha anaye wazuia anavunja katiba ASHUGHULIKIWE Kwa mujibu wa Katiba!
   
 6. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #6
  Jan 12, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,187
  Likes Received: 1,905
  Trophy Points: 280
  Washiriki siasa bila kizuizi chochote ni haki yao ya kiraia!
   
 7. k

  killa Member

  #7
  Jan 12, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nafikiri kuna sababu kubwa ya kuuwambia wasiingilie siasa, kwani wao wana ushawishi mkubwa wa kiroho na mtu yuko tayari kufa kwa imani yake ya kiroho kuliko kufa kwa ajili ya CCM au CHADEMA kwani hivi ni vikundi vya mpito tu leo vipo kesho havipo. Ndio maana nchi zote za Demokrasia watu wa dini wanawekwa pembeni washughulikie wafuasi wao kiroho, kama wanataka kuingia kwenye siasa inawabidi waache kimoja.

  Taasisi za kidini zinapewa upendeleo wa kodi kwa ajili ya hili. Sasa kweli wakijiingiza na kuanza kutoa matamshi yasiyokuwa neutral nchi inaweza ikawaka moto, kwani wakijibiwa wasijifanye kwamba hawewezi kukosolewa, nchi itagawanyika kwani Waislamu kamwe haitawaona kuwa wako kupigania interest zao. Tusijidanganye kila mtu anajua viongozi wote wa dini wanataka upande wao ndio uwe mbele awe mkristo au muislamu, sasa awa maaskofu wasipokuwa makini tutageuka Lebanon... Ndiyo maana Nyerere licha kuwa mkatoliki mzuri lakini hakuwaachia maaskofu na mashekhe kuzungumzia siasa na aliondoa sensa ya idadi ya wakristo na waislamu tangu 1967 kwa kuona mbali. Sasa watu wasiokuwa na busara wanataka kuliamsha zimwi ambalo litaiangamiza Tanzania wasipotumia akili. Maaskofu na Mashekhe wanatakiwa kuwa waleta amani katika jamii na sio kuchochea uhasama kutokana na kutofautiana kimawazo kidini au kisiasa .
   
 8. coscated

  coscated JF-Expert Member

  #8
  Jan 12, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 180
  kumbuka mkuu kuwa roho inakaa kwenye mwili
   
 9. A

  ASKOFU MSAIDIZI JF-Expert Member

  #9
  Jan 12, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huyo anayesema maaskofu wasiingilie mambo ya siasa , kwa nini NEC iliwapa kazi ya kisiasa kutoa elimu ya uraia wakati wa uchaguzi 2010 ???
   
 10. k

  killa Member

  #10
  Jan 12, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakupata Muadhamu Askofu Msaidizi, kutoa elimu ya urai si kujingiza moja kwa moja katika dimbwi la ushindani wa kisiasa, kwani kutoa elimu ya urai unasimamia katika ukweli halisi ("based on facts"), malumabano na mashindano ya kisiasa yanasimama katika uwongo (lies), kupindisha ukweli (exaggerations), kashifa (innuendos) na ahadi za uwongo ( false promises) na ubabe wa kweli au tisha toto (literal or metaphoric threats ) na ukweli kidogo.
   
 11. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #11
  Jan 12, 2011
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Nadhani kwa kuanza CCM wasingemteua mama Lwakatare kuwa mbunge.
   
 12. M

  Mesaka Member

  #12
  Jan 12, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 31
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Tunapowaongelea maaskofu tujaribu kuelewa sana kazi zao, Maskofu wanaiongoza na kuihudumia jamii Kiroho na Kimwili maana Huwezi kutenganisha mwili na roho.
  Hivyo wanayo haki ya kuikemea serikali maana Nchi ya MUNGU na serikali huwekwa na MUNGU. Na ukiingia ndani zaidi Rais au kiongozi yeyote wa serikali yu chini ya uangalizi wa viongozi wa kidini. Ndiyo maana machifu na watemi zamani hawakufanya jambo lolote bila baraka za ma priest vinginevyo mambo yalienda ovyo.
   
 13. M

  Mesaka Member

  #13
  Jan 12, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 31
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Dini na serikali ni mikono ya MUNGU kuhudumia watu wake
   
 14. L

  LAT JF-Expert Member

  #14
  Jan 12, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  pia ... roho ndiyo iliyoshawishiwa na shetani.., halafu mwili ( tunda la kati ) ukaliwa
   
 15. Mbaha

  Mbaha JF-Expert Member

  #15
  Jan 12, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 697
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hivi ni nani asijua mchango wa Rev Desmond Tutu katika maendeleo ya nchi yake S.A.????!!! Mnasema viongozi wa dini wana ushawishi mkubwa sawa kama Kiongozi wa kisiasa he is doing right things nani atamkusoa???? Viongozi wa kidini ni viongozi wa kiroho! Lakini roho bila mwili haitawaliki!!!! Ni jukum la viongozi wa dini kuona kuwa wafuasi wao wanakuwa na hali nzuri kimwili (of which is Siasa) ili roho ziwe salama zaidi. After all misikiti au makanisa si vyombo vya dola!!! Ni taasisi zinazo hubiri amani. Kwa hiyo whoever ambae anahatarisha amani lazima akemewe!!!! Hili la ku - exempt viongozi wa dini kwenye siasa mimi linanikera sana!!! Ni kuwanyima haki yao ya kimsimgi viongozi hao, ambao mchango wao wa maendeleo katika jamii ni mkubwa.
   
 16. l

  limited JF-Expert Member

  #16
  Jan 12, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 300
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Sasa Tume Mgundua ni "JK is One of the Corrupt Person in Tanzania and Has Very Very Poor Leadership Skills" It's Over CCM...

  nikweli kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa, kila kona watu wanalalamika, wanamsutumu but he never say a thing, he is just quite like nothing is hapenning.
   
 17. P

  Paul S.S Verified User

  #17
  Jan 12, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Jamani kwa nijuavyo mimi jk nyerere hakuwahi kuruhusu kitu kama hii kamwe, nirahisi kumchagua kiongozi wa dini kuwa kiongozi wa kisiasa kwa elimu yake, na si kuacha viongozi wa dini sasa kuropoka kila kitu bila kujali athari zake kwa jamii.
  Haiwezekani leo hii viongozi wa dini wamegeuka utadhani ngos za akina ananilea nkya, wamesahau kabisa wajibu wao makanisani na misikitini kuwa wanamzigo mzito ktk jamii kwa kuanza kuwaweka sawa waumini wao ktk nyumba za ibada maana hao mafisadi ndio waumini na kondoo zao wanao wachunga huko, na anguko la maadili linaanzia kwao.
  Kadri siku zinavyo kwenda ndio hali inazidi kuwa mbaya imefikia sasa viongozi wa dini wamekuwa watoa matamko kila panapotokea issue kubwa ya kisiasa, pengine kosa lilianza pale jk alipo kaa kimya baada ya kuambiwa yeye ni chaguo la mungu na sasa hao hao wamekuja kumuona mtu alieshindwa kuongoza nchi(si dhani kama Mungu mpuuzi namna hii), nahii ni kuwa ktk siasa hakuna rafiki wa kudumu na ndio maana tunao tazama mbali hatukubaliani na viongozi wa dini kuwa wasemaji wa mambo ya kisiasa. lazima wajue kuwa wao ni tofauti na vyama vya siasa au ngos.
  Mambo ya kidini ni zaidi ya upeo wa kawaida wa mtazamo, ni imani inayogusa hisia kali inayoweza kupelekea hata mtu kufanya mambo ya ajabu.
  Warudi ktk nyumba za ibada na wa play part yao kama viongozi wa dini kwa kuwasimamia vizuri waumini wao wawe bora na watii maana katika hao ndio tutapata viongozi bora toka kwao.
   
 18. k

  killa Member

  #18
  Jan 12, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakupata Mkuu, lakini kumbuka kiongozi wa kiroho anapokuwa hayuko neutral katika ugomvi wa kisiasa na kuunga chama kimoja cha kisiasa hathari zake ni kuwa wafuasi wa dhehebu lakini humfuata kama kondo bila ya kupima hoja na kutumia akili zao wao wenye kupambua mambo kwani wengi wanamchukulia mchungaji kama ndio neno lenyewe, kwahiyo upande unaoungwa mkono na askofu uwambatanishwa na ukweli wa neno wakati hali halisi ni kuwa maaskofu ni kama mimi na wewe wanafanya upenzi kutokana na hisia maslahi yao na wafuasi wao. Sasa kila dhehebu likifanya hivyo kutakuwa hukutawaliki Tanzania. Waislamu watafuata matamshi ya viongozi wao, wakristo na ndio hivyo wamekwisha anza basi nchi itaparaganyika.
   
 19. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #19
  Jan 12, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Huyu mama usimfikirie hata siku moja maana is a two sided person
   
 20. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #20
  Jan 12, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Tatizo CCM likifanyika jambo baya utasikia wanasema watu wasilihusishe na CCM ila Serikali likitokea jambo zuri utasikia CCM wanakwambia hiyo ni moja ya ilani yao iliyoko kwenye chama chao CCM.
   
Loading...