Maaskofu wamshambulia Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maaskofu wamshambulia Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Oct 17, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,918
  Likes Received: 83,432
  Trophy Points: 280
  • Wamuonya asiilipe Dowans kwa vile alishaikana

  na Danson Kaijage, Dodoma
  Tanzania Daima


  MAASKOFU wa Kanisa la Christian Mission Fellowship (CMF), wamesema kitendo cha Rais Jakaya Kikwete, kuendelea kuwakumbatia watuhumiwa wa ufisadi ndani ya serikali yake kinazidi kuwaangamiza Watanzania kwa umaskini.

  Mbali na lawama hizo, pia wamesema kuwa kanisa hilo litaungana na wanaharakati wa kweli na wapenda maendeleo nchini ili kuhakikisha wanaipinga serikali kulipa deni la Dowans la sh bilioni 94.

  Maaskofu hao, walitoa kauli hizo jana mjini hapa wakati wa ibada maalumu ya kumsimika Makamu Askofu Mkuu wa Kanisa hilo nchini, Askofu Dorlinad Mhango, iliyoongozwa na Askofu Mkuu wa CMF, Dk. Mungulu Kilimba.

  Kauli hiyo inakuja siku chache tangu Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, isajili tuzo ya Dowans iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC), ikilitaka Shirika la Ugavi wa Umeme Nchini (TANESCO), kulipa fidia hiyo kutokana na kosa la kuvunja mkataba baina yake ya kampuni ya Dowans Tanzania.

  Askofu Kilimba alisema kuwa inashangaza kuona serikali inaridhia kulipa deni hilo haraka wakati haina fedha za kuendeshea shughuli mhimu za kimaendeleo za kumkomboa Mtanzania anayeishi kwa kipato cha chini ya dola moja kwa siku.

  Alibainisha kuwa kanisa hilo, kamwe halitanyamazia kitendo hicho na hivyo lazima waungane na wanaharakati nchini kuhakikisha wanapinga ulipwaji wa fedha hizo licha ya ICC kutoa hukumu ya kuitaka TANESCO kulipa fidia hiyo.

  "Kamwe viongozi wa dini hatuwezi kunyamaza juu ya hili, kwani tunajiuliza kuna nini hadi serikali iridhie haraka kulipwa kwa fedha hizo wakati kuna matatizo mengi ambayo yanatakiwa kutatuliwa," alihoji askofu huyo na kuongeza:

  "Watanzania wangapi wanaishi chini ya dola moja kwa siku na hawajui hatma ya maisha yao, hawana umeme, huduma za afya ni mbovu halafu inakuwaje serikali iwe tayari kulipa deni la Dowans upesi na kuacha kushughulikia matatizo mengine muhimu? Sisi kama kanisa hapa hatuwezi kunyamaza."

  Aliitaka serikali kuueleza umma wazi wazi ni wapi fedha hizo za kuilipa Dowans zinatoka na zinalipwa kwa nani ikiwa viongozi wote wa juu akiwemo Rais Jakaya Kikwete, walikiri kuwa hawawajui wamiliki wa kampuni hiyo.

  "Jamani ndugu zangu lazima tujiulize kuna nini kati ya serikali na Dowans? Wazee wa Jumuiya ya Afrika Mashariki hadi leo wanaandamana hadi kulala barabarani hawajalipwa madeni yao, lakini leo hii serikali inaharakisha kulipa deni la Dowans, hii haiwezi kukubalika kirahisi na ni haki yetu kuhoji na kuungana na wanaharakati wa kweli wapenda maendeleo kupinga malipo hayo," alisisitiza askofu huyo.

  Katika hatua nyingine, Askofu Kilimba aliwataka watumishi wa kanisa hilo kuhakikisha wanasema ukweli juu ya mambo yanayokwenda kinyume na matarajio ya nchi hasa suala la rushwa, ufisadi na viongozi wa serikali kujilimbikizia mali wakati Watanzania wengi wanakufa kwa umaskini.

  "Viongozi wa dini ni lazima kuikosoa serikali bila woga kwani sisi ndiyo kazi kubwa tunayotakiwa kuifanya, sasa angalia viongozi wa serikali wanavyojichukulia mali pamoja na kuingia mikataba mibovu na kulisababishia taifa janga kubwa la umaskini na madeni. Lazima tupige kelele kwa ajili ya kufanya mabadiliko," alisisitiza Askofu Kilimba.

  Kwa upande wake, Makamu mpya wa Askofu Mkuu, Mhango, alisema kuwa kinachosababisha umaskini nchini ni Rais Kikwete kutokuwa na maamuzi kwa viongozi aliowachagua.

  Askofu Mhango alisema Rais Kikwete ameshindwa kuwa na maamuzi magumu ya kuwawajibisha watendaji wazembe na wale ambao si waaminifu na badala yake amekuwa kinara wa kuwakumbatia.

  "Wapo watumishi wengi ambao amewateua kushika nyadhifa mbalimbali ambao wanatuhumiwa kwa ufisadi lakini Rais amewakumbatia anashindwa kutoa maamuzi magumu kwa lengo la kunusuru nchi katika janga la umaskini uliopindukia.

  "Kuna jamaa zake wengi ambao wanatuhumiwa kwa rushwa lakini amewakumbatia. Pamoja na kutoa misemo ya kujivua gamba lakini hizo ni porojo tu wakati Watanzania wakizidi kuangamia," alisema Mhango.

  Askofu Mhango alisema kwa nafasi yake, atahakikisha anazungumza na serikali kwa kuitaka ijenge viwanda vikubwa na vidogo ambavyo ni vya ndani ili kuepukana na taifa kugeuzwa dampo la kutupa takataka kutoka nje ya nchi.
   
 2. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #2
  Oct 17, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  mie nangojea tamko la bakwata nione litakuwa na mlengo wa kidini au kutetea maslahi ya taifa, tusubiri
   
 3. Atubela

  Atubela JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2011
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 637
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 180
  Ndio hivyo kaka, Kama unaikumbuka hii ya Mh David Kafulila "Serikali legelege ufanya mambo legelege" wakamkomalia wee! lakini ukweli unabaki palepale!
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,918
  Likes Received: 83,432
  Trophy Points: 280
  Wale hata siku moja hawatatoa kauli yoyote ya kumpinga Kikwete ukiondoa ile issue ya mahakama ya Kadhi. Yaani utadhani kama nchi kwenda mrama hakuwagusi kabisa wao. Nimejaribu kutafuta kama Bakwata wameshatoa tamko lolote lile la kupinga malipo ya Dowans lakini sikuambua kitu, labda siku za usoni nao watafanya hivyo.
   
 5. Jakubumba

  Jakubumba JF-Expert Member

  #5
  Oct 17, 2011
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 1,627
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  kila siku matamko tu! Mda umefika tunahitaji matendo. Maaskofu na mapadri na mashehe muandae maandamano nchi nzima tumfukuze jakayaa. Nafikili hapo inakuwa ni nchi nzima imeandamana maana naamini kila mtu ana dini. Matamko hayasaidii bali yanawapa mafisadi njia mbadala ya kuiba.
   
 6. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #6
  Oct 17, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Wanatafuta umaarufu tu.
   
 7. N

  Ngoiva Lewanga Senior Member

  #7
  Oct 17, 2011
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 160
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  one step ahead.
   
 8. c

  chief72 JF-Expert Member

  #8
  Oct 17, 2011
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 567
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Muda wa matamko ushapita,umebaki muda wa vitendo,BAKWATA wao ni kujipendekeza na kujikomba kwa serikali kituambacho ni makosa kwa mujibu wa Qur an na hadth
   
 9. siemens c25

  siemens c25 Senior Member

  #9
  Oct 17, 2011
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 198
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  mapinduzi ya kweli 2015 tunaitaji mshikamano maana kwa mwendo huu wa magamba tutakuwa maskini milele.
   
 10. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #10
  Oct 17, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,151
  Likes Received: 2,113
  Trophy Points: 280
  utashambuliwa kwa tuhuma za udini best
   
 11. THE GAME

  THE GAME JF-Expert Member

  #11
  Oct 17, 2011
  Joined: May 30, 2010
  Messages: 441
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  matamko hadi lini?waumini wote tuingieni barabarani kupinga huu wizi.
   
 12. N

  NASSOR Member

  #12
  Oct 17, 2011
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Maisha yetu,ya watoto wetu, na wajukuu zetu yanategemea uamuzi wetu na matendo yetu ya sasa. Hata humu jf watu ni waongeaji zaidi kuliko vitendo na hata kwenye vitendo tunawaachia watu wachache saana, hatutafika kwa njia hiyo.
  Cha kufanya tupange siku moja tunakutana wapi na tuwe wote tuanze harakati za maandamano ya kweli kuna baadhi yetu tutakufa ili wengine wawe huru.
   
 13. M

  MAJANI YA KUNDE JF-Expert Member

  #13
  Oct 17, 2011
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 213
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  naomba tarehe itajwe tukutane pale jangwani ili tujadili hatima ya nch yetu na vizazi vyetu.niko tayari kulipia vyombo vya muziki kwa ajili ya kutumika siku hiyo pale Jangwani,.
   
 14. MPAMBANAJI.COM

  MPAMBANAJI.COM JF-Expert Member

  #14
  Oct 17, 2011
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 704
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 60
  Alikuja Mwinyi akalaumiwa, akaja Mkapa watu wakasema afadhali Mwinyi, Akaja Kikwete mkasema walau Mkapa kesho mtasema angalau Kikwete. Hapa hata wewe ukipewa shavu utakula tuu. Ufisadi upo palepale lililopo tufanye kazi na viongozi waoneshe njia
   
 15. M

  MAJANI YA KUNDE JF-Expert Member

  #15
  Oct 17, 2011
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 213
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  sijasema afadhali fulani ninachosema tukutane pale jangwani tujadili hatima ya Taifa letu na vizazi vyetu.kogoamano ambalo ahlina sura ya chama chochote yatakayojadiliwa hapo tutajulishana Lakini mloja kubwa ni Wizi,ubadhirifu,ufisadi,rushwa,uwajibikaji,utawala wa sheria,Wapi tunataka kuelekea kesho Tanzania
   
 16. Sniper

  Sniper JF-Expert Member

  #16
  Oct 17, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,944
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Malipo ya Dowans = Mtaji wa CCM kampeni za 2015
   
 17. mchemsho

  mchemsho JF-Expert Member

  #17
  Oct 17, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 3,158
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Kosa lingine kubwa serikali ya CCM chini ya kikwete linafanyika ni kujiweka kando na marumbano ya kidini ambayo sasa yanashika kasi, serikali inakaa kimya kana kwamba haijui athari za machafuko ya kidini. KIKWETE NI MWOGA NA SI JASIRI.
   
 18. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #18
  Oct 17, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Unafikiri Rostam alikubali kupiga kampeni Igunga hivi hivi? ilikuwa ni baada ya kuhakikishiwa malipo yatapita immediately! ndo TZ yetu hiyo na JK hajaesema tena kama sasa amewajua wamiliki wa Dowans ama bado
   
 19. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #19
  Oct 17, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,829
  Trophy Points: 280

  Jamani JK, hawa watu wote wanalalamika kutochukua hatua kwa wasaidizi wako. Sikia kilio cha watu. Wanakupenda sana hawa ndio maana wanasema wazi bila unafiki.
   
 20. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #20
  Oct 17, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  si walisemaga hapo awali kwamba ameteuliwa na Mungu ?Imekuwaje tena?
   
Loading...