Baraka Roman
JF-Expert Member
- Feb 16, 2013
- 692
- 262
Hana lo lote. Hawa ndiyo maaskofu wa Baali. Kiboko yao Eliya.Asanteni maaskofu, msg sent ila sidhani kama itafanyiwa kazi na hawa watu maana vichwa vyao vigumu sana.
Hicho kikundi kipo.kwenye katiba ya Chadema.Viongozi wa dini wafanye tafiti badala ya kupotosha waumini wao
hajatamka hata neno moja kuhusu chadema hapo. au mtu akisema vyama vya siasa anamaanisha chadema?
Nono,Mimi naona tamko la Askofu ni sawa kabisa, na hakuna mahali anakoishutumu CDM. Ujumbe hapa ni uwa vikundi hivi havitajenga amani. Na CCM wakiwa waasisi, ambao wameamua kuvitumia sambamba na polisi kudhuru wananchi wasio na hatia, pale wanapohisi kuwa wamevutiwa na hoja za vyama vya upinzani ndio walengwa namba moja katika hili. Ingekuwa ccm hawatumii Green gurds kuuwa, kuteka, kumwagia tidikai, kuiba kura, kupiga n.k kungekuwa na haja gani ya kuwa na Red brigade? Ingekuwa polisi wanatoa ulinzi na kuhakikisha haki inapatikana kwa wote, kungekuwa wapi na haja ya brigadia hizi?
Saanane usishangae, MWEMA (IGP) Aliwaambia maaskofu na wachungaji waanzishe vikundi vya ulinzi kwenye mihadhara na ibada zao ili kujilinda na wa magaidi. Sembuse CDM yenye malengo mahususi kuchukua madaraka ya nchi? Hii ni kujisahau tu
Askofu KKKT atahadharisha uanzishwaji vikundi vya ulinzi
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Dodoma, Amon Kinyunyu, amesema kitendo cha viongozi wa vyama vya siasa ya kuamua kujianzishia vikundi vya ulinzi wa kujilinda kwenye vyama vyao, ni ishara tosha ya kuhatarisha amani ya Taifa.
Askofu Kinyunyu amesema viongozi wa siasa wanaoanzisha vikundi vya namna hiyo ni kuashiria jinsi gani walivyokosa heshima kwa Mungu na kwa mamlaka ya serikali ambayo ina ulinzi na usalama unaolinda nchi kwa ujumla.
Alitoa kauli hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa miradi ya mifumo ya miundombinu ya watoto ikiwamo ya maji, madarasa na vyoo vya kisasa iliyodhaminiwa na shirika la Compassion International Tanzania kwa kushirikiana na washirika wenza kutoka kwenye Makanisa ya Huduma ya Mtoto iliyofanyika katika viwanja vya Kanisa la Tag Miyuji mjini hapa.
Askofu Kinyunyu alisema kitendo cha vyama hivyo kuanzisha vikundi vya kujilinda, ni ishara ya kuleta machafuko ya amani ya nchi.
Pia alisema kitendo hicho kitawafanya vijana waliopo katika vyama hivyo kuendelea kuchukiana badala ya kupendana.
Alisema viongozi wa kisiasa hawana budi kutambua kuwa kwa kuanzisha vikundi hivyo ni kuzidi kujenga uhasama mkubwa utakaoiumiza jamii isiyohusika wakiwamo watoto, wanawake, wazee na walemavu.
Hapa wanatakiwa kujua kuwa kitendo hicho ni ishara tosha inayoashiria kuanzisha vita ambayo washirika wakubwa ni vijana tunaowategemea kushika madaraka mbalimbali ya kiserikali na ya kisiasa, alisema.
Askofu Kinyunyu amewataka viongozi wa vyama vya siasa kuheshimu amani iliyopo iliyobarikiwa na Mungu tangu kuumbwa kwa ulimwengu.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Compassion Intenrational Tanzania (CIT) hapa nchini, Mchungaji Joseph Mayala, alisema kitendo hicho ni sasa na uwekezaji kwa vijana wawe na roho ya ukatili badala ya upendo na amani.
Source: Home
NB:
..Askofu Mkuu wa KKKT Malasusa naye ametoa kauli inayoelekea kuwananga CDM.
..soma hapa chini:Home
Mwenye macho haambiwi tazama.
Maaskofu wamenena na kauli za Maaskofu huwa siyo za kukurupuka kama wengine watakavyotaka kuwaaminisha watu hapa.
Maneno ya Maaskofu yanadhihirisha ukweli wa maneno ya Rais, IGP na wapenda amani wengine nchini na kikubwa zaidi, kwa nini kauli ya Maaskofu imekuja baada ya CHADEMA kutoa tamko kuhusu Red brigade.
Kuna kitu wamefunuliwa na Mwenyezi Mungu na kukiona kile kilichoko nyuma ya dhamira za CHADEMA kutaka kuanzisha na kukiimarisha kikundi cha ulinzi.
Maaskofu wametimiza wajibu wao kama Mwenyezi Mungu anavyo waasa wakemee maovu katika jamii kwa nguvu zao zote.
Askofu KKKT atahadharisha uanzishwaji vikundi vya ulinzi
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Dodoma, Amon Kinyunyu, amesema kitendo cha viongozi wa vyama vya siasa ya kuamua kujianzishia vikundi vya ulinzi wa kujilinda kwenye vyama vyao, ni ishara tosha ya kuhatarisha amani ya Taifa.
Askofu Kinyunyu amesema viongozi wa siasa wanaoanzisha vikundi vya namna hiyo ni kuashiria jinsi gani walivyokosa heshima kwa Mungu na kwa mamlaka ya serikali ambayo ina ulinzi na usalama unaolinda nchi kwa ujumla.
Alitoa kauli hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa miradi ya mifumo ya miundombinu ya watoto ikiwamo ya maji, madarasa na vyoo vya kisasa iliyodhaminiwa na shirika la Compassion International Tanzania kwa kushirikiana na washirika wenza kutoka kwenye Makanisa ya Huduma ya Mtoto iliyofanyika katika viwanja vya Kanisa la Tag Miyuji mjini hapa.
Askofu Kinyunyu alisema kitendo cha vyama hivyo kuanzisha vikundi vya kujilinda, ni ishara ya kuleta machafuko ya amani ya nchi.
Pia alisema kitendo hicho kitawafanya vijana waliopo katika vyama hivyo kuendelea kuchukiana badala ya kupendana.
Alisema viongozi wa kisiasa hawana budi kutambua kuwa kwa kuanzisha vikundi hivyo ni kuzidi kujenga uhasama mkubwa utakaoiumiza jamii isiyohusika wakiwamo watoto, wanawake, wazee na walemavu.
Hapa wanatakiwa kujua kuwa kitendo hicho ni ishara tosha inayoashiria kuanzisha vita ambayo washirika wakubwa ni vijana tunaowategemea kushika madaraka mbalimbali ya kiserikali na ya kisiasa, alisema.
Askofu Kinyunyu amewataka viongozi wa vyama vya siasa kuheshimu amani iliyopo iliyobarikiwa na Mungu tangu kuumbwa kwa ulimwengu.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Compassion Intenrational Tanzania (CIT) hapa nchini, Mchungaji Joseph Mayala, alisema kitendo hicho ni sasa na uwekezaji kwa vijana wawe na roho ya ukatili badala ya upendo na amani.
Source: Home
NB:
..Askofu Mkuu wa KKKT Malasusa naye ametoa kauli inayoelekea kuwananga CDM.
..soma hapa chini:Home
Kwanini aseme wakati huu ambapo CDM imeweka wazi kujilinda baada ya polisi kutowatendea haki.Labda kama ameyasema hayo wakati anasimikwa kuwa askofu tutamsamehe kwa kuwa ndo kwanza anaanza kazi, lakini kama alikuwepo hakuna namna ya kumtenganisha na wanafiki wengine.hajatamka hata neno moja kuhusu chadema hapo. au mtu akisema vyama vya siasa anamaanisha chadema?