Ukisoma biblia utawaona watumishi wa Mungu wa kweli walivyofanya kazi ya Mungu bila upendeleo hata wengine iliwaghalimu maisha yao kwa kuwakosoa watawala pale walipokosea,soma habari za Yohana mbatizaji,Yeremia,Daniel,Yohana aliyeandika kitabu cha ufunuo na wengine wengi,Walisimamia kweli bila kujali cheo au mamlaka ya mtu aliyokuwa nayo bali walipeleka ujumbe wa Mungu kama ulivyo na Mungu aliwatetea kwa uweza wake.
WAKO WAPI WATUMISHI WA NAMNA HII KTK KIZAZI HIKI?
Watumishi wa siku hizi wanaangalia upepo unasemaje wasije wakawaudhi watawala wakawagomea kwenda kwenye harambee za majengo ya ibada.Hii imesababisha heshima za watumishi kushuka na ndo maana wengine wamehusishwa na kashfa za madawa ya kulevya maana tabia ya Ki-Mungu ndani yao haijitokezi nje ili waumini wao waione.
Ni kawaida siku hizi kusikia kiongozi wa dini kafungiwa mlango wa nyumba ya ibada na waumini wake,mara kamwagiwa tindikali, mara kanisa limechomwa moto na mengine mengi,na Mungu hawaadhibu wanaofanya hayo,hii inatokana na nyumba za ibada kupigwa IKABODI(utukufu wa Mungu kuondoka) kwa sababu ya maasi ya makuhani wanaosimama kwenye madhabahu hizo kuwa ndumilakuwili,hawamtumikii Mungu bali wanaangalia nani kasema,anatoa sadaka kiasi gani na hivyo kutoa hukumu zilizopotoka.Viongozi wa dini wajitafakari upya na kuchagua kumtumikia Mungu au mamoni.