Maaskofu wa Pentekoste wapinga kukaguliwa na Serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maaskofu wa Pentekoste wapinga kukaguliwa na Serikali

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by nngu007, May 5, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 5, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Imeandikwa na Shadrack Sagati; Tarehe: 5th May 2011

  MAASKOFU na wachungaji wa makanisa ya Pentekoste nchini, wamepinga hatua ya Serikali ya kuwalazimisha kuwasilisha hesabu zao za kila mwaka kwa Wizara ya Mambo ya Ndani wakati hawapewi ruzuku na mamlaka yoyote ya kiserikali.

  Wakizungumza katika chakula cha pamoja cha usiku, Mchungaji wa Kanisa la Maombezi GRC Ubungo Kibangu, Anthony Lusekelo na Askofu wa Kanisa la Christian Mission Fellowship, Dk. Mgullu Kilimba, walisema kitendo hicho ni uonevu kwa makanisa hayo.

  Chakula hicho kilichoandaliwa juzi kilihusisha wachungaji wa makanisa mbalimbali ya Pentekoste yaliyoko mjini Dar es Salaam kwa lengo la kudumisha umoja miongoni mwao na kuelezana namna ya kuwahamasisha waumini wao washiriki katika masuala mbalimbali ya kitaifa.

  “Sisi hawatupi ruzuku kwa nini watudai return (mapato na matumizi) ya hesabu za kanisa…hii sheria ni kandamizi na lazima tuipinge kupitia Katiba mpya,” alisema Mchungaji Lusekelo.

  Kwa mujibu wa Sheria namba 337 ya mwaka 1954 ambayo ilifanyiwa marekebisho mwaka 2002, Wizara ya Mambo ya Ndani kupitia kwa Msajili wa Vyama vya Kijamii, ina mamlaka ya kuandikisha vyama vya kijamii.

  Chini ya sheria hiyo, makanisa na vyama vingine vya kijamii vinatakiwa kuwasilisha hesabu zake za mapato na matumizi kwa msajili wake kila mwaka.

  Ni sheria hiyo ambayo Mchungaji Lusekelo aliwaambia wachungaji kuwa ina upungufu kwani kitendo cha kutakiwa kupeleka hesabu wakati hupewi ruzuku ni unyanyasaji unaofanyiwa makanisa.

  Kutokana na unyanyasaji huo kwa mujibu wa madai yao, viongozi hao wamehamasishana kupinga sheria hiyo wakati wa mchakato wa kujadili Katiba mpya.

  Mchungaji Lusekelo alitaka Serikali ijenge heshima kwa makanisa hayo ambayo alidai yana waumini zaidi ya milioni tatu nchi nzima.

  “Hivi sisi tunaokoa ndoa ngapi zisivunjike? Vibaka wangapi wanaacha kuiba kutokana na mahubiri yetu?” Alihoji Mchungaji huyo.

  Makanisa hayo yamekuwa yakipata fedha za michango, sadaka na zaka kutoka kwa waumini wao, lakini pia yamekuwa yakipata misaada mbalimbali kutoka nje ya nchi ambayo Mchungaji Lusekelo, alisema fedha hizo za wafadhili zinachangia kuwasambaratisha.

  “Hizi fedha ambazo makanisa yanapata kutoka nje kwa wafadhili, ndio chanzo cha kutuvuruga, mchungaji hapa kanisa lake likipata ufadhili tu vurugu zinaanza, jambo hili kwa kweli sio zuri,” alisema Mchungaji huyo.

  Kiongozi huyo wa kiroho pia aliwataka wachungaji wa makanisa hayo kuhamasisha waumini wao kuombea mjadala wa Katiba mpya ili kusizuke ghasia na fujo wakati wa mchakato wa kuelekea kuipata Katiba hiyo.

  Katika eneo ambalo Mchungaji Lusekelo alitaka waumini wa makanisa hayo waliboreshe ni kupinga Rais kuteua na kuunda Tume ya Uchaguzi ambayo alisema inafanya kusiwepo uchaguzi huru na wa haki.

  “Tunahitaji tume huru ambayo Rais ajue kuwa akiboronga anaweza kuondolewa kwa sanduku la kura, hii ya sasa hivi inaonekana kama ya mchezaji na mwamuzi wakati huo huo, haki haiwezi kutendeka,” alidai Mchungaji Lusekelo.

  Kwa upande wake, Dk. Kilimba, alitoa mwito kwa wachungaji hao kuhamasisha waumini wao kufanya maombi ili mchakato huo wa Katiba mpya usitawaliwe na jazba wala vurugu.

  “Hii ni nchi yetu sote sio ya chama fulani, tuliombee Taifa letu na rasilimali zetu ili zitumike vizuri kwa manufaa ya nchi yetu,” alisema Dk. Kilimba. Wachungaji hao pia wameazimia wakati wa mchakato wa Katiba mpya kupinga kipengele cha sheria kinachoyataka makanisa kusajiliwa kama zinavyosajiliwa kampuni nyingine.

  Walisema Tanzania inawahitaji wachungaji waisaidie kwani hali ya kisiasa imebadilika kutokana na kuwepo mwamko mkubwa wa kisiasa kutoka kwa vijana na wasomi.

  “Upepo huu wa kisiasa ni mkubwa hivyo sisi wachungaji kazi yetu ni kuomba upepo huu usisababishe vurugu na fujo katika nchi yetu,” alisema Lusekelo.

  Pia aliwataka wachungaji hao kusimama kidete wakati wa mchakato wa Katiba mpya wasibaguliwe kama ambavyo imekuwa siku za nyuma.

  Alisema licha ya walokole kuwa zaidi ya milioni tatu nchini, lakini wachungaji wao hawapewi hata vipindi kwenye vyombo vya habari vya Serikali kama inavyofanyika kwa madhehebu mengine.
   
 2. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #2
  May 5, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  source?
   
 3. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #3
  May 5, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Nadhani kunahitajika uwajibikaji wa kila mtu, sioni kuna tatizo gani kwa makanisa kuwasilisha mahesabu yao kama hawana kitu wanachoficha.

  Katika zama hizi lolote linawezekana na kuweka kipengele kinachokataza uwajibikaji wa raia ni sawa sawa na kuwa na kipengele kinachozuia mambo fulani yasijadiliwe... kama serikali haitayasajiri (makanisa na vikundi vingine vya kidini) hakuna atakaye yawajibisha kwani hakutakuwa na sheria ya kuwabana na matokeo yake wahuni wanaweza kuyatumia kuendesha mambo yao ya kishetani kwa kisingizio kuwa ni dini!
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  May 5, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Maaskofu hao wamekwenda kinyume cha ukweli kwa kukataa kukaguliwa matumizi ya pesa.
  Pesa zinazotolewa na waamini kama sadaka pamoja na zile za misaada toka nje na dani ya nchi ni kama pesa ya walipa kodi, na hivyo wakati mwingine huwa hakuna mchanganuo wa wazi juu ya mapato na matumizi sahihi ya pesa makanisani. Tujue watumishi wa makanisa ni binadamu wenye madhaifu kama wengi wetu walivyo, ni bora kuwepo na mfumo wa uangazi wa utandawazi wa pesa za kanisa.

  Baadhi ya nchi pesa ambazo waamini wanachangia sadaka zinapata hadhi ya tax na hivyo hurudishiwa pesa hizo na serikali katika tax return ya mwisho wa mwaka kutokana na pesa hizo kufanya kazi za kuhudumia jamii katika elimu, afya nk.

  Hivyo hoja ya Maaskofu hao haina uzito na ni kwa ajili ya kuficha uwazi wa matumizi halali ya pesa hizo.
   
 5. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #5
  May 5, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Wanogopa nini?

  Source si michango ya waumini tu full stop hamna maswali!
   
 6. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #6
  May 5, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Mbona wanapotaka viwanja vya kujenga kanisa wanaomba serikali iwape bure?
  Halafu serikali kama sikosei imewapo udhuru wa kutolipa kodi wa ardhi ya viwanja, hivyo ni sahihi kuchunguzwa
   
 7. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #7
  May 5, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kama kweli wamesajiliwa, wanawatumikia watu na kupokea michango/sadaka kutoka kwa watu wa serikali hii, ni vizuri wakawa wawazi katika mapato na matumizi ya mapato yao. Kama wanatangaza kanisani mapato na matumizi yao ya kila juma, inakuwaje vigumu kupeleka tu haya maelezo kwa mkaguzi wa serikali? Kupinga kwa nguvu sana kunanitia wasiwasi katika mapato na matumizi ya makanisa haya.
   
 8. Khakha

  Khakha JF-Expert Member

  #8
  May 5, 2011
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 2,983
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kutoa sadaka iwe kanisani au msiktini ni sawa na tunavyolipa kodi serikalini. Mwisho wa siku lazima ijulikane pesa hizo zimetumikaje. Wachungaji hapa naona wamechemka. Uzuri zaidi ishu hii ipo kisheria
   
 9. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #9
  May 5, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Kwa mujibu wa Sheria namba 337 ya mwaka 1954 ambayo ilifanyiwa marekebisho mwaka 2002, Wizara ya Mambo ya Ndani kupitia kwa Msajili wa Vyama vya Kijamii, ina mamlaka ya kuandikisha vyama vya kijamii. Chini ya sheria hiyo, makanisa na vyama vingine vya kijamii vinatakiwa kuwasilisha hesabu zake za mapato na matumizi kwa msajili wake kila mwaka.

  Hata hivyo maaskofu na wachungaji wa makanisa ya Pentekoste nchini, wamepinga hatua ya Serikali ya kuwalazimisha kuwasilisha hesabu zao za kila mwaka kwa Wizara ya Mambo ya Ndani wakati hawapewi ruzuku na mamlaka yoyote ya kiserikali. Wanasema kitendo hicho ni uonevu kwa makanisa hayo.

  Wanadai kuwa kwa vile hawapati ruzuku toka serikalini kwa nini serikali iwadai return (mapato na matumizi) ya hesabu za kanisa? Wafikiri hii sheria ni kandamizi na lazima ipingwe kupitia Katiba mpya.

  Akina Rev Fr Masanilo wana kazi kubwa. Sijui ameshapeleka mapato na matumizi ya kanisa lake wizara ya mambo ya ndani?
   
 10. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #10
  May 5, 2011
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Zamwizi Arobaini..
   
 11. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #11
  May 5, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,959
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  Mi nishaacha kusali. Wizi mtupu
   
 12. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #12
  May 5, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,496
  Likes Received: 19,903
  Trophy Points: 280
  hapa si kuna thread zilikuwa zinasema kuwa serikali inawapa makanisa pesa? mbna wanadai kuwa hawapewi? vipi?
   
 13. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #13
  May 5, 2011
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Makanisa yalisharubuniwa na Freemasons wakakubali kutenganisha dini na siasa.Hili lilikuwa pigo na kosa kubwa kwa kanisa. The Freemasons knew kwamba kama kanisa lisingetenganishwa na siasa ujinga wao usingefanikiwa kamwe.I am warning the Church.He ni last attempt ya Freemasons who now control the government kulikamata kanisa.Kama kanisa likikubali accouts zao kuwa audited na serikali,the game will be over. Itakuwa na maana sasa kwamba Freemasons wamelikamata kanisa 100%.
   
 14. M

  Mchapakazi Member

  #14
  May 5, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 67
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kama ni wasafi wka nini wanaogopa kupeleka mahesabu yao?
  Kama serikali ina jukumu la kuratibu pesa zinazokusanywa na vyama vya kijamii makanisa yakiwepo. Hii biashara ya kutumia makanisa kufanya money laundering haina nafasi.
  Sheria ni msemeno kama kanisa halileti mahesabu yake ya mapato kama inavyotakikana linafutwa kwe usajili na misamaha yote ya kodi inakoma. Misaada yao ikija inachapwa tax kama kawaida maana wanachoonyehsa ni kuwa wapo kimaslahi zaidi.
  Kuna wachungaji wanatumia makanisa yao vibaya kujilundikia mali na kuwanyonya waumini ambao wanaishi maisha ya shida ni bora tujue walichopata ili waumini waweze kuhoji matumizi.
  Kaazi kweli kweli
   
 15. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #15
  May 6, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kuna baadhi ya Makanisa na mashirika ya dini hufanya hivyo kila mwaka. Hupeleka riport ya mapato na matumizi kwa Certified odita na huyo baada ya kusafu mahesabu hupeleka nakala serikalini. Moja ya shirika la dini Katoliki nimeshuhuda wakifanya na wanajua ni wajibu. Nashangaa makanisa mengine kama wanapinga sheria ya nchi.
   
 16. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #16
  May 6, 2011
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Hivi wanapewa bure? Au wanapewa kwa upendeleo kama ni kwa ajili ya shughuli ya kijamii? Mimi sijui. Ila mahesabu ni lazima watoe, maana hata mataifa makubwa kama Marekani wanatakiwa kufanya hivyo.
   
Loading...