Maaskofu ndio wasaliti

Maaskofu ndio wasaliti

musami

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2011
Posts
1,434
Reaction score
460
Tokea Kardinali Pengo atoe kauli ya kupinga mapendekezo ya Maaskofu juu kura ya hapana kwa katiba inayopendekezwa,amekuwa akiitwa msaliti hata kufikia kutukanwa na akina Gwajima, lakini nionavyo mimi wasaliti ni maaskofu.

1. Wameusaliti wito wao wa kuutangaza Ufalme wa Mungu badala yake wamekaa wakipoteza muda kuujadili ufalme wa duniani Luka 9:2 Yohana 18:36 labda watuambie wameongozwa na andiko gani

2. Wamesaliti umoja wa Taifa la Tanzania maana unapotoa tamko la wakristo kupiga kura ya hapana unawaambia nini watu wa imani nyingine?je na wao wakikutana kupiga kura ya ndio,mustakabari wa Taifa utakuwaje?

3. Je huu sio mwanzo wa kutumia umoja huu kufanya kampeni za viongozi wanaoona wao wanafaa kuongoza kipindi cha uchaguzi?

4. Makanisa yanahusisha watu kutoka makundi mbalimbali, wapo wanaoipinga katiba inayopendekezwa na wapo wanaoikubali,je huu sio mwanzo wa kukaribisha migogoro ya kiitikadi ndani ya makanisa.

Mungu atusaidie...
 
Kwa hiyo wewe unakubali serikali inavyoipigia debe katiba? Serikali yenyewe ina ajenda gani inapowaambia watu wapige kura ya NDIYO? Kwa nini serikali wasitoe tu uhamasishaji wa kusoma katiba wakawaacha watu kuamua wenyewe? Mifano halisi ninayo. Waziri Mh Mary Nagu juzi kati alikuwa na wamasai akawaambia hii katiba ni nzuri wapige kura ya NDIYO (Hiyo ni kampeni ya serikali) Makamu wa pili wa rais kule Zanzibar naye hivi majuzi kule Zanzibar aliwaambia wananchi kuwa wapige kura ya NDIYO. (Pia hiyo ni kampeni ya serikali)

Sasa inakuwaje vibaya Maaskofu kuwaambia waumini wao wapige kura ya HAPANA wanapoona inatakiwa kuwa hivyo? Jamii forum ni ya watu wenye akili wanaoweza kuchambua mambo lakini nasikitika kuona watu wengi wanashindwa kuielewa vizuri hii nchi yetu. Tukubaline hapa kama Maaskofu wamekosea basi na serikali ishakosea zamani na hakuna wa kumlaumu mwenzie..
 
Mimi ni Roman Catholic lakini hawa maaskofu wamenifanya niufikirie mara mbili mbili huu ukatoliki wangu.

Kwanini hawa maaskofu watudharau kwa kiasi hiki? Yani wametuona sisi ni ma-Robot tusioelewa chochote hadi tuelekezwe cha kufanya?

Hawa maaskofu kwa akili zao wanadhani Mungu alishindwa kutufanya ma-Robot tufanye anayoyataka yeye tuepukane na haya mateso ya hii Dunia?

Wamenikera sana hao maaskofu.
 
nampendayeye

Kwa hiyo unafurahi kuona kanisa linashindana na serikali?ni ukristo wa wapi huo? Rumi 13:1
 
Last edited by a moderator:
Mimi ni Roman Catholic lakini hawa maaskofu wamenifanya niufikirie mara mbili mbili huu ukatoliki wangu.

Kwanini hawa maaskofu watudharau kwa kiasi hiki? Yani wametuona sisi ni ma-Robot tusioelewa chochote hadi tuelekezwe cha kufanya?

Hawa maaskofu kwa akili zao wanadhani Mungu alishindwa kutufanya ma-Robot tufanye anayoyataka yeye tuepukane na haya mateso ya hii Dunia?

Wamenikera sana hao maaskofu.
wewe ni Roman hamia Ugiriki. Huku umepotea eneo, unakasirishwa na maaskofu ndivyo walivyo!
 
Mimi ni Roman Catholic lakini hawa maaskofu wamenifanya niufikirie mara mbili mbili huu ukatoliki wangu.

Kwanini hawa maaskofu watudharau kwa kiasi hiki? Yani wametuona sisi ni ma-Robot tusioelewa chochote hadi tuelekezwe cha kufanya?

Hawa maaskofu kwa akili zao wanadhani Mungu alishindwa kutufanya ma-Robot tufanye anayoyataka yeye tuepukane na haya mateso ya hii Dunia?

Wamenikera sana hao maaskofu.

Unakereka bure tu mkuu, huenda hujui kazi za maaskofu. Kama unaamini askofu hawezi au hana wajibu wa kukuelekeza cha kufanya sijui huwa anafuata nini kanisani kama kweli wewe ni mkatoliki!!
 
kwa hiyo unafurahi kuona kanisa linashindana na serikali?ni ukristo wa wapi huo?Rumi 13:1

Mimi hapo sioni ushindani wowote. Mbona serikali hiyo hiyo inahimiza viongozi wa dini kuwalea watu wake katika maadili na kupelekea nchi kupata viongozi wazuri? Huwezi kutenganisha dini na serikali. Utasali wapi kama hakuna amani? Hapa Maaskofu walimaanisha kuikubali katiba hii ni sawa sawa na kutenda dhambi kwa maana wanajua hii katiba itaathiri vizazi miaka mingi mbele na hii dhambi itatokana na maamuzi ya leo.

Tukubaliane hivi, serikali ikiipigia kampeni hii katiba ili ipite acha na wengine waipinge. Kwanini serikali inalazimisha watu kuipigia kura ya NDIYO hii katiba? Nijibu hilo swali langu ndo nitaendelea kuchangia hii thread.
 
Mimi ni Roman Catholic lakini hawa maaskofu wamenifanya niufikirie mara mbili mbili huu ukatoliki wangu.

Kwanini hawa maaskofu watudharau kwa kiasi hiki? Yani wametuona sisi ni ma-Robot tusioelewa chochote hadi tuelekezwe cha kufanya?

Hawa maaskofu kwa akili zao wanadhani Mungu alishindwa kutufanya ma-Robot tufanye anayoyataka yeye tuepukane na haya mateso ya hii Dunia?

Wamenikera sana hao maaskofu.

Ufikirie mara.mia pia Utanzania wako....serikali yako inavyohamasisha kuipigia kura ya ndio katiba pendekezwa wapo sahihi?
 
Mimi ni Roman Catholic lakini hawa maaskofu wamenifanya niufikirie mara mbili mbili huu ukatoliki wangu.

Kwanini hawa maaskofu watudharau kwa kiasi hiki? Yani wametuona sisi ni ma-Robot tusioelewa chochote hadi tuelekezwe cha kufanya?

Hawa maaskofu kwa akili zao wanadhani Mungu alishindwa kutufanya ma-Robot tufanye anayoyataka yeye tuepukane na haya mateso ya hii Dunia?

Wamenikera sana hao maaskofu.

Na lingine ni kuwa, hawakutushirikisha! Wangeanza from bottom up, not from top bottom.
 
Unakereka bure tu mkuu, huenda hujui kazi za maaskofu. Kama unaamini askofu hawezi au hana wajibu wa kukuelekeza cha kufanya sijui huwa anafuata nini kanisani kama kweli wewe ni mkatoliki!!
Amekuambia yeye ni ROMAN CATHOLIC kwa hiyo usione ajabu kwa anayoyasema.Yuko Tz by accident!
 
Katiba ya nchi inatakiwa kuamuliwa na wananchi maaskofu wako saw a kabisa kuwaelekeza cha kufanya waumini wao sababu wao(maaskofu) wameshaona mbali kuhusu katiba natoa pongezi nyingi sana kwa jopo hilo la maaskofu
 
Mimi ni Roman Catholic lakini hawa maaskofu wamenifanya niufikirie mara mbili mbili huu ukatoliki wangu.

Kwanini hawa maaskofu watudharau kwa kiasi hiki? Yani wametuona sisi ni ma-Robot tusioelewa chochote hadi tuelekezwe cha kufanya?

Hawa maaskofu kwa akili zao wanadhani Mungu alishindwa kutufanya ma-Robot tufanye anayoyataka yeye tuepukane na haya mateso ya hii Dunia?

Wamenikera sana hao maaskofu.

ukatoliki wako n wamashakamashaka hv hujui kuwa maaskofu nao ni sehem ya jamii hivyo nao wana wajib mkubwa wa kuielimisha,kuiadilisha na hata kuikosoa jamii pale inapotokea kuna mambo ya hovyohovyo ktk hyo jamii
 
Mimi ni Roman Catholic lakini hawa maaskofu wamenifanya niufikirie mara mbili mbili huu ukatoliki wangu.

Kwanini hawa maaskofu watudharau kwa kiasi hiki? Yani wametuona sisi ni ma-Robot tusioelewa chochote hadi tuelekezwe cha kufanya?

Hawa maaskofu kwa akili zao wanadhani Mungu alishindwa kutufanya ma-Robot tufanye anayoyataka yeye tuepukane na haya mateso ya hii Dunia?

Wamenikera sana hao maaskofu.

hiyo ID yako inaendana na mawazo yako.halafu wewe siyo mkatoliki kwa jinsi pointi yako isivyokuwa na mantiki.Mkatoliki kamili anajua ni kwanini ni muhimu kufuata maelekezo ya Maaskofu.
 
Katiba ya nchi inatakiwa kuamuliwa na wananchi maaskofu wako saw a kabisa kuwaelekeza cha kufanya waumini wao sababu wao(maaskofu) wameshaona mbali kuhusu katiba natoa pongezi nyingi sana kwa jopo hilo la maaskofu
safi kabisa,wewe kweli umekomaa kiimani.
 
musami

maandiko hayana maana km unavyofikiria wewe,hivi Maaskofu wakitulia pasipo kusema chochote huku mambo yanaharibika,kesho na kesho kutwa nchi isipokalika huo Ufalme wa Mungu watauhubirije?,Na je watu wakianza kukimbia machafuko huo Ufalme wa Mungu watamhubiria nani??? KAA FIKIRI KWA KINA.
 
Kwa hiyo wanaipinga hii katiba ili wawe na mazingira mazuri ya kuhubiri injili au ni misukumo ya kidunia?hivi hapa nchini tukianza kufanya maamuzi kwa misingi ya kiimani,tutakuwa tunalipeleka wapi hili Taifa,uoni kama hawa maaskofu wanatutengenezea Bomu?
 
kuwa makini ndugu yangu! kwenye tamko lao hawajasema kuwa msimamo huo ni wa kidini,halafu tambua kuwa kiongozi yeyote wa Dini ana wajibu wa kuwaelekeza watu wake hata ktk mambo ya kimwili,maana mwili na Roho hutegemeana,usiwe mtumwa wa watawala wabovu.
 
Kanisani sio sehemu za kujadili katiba hayo mambo yafanyeni mitaani kwenu,Mkiendelea hivi na hoja dhaifu kwamba mnapaswa mjadili na mambo ya kimwili ipo siku mtajadili na mechi za simba na yanga kanisani
 
kuwa makini ndugu yangu! kwenye tamko lao hawajasema kuwa msimamo huo ni wa kidini,halafu tambua kuwa kiongozi yeyote wa Dini ana wajibu wa kuwaelekeza watu wake hata ktk mambo ya kimwili,maana mwili na Roho hutegemeana,usiwe mtumwa wa watawala wabovu.

Tatizo Lako Mkuu Bado Hujamuelewa Vizur MUSAMI Kwa Ufupi ilitakiwa Maaskofu Wakae Pamoja Na Mashekhe Wajadil Msimamo Wao Ndo Wautoe Hadharani. Lakin Kusema Maadhimio Ya Maaskofu Tz Ni ... Juu Ya Katiba. Swali, Je Masheikh Nao Wakija Na Msimamo Wao Kinyume Na Maaskofu Huoni Kama Itatokea Balaa Kubwa?.
 
Back
Top Bottom