Waraka wa Maaskofu KKKT: Tunasikitishwa na matukio ya kupotezwa watu, kubanwa kwa Uhuru wa Mahakama, Bunge na Tume ya Uchaguzi...

Hivi hii taarifa imetayarishwa na Chadema nini?? Mbona maneno mengi ndiyo yale yale yanayotumiwa na Chadema??

Aaah nilikuwa nimesahau kuwa KKKT waliombwa na Lowassa wamchague kwa kuwa ni zamu yao kuongoza nchi hii. Okay tumewasikia na kuwaelewa!




Nenda kasome waraka wa RC.

Yani CCM kila taasisi inainyooshea Vidole bado waislam tunasubiri waraka wao.
 
Nyinyi makada wa Lumumba, viongozi wa dini wakitoa tamko la kuukosia huu utawala wa awamu ya 5 mnawaita Chadema

Lakini hapo hapo Mwenyekiti wenu haishi kuwaomba viongozi hao hao wa dini wamuombee

Hivi inawezekanaje uwaombe viongozi wa dini wakuombee, halafu viongozi hao hao wanapokwambia utubu, unawaletea watu wa TRA wakuchunguze kwa "kulazimisha" makosa??
Kwani anaposema wamuombee anawaambia viongozi wa kiprotestants? Yeye anawaambia viongozi wa dini anayoabudu acheni kujipendekeza, sisi tunamuombea kila siku, na akiona amekosea Mungu anatubu kwa utaratibu wa kanisa analoabudu nyie mdeal na waumini wenu kama akina Lwsa, Sumye, Mbwawe n.k.Mh raisi kwa maswala ya imani siyo muumini wenu.
 
Pamoja sana Brother Informer. Nadhani kuna tatizo mahala kwani ukiona hadi Viongozi wa Dini wana wasiwasi hivi na wanakazania jambo fulani jua kuna la maana, ila kinachonisikitisha sana ni kwamba sijui Viongozi wa Kiislamu wa nchi hii wao macho yao hayaoni kama ambavyo hawa Viongozi wa Kikristo wanavyoona! Inasikitisha mno.
 
Safi sana viongozi wa KKKT

Kwa tamko hili mmeonyesha uzalendo wa hali ya juu kwa nchi yenu

Tunapaswa watanzania wote bila kujali itikadi zetu za kisiasa, tuhakikishe tunapaza sauti zetu kwa nguvu zetu zote kuhakikisha kuwa utawala huu unarejea kwenye utawala wa Katiba, na siyo utawala wa kutoa matamko kwenye majukwaa ya kisiasa na kuhesabika kuwa matamko hayo kuwa sheria
Nukuu: kiongozi mzalendo haiwezi Kuwa mmbadala wa katiba
 
Hivi hii taarifa imetayarishwa na Chadema nini?? Mbona maneno mengi ndiyo yale yale yanayotumiwa na Chadema??

Aaah nilikuwa nimesahau kuwa KKKT waliombwa na Lowassa wamchague kwa kuwa ni zamu yao kuongoza nchi hii. Okay tumewasikia na kuwaelewa!
Mbona usemi umefanana na waraka wa kanisa katoliki uliyotelewa majuzi !!?? Sana sana tunasubiri waraka wa Waislam na makanisa mengineyo kanisa la Pentekoste natumaini ule waraka wa Kakobe unatosha .
 
Ngumu kumeza hii kwa walengwa lakini wanasema sikio la kifa halisikii dawa. Maana yake ninini kama umeshakua sikio la kufa yaani sikio lisilopona, basi tutarajie kutokusikia dawa, na kwa namna hii tutarajie pia mwisho usio mwema.
 
Tukubaliane na ukweli mchungu.

Kuna watu hawajui hata washike wapi, walianza wale maaskofu wa Wakatoliki, wamekuja hawa wa KKKT. Tuseme wote ni wapinzani?

Kuna watu wako radhi kutukana hata wazazi wao ili kutetea uovu!
 
Back
Top Bottom