Wengi wetu tumejikuta kwenye mahusiano yaliyotuletea machungu na hata wengine kufikia kujuta sana na kukosa hamu ya maisha au hamu ya kuwa na mahusiano tena hapa duniani. Wenzi wetu wanakuwa na tabia zisizovumilika na tunabaki kuwalaumu kuwa wamebadilika sana, mwanzoni hawakuwa hivyo, au tunajilaumu sisi wenyewe kuwa tulikuwa tunafikiria nini wakati tunaamua kuwachukua.
Katika pita pita zangu za kwenye vitabu leo nimekutana na kitabu cha Barbara de Angelis kinaitwa Are you the one for me? Kina mambo mengi kuhusu mahusiano ya wapenzi na wanandoa lakini kuna kipengele kimoja kimenigusa zaidi. Kipengele hiki kinaongelea makosa makubwa 6 tunayoyafanya mwanzoni mwa mahusiano ambayo kama tungeyazuia basi tungeweza kupunguza kama si kuondoa majanga kwenye mahusiano. Nitayataja yote kama yalivyoandikwa kwa kingereza 6 kisha nitatoa mfano wangu kwa kosa la pili la 2. La 1, 3, 4 na 6 yamenigusa pia lakini sitayaongelea kibinafsi ila mnaweza pia kuchangia.
1. 1. We dont ask enough questions
2. 2. We ignore warning signs of potential problems
3. 3. We make premature compromises- changing or editing your own values, behaviours, and habits in hopes that your new partner will appear to get along more harmoniously.
4. 4. We give in to Lust Blindness
5. 5. We give in to material seduction
6. 6. We put commitment before compatibility
Sasa hilo kosa la pili hapo la kudharau alama za onyo/tahadhari ndo napenda niwashirikishe na kila mmoja aangalie na alihusianishe na mahusiano yake yaliyopita au aliyoko sasa. Nia yangu ni kutaka tutafakari na kuchukua muda kufanya maamuzi sahihi kwenye mahusiano kama tunavyofanya tunapotaka kununua viwanja, magari na hata viatu.
Katika kulielezea, Barbara ametoa zoezi kwa msomaji . Aandike jina la mpenziwe huyo na tarehe ya kuanza hadi kufa kwa uhusiano huo au tarehe ya kuanza mpaka hapo walipofika; kisha afunge macho halafu aanze kuangalia kama movie ya mahusiano yake hayo. Aiangalie toka mwanzo huku akizingatia alama za tahadhari alizoziona. Baada ya hapo achukue kalamu aanze kuandika alama alizoziona na mwishoni aseme kama kufa kwa mahusiano yake au matatizo yaliyopo ni ajali au ni mchakato ulioanza zamani.
Mimi uhusiano wangu ulikufa kutokana na ukosefu wa uaminifu (infidelity). Niliongea weeeee, nililia weeeee lakini wapi. Matatizo mengine yalikuwepo lakini hili liliniumiza zaidi.
Basi baada ya kusoma nami nikachukua kalamu nikaandika jina la mpenzi wangu tuliyekutana chuo na tarehe ya kuanza na kwisha kwa uhusiano huo kisha nikaanza kutiririsha alama za tahadhari nilizozidharau kama ifuatavyo:
NB: Alama hizi za tahadhari hazijaandikwa kwa mtiririko wa jinsi zilivyotokea na ni kwa miaka yote niliyokuwa katika uhusiano huo, si mfululizo.
JINA: MAHABA NIUE 2004-2008
1. Ndoa ya wazazi wake ilifeli, sikufikiria kuchunguza kama imemuathiri vipi katika mtazamo na mwenendo wake kwenye mahusiano.
2. Tukiwa kwenye mtoko kwenye ufukwe mmoja mkongwe jijini akaangalia mahali kisha akatabasamu na kusema zamani akiwa mdogo alikuwa anakuja na babake na totoz yake, wao wanakaa pale yeye anaogelea kule. Likanishtua lakini sikulitilia maanani.
3. Tulikuwa tukitumia ndomu. Nikasafiri zikiwa zimebaki mbili, niliporudi sikuzikuta badala yake nilikuta moja na ni aina tofauti na tulizokuwa tukitumia. Akasema kakake alikuja na demu wake ndo wamezitumia na kubakiza ile niliyoikuta. Nilibaki na shaka ila nikamezea.
4. Kulikuwa na picha yetu ukutani, siku moja sikuikuta akasema imeaguka yenyewe na kioo cha fremu kimepasuka na niliponunua fremu nyingine hakutaka picha irudi ukutani. Nikapotezea.
5. Kulikuwa na nguo zangu chache. Sikuziona pale zilipokuwa zinakaa. Akasema bibi alikuja kumtembelea na kwa kuwa hakutaka maswali yake akaona bora azifiche tu. Maswali yangu yakabaki moyoni.
6. Alianza tabia ya kuficha simu, kuiweka password kuitoa sauti usiku na kwenda nayo bafuni. Tukawa tunagombana kuhusu hilo, baadae nikaliacha.
7. Niliwahi kukuta chupi bafuni kwenye bomba la shower akasema ameninunulia na aliniwekea bafuni kama surprise. Sikuivaa na baada ya muda ikabidi aitupe huku akinungunika kuwa nimemvunja moyo.
8. Nikiulizia kuhusu kuingia level nyingine ya commitment ananiuliza nina wasiwasi gani? Angekuwa hana mpango na mimi angeshaniacha zamani. Mara kadhaa pia alikuwa akisema ndoa si ya kukimbilia lakini sikuwa naipa uzito hiyo kauli.
9. Alidai ufunguo wake umepotea hivyo nimpe ule wa kwangu. Hakunirudishia tena kwa hivyo kwake sikuweza kwenda bila miadi. Moyo ukawa unauma lakini sisemi.
10. Alipunguza safari za kunitembelea na kusingizia kuwa anachoka sana na kazi.
11. Birthday yake moja nikaenda nyumbani kwake kumpelekea zawadi. Mezani nikakuta zawadi za kuvutia na kadi toka kwa dada mmoja niliyekuwa nikimfahamu kama rafiki yake wa karibu chupa ya mvinyo, designer perfume na kadi yenye maneno mazito matamu. Nikahoji akasema nina hisia mbaya sana! Ninawezaje kumhisi vibaya na rafiki yake wa karibu na wa siku nyingi namna ile? Kwa ufupi uhusiano wao ulipamba moto na nikasahaulika kwa muda. Hapa ndipo ganzi ya ujinga ikanitoka nikakimbia. Mwaka wa 4!
Kwa mujibu wa mwandishi Barbara, wito wa kuzingatia alama za tahadhari haumaanishi kwamba ukiziona tu ukimbie au umuache mwenza wako. La, anataka usizichukulie kirahisi bali uzipime, ujipime. Kama utaona huziwezi ila una mapenzi ya dhati kwa mwenzio na nia basi umshirikishe. Mwenzio akikubali kuwa ana matatizo na akawa tayari kuyafanyia kazi mnaweza kuwa na uhusiano mzuri wenye afya. Akikataa basi huna budi kuondoka kungali mapema. Uhusiano unakuwa mgumu pale tatizo la mwenzio linapokukera na ukimwambia haonyeshi kulikubali (anakuwa kwenye denial).
Nawatakia wikiendi njema.