Maandishi kwenye t-shirt

Maandishi kwenye t-shirt

BUSY TONE NOT MY ASS
hii kavaa mbeba lumbesa mmoja pale sokoni tandale
 
serious...nilipokwenda kuanza form one nilikuwa na t'shet imeandikwa NO MONEY..kufika shule (boarding) wakubwa wa shule wakawa wananiambia hata kama sina pesa nitazitoa tu...ilinisaidia kimtindo.
 
Mie niliona mdada huku A-town kavaa T-shirt imeandikwa "MY BOYFRIEND'S WIFE HATES ME"
 
Wengine tunadanganyana tu hapa nimeshaona
 
Jana nikiwa kazini mara nikamuona sharo-b mmoja katinga t-shirt yake iliyochorwa fuvu la mtu akiwa amechuchumaa kuonyesha ana-fart. Kuna maandishi yameandikwa
'SILENT BUT DEADLY'.
Ikanikumbusha t-shirt nyingine ya jamaa mmoja hapohapo kazini iliyokuwa imeandikwa
'FIFTEEN MEN ON DEADMAN'S CHEST' huku imechorwa vikaragosi 15 kwenye eneo lililosawa na kifua cha jamaa.

Sijui wanavaa wakijua ama inatokea tu.

weka uliyoona.

Dogs rule
 
Pale calabash pub lufungira kuna dogo alivaa t-shirt imeandikwa I SUPPORT GAY MARRIAGES. Tukamwita tukamuuliza kama anajua maana yake akasema hajui. Tukamwambia, alitoka mbio kwenda kuivua utafikiri tumemwambia ageuke atoe tigo.
 
M4C, Maisha Bora Kwa kila Mtanzania, FORWARD, Ngangari, M4V, Thanki Vere Macheee.
 
moja iliandikwa how about a nice cup shut thy fack up!

kuna dogo mmoja moshy alivaa imeandikwa tap my back
 
Nilipokuwa Secondary Lombeta Moshi kuna jamaa alikuwa anaitwa Ramadhani Mdaile alikuwa na T-Shirt imeandikwa "Lick me till I scream"
 
"MORTUARY ATTENDANT".....jamaa tunamfahamu, nilikuwa na maza tunakatiza mitaa ya one way Dom, yaani ile ananyoosha mkono ku-shake hand niliangaliaje pemebeni sasa. kumbe siyo hata mortuary attendant kanunua t-shirt sijui kwenye mitumba au alipewa msaada na wa-missionary!
 
Mi nnazo zilizoandikwa "KAMA HUWEZI KULIPA 200 PIGA MBIZI" kwa anayezitaka naomba ani PM
 
Back
Top Bottom