Maandamo Kuing'a Serikali Algeria Yakwama

boma2000

JF-Expert Member
Oct 18, 2009
3,280
310
Maandamano yaliyoanza Algeria ya kumwondoa rais wake yameota mbawa baada ya serikali kumwaga polisi wengi mitaani kuwashughulikia waandamanaji. Hii inaonyesha Waalgeria ni waoga sana katika mataifa ya Kiarabu na hawakuwa na dira yoyote, walifuata mkumbo tuu baada ya kuona Tunisia na Misri wamefanikiwa kuwatoa watawala wao dhalimu
 
Waandamanaji wa TANZANIA nao washughulikiwe kama wenzao wa ALGERIA....! HONGERENI POLISI WA ALGERIA KWA KUWEKEZA AMANI NA UTULIVU
 
Hii nayo kali. Unataka waandamanaji wa Tanzania washughulikiwe! Kwa mawazo yako hapo ndiyo unawekeza katika amani na utulivu? Wewe Mahesabu hiyo hesabu yako siyo kabisa.
 
Hii nayo kali. Unataka waandamanaji wa Tanzania washughulikiwe! Kwa mawazo yako hapo ndiyo unawekeza katika amani na utulivu? Wewe Mahesabu hiyo hesabu yako siyo kabisa.

kwa hali halisi iliyopo Tanzania kwasasa ni dhahiri tunakoelekea kubaya hata hao Polisi ni miongoni mwa waathirika sijui nani atamzuia mwenzake itapofikia watanzania wakawa na kauli moja ya 'tunataka mabadiliko' hii harufu inanukia dhahiri, hili la G'mboto wote ni waathirika
 
Nafikiri kwa Tanzania kwa vile tayari utamaduni wetu haurusu kwa rais kukaa zaidi term mbili basi tujitahidi kufanya mabadiliko kwenye uchaguzi ujao kutegemea na wagombea watakaokuwepo na siyo chama. Mimi naamini katika uwezo wa mtu kutenda, maana chama hata kikiwa na sera nzuri kiasi gani kama kiongozi ni hovyo na serikali itakuwa hovyo.
Tusiige mkumbo kama algeria walivyofanya
 
Back
Top Bottom