Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,625
- 46,270
Wale wanapropoganda local anti-west mnaopiga yowe kulazimisha kufananisha maandamano yanayoendelea Ufaransa na Israel na yale ya Iran au Arab spring ni vyema mkaelewa tofauti hizi.
1. Mpaka sasa hakuna waandamanaji waliouwawa na serikali zao katika haya maandamano zaidi sana waandamanaji hawawatafunguliwa kesi. Makadirio ya chini wa waliouwawa katika maandamano Iran ni raia 500, bunge la nchi hiyo lilipendekeza raia wengine 15,000 wapewe adhabu ya kifo.
2. Iran na nchi nyingine za kidikteta huwa wanapinga utawala mzima mbaya. Mfano Iran waandamanaji walikuwa wanapinga wanawake kulazimishwa kuvaa hijabu. Waandishi huko wanapinga mfumo mzima wa utawala ku control maisha yao binafsi juu ya dhuluma nyingine za uchumi na kijamii. Ufaransa waandamanaji hawataki tu kuongezewa muda wa kustaafu kufanya kazi kutoka miaka 62 hadi 64.
3. Raia wa nchi za kidikteta kama Iran hawana fursa ya kubadilisha sera au jinsi nchi zao zinaongozwa kidemokrasia. Ayatollah anayeamua kila kitu Iran ni kiongozi mkuu wa kudumu katika taifa hilo, njia pekee ya kubadilisha mambo ni kwa njia kama hizo za maandamano makubwa na uasi. Ufaransa raia wake wana fursa ya kubadilisha utawala kama hawapendi sera zinazopitishwa. Macron ni Rais wa kwanza wa Ufaransa kuchaguliwa kwa muhula wa pili baada ya miaka 20, hata hivyo mwaka 2027 utawala wake utafika tamati na raia wengi watakuwa na uwezo wa kumuweka mwingine wanayemtaka.