Maandamano ya mabucha ya Nguruwe 1993

Maswali
1. Je waliwatoa hao masheikh siku hiyo?

2. Sheikh Kassim ilikuaje akakosekana kwenye maandamano aliyoyanzisha akawa arusha akielekea Nairobi "kwenye matibabu"?


 
Huyu Rashid Idd Athuman Njeja alikuja kuokoka na kuanza kuhubiri akiukosoa Uislamu namfahamu. Hakika ni zamani yenye mafunzo.


 

Thank you. This is a very balance narration in my opinion. Na inaleta hamasa kusoma.
Kama mtu anauziwa nyama ambayo sio aliyoagiza na anakataliwa kurudishiwa hela yake, that is a problem. Muuza bucha kutoka Mbokumu, Kule Moshi hakusoma alama za nyakati
 
Rashid Njeja anasema kuwa wao walimtuma mtoto makusudi akanunue nyama ya Nguruwe ili kutafuta chokochoko walimtuma then wakawa wanasubiria aje walianzishe. Wanasema lengo lilikuwa ni hilo kutafuta ugomvi na wasio waislamu. Na wakapata chanzo. Anayezungumza haya ni mwislamu mwenzi aliyeshiriki kadhia hiyo na baadaye akaacha uislamu.

 
Chizi,
Umenipa taarifa ambazo sikuwa nazijua.
Ahsante sana.
 
Huyu Mzee ni lini ataacha kuandika maboko...

Ati Sheikh asishangawe kwa kutoisimamia haki? Yaani nae aunge mkono kuvunja Mabucha ya Watu wa Dini tofauti katika nchi inayosimamia haki kwa kila mtu na Serikali isiyo na dini afuate mihemka ya imani ya dini yake si ataumia na kisha umcheke tu.
 
...Ndipo Sheikh Waziri Ramadhani akasimama na kusema, "Ndugu zangu Allah leo ametuletea mtihani kutuangalia kama tunaweza kusimama kuipigania dini yake.
Kwa ufupi, uisilamu ni uwanaharakati, sidhani kama ni dini
 

Umepita nchi zote nguruwe ulikuta TZ tu.kwa kuwa sio nchi yako
Hapa kichwa cha habari na story nimeshindwa kuelewa kwa hiyo sisi nguruwe huo mwaka
 
sio balanced kama unavyodhani , huyu kasimulia ili kuwafanya waislam waonekane ni 'good guys' kwenye huo mgogoro, Waislam ni watu wanaotaka imani yao kuwa ndio iwe sheria ya kutolea maamuzi kwenye mambo yote ya kijamii, na kwenye hili nina uhakika hawawezi kuwa innocent kama huyu jamaa alivyosimulia japo kuna uwezekano wa Serikali kufanya makosa pia

tafuta msimulizi mwingine wa upande wa Serikali au wa wauzaji wa Bucha wasimulie na wao ndipo utajua hasa ni yupi mchokozi
 
Picha ambayo hainitoki kichwani mwangu ni picha ya Sheikh Kassim Juma mwaka wa 1979 anamkaribisha Nyerere ndani ya Msikiti wa Mtoro kwenye khitma ya aliyekuwa Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir.


MZEE HIYO HAPO JUU INAHUSIANA NINI NA KICHWA CHA HABARI?
 
Siri ya kukosa uvumilivu


View: https://m.youtube.com/watch?v=oiVFGmCKEAADr. Robert Spencer mwanazuoni na mtafiti nguli wa religious studies aliyeandika kitabu - 'Ukweli Kuhusu Muhammad: Mwanzilishi wa Dini Isiyo Na Uvumilivu Zaidi Ulimwenguni', Spencer anajadili vyanzo vya mwanzo kabisa vya Kiislamu kuhusu maisha ya Muhammad nabii wa Uislamu, na anaonyesha jinsi ghasia, kutovumiliana, na ukandamizaji ambao umeashiria utamaduni wa Kiislamu si ukiukwaji. ya kanuni za Kiislamu, lakini zimekita mizizi katika mafundisho na mfano wa muasisi wa Uislamu.

Religious Studies ni nini : Masomo ya kidini, ambayo pia hujulikana kama utafiti wa dini, ni uwanja wa kitaaluma unaojitolea kufanya utafiti wa imani za kidini, tabia na taasisi. Inafafanua, inalinganisha, inafasiri, na inafafanua dini, ikisisitiza mitazamo ya utaratibu, yenye msingi wa kihistoria, na ya tamaduni mbalimbali.
 
Uzalendo,
Mufti Sheikh Hassan bin Ameir alimkaribisha Nyerere katika TAA akiwa mjumbe wa TAA Political Subcommittee tokea 1950.

Wajumbe wengine katika kamati hiyo walikuwa: Dr. Vedasto Kyaruzi, Abdul Sykes, Hamza Mwapachu, Sheikh Said Chaurembo, Steven Mhando na John Rupia.

Mshauri wa kamati hii alikuwa Earle Seaton.

Hii ndiyo kamati ndani ya TAA iliyoshughulika na siasa.

Nyerere katika kuivunja EAMWS akatoa amri Mufti Sheikh Hassan bin Ameir akamatwe na arudishwe kwao Zanzibar.

Hii ni sawa na Rais Mwinyi atoe amri Kadinali Pengo akamatwe na kurejeshwa kijijini kwao.

Uhusiano wa hayo maneno ni kule Nyerere kualikwa na masheikh wa BAKWATA kuhudhuria khitma ya Sheikh Hassan bin Ameir kiongozi wa Waislam aliyemfukuza nchini kwa kuwa alikuwa akiwaongoza Waislam kujenga Chuo Kikuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…