Maandamano ya kumpinga Trump yafanyika Marekani

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,191
4,104
Waandamanaji walikusanyika mjini New York, Marekani hapo jana kwa lengo la kushinikiza kushitakiwa na kuondolewa madarakani rais Donald Trump.

Mkusanyiko huo unafanyika katika kipindi kifupi kabla ya leo hii, siku ambayo Baraza la Wawaikilishi linatarajiwa kupiga kura kuridhia hatua ya kushitakiwa kiongozi huyo. Waandaaji wa maandamano wanasema wanatarajia maelfu zaidi kushiriki maandamano hayo.

Eneo la Manhattan, la mjini New Yorki ni moja kati ya maeneo 600 ambayo yamepangwa kufanyika maandamano ya kushikiniza kushitakiwa kwa rais Trump.

Trump anakabiliwa na shitaka la matumizi mabaya ya madaraka kwa kuiagizia Ukraine kumchunguza makamo wa rais wa zamani wa Marekani Joe Biden, ambae anaongoza katika kinyang'anyiro cha kuwania urais kwa upande wa chama Democratic, ikitajwa kuwa kama hatua ya kumpinga katika kuwania urais katika uchaguzi wa 2020 wa Marekani.

Trump pia anakabiliwa na shitaka la kufanya njama za kuvuruga uchunguzi wa bunge dhidi yake katika tuhuma hiyo.

1576664729800.png
 
Back
Top Bottom