Maandamano ya CHADEMA Bunda mabomu yapigwa

mende 2014

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2014
Posts
763
Reaction score
131
Wanachama wa chama cha CHADEMA wapigwa mabomu baada ya kufanya maandamano katika mtaa wa @Nyasura center hapa mjini Bunda mkoani Mara. Watu kadhaa wamekamatwa na kupelekwa polisi.

Leo kuanzia saa mbili asubuhi Makamanda na wanachama wa CHADEMA na wananchi wasio na vyama vya siasa walikusanyika katika mtaa wa Nyasura kwa ajili ya kuanza maandamo ya kupinga Bunge la Katiba kuendelea na vikao vyake. Wananchi walikuwa wengi kama 1200 na ilipofika saa tano kamili maandano yalianza kuelekea stendi ya zamani ambapo ilitalajiwa ufanyike mkutano mkubwa, polisi walikuja na kuanza kulusha mabomu ya machozi na kwa kuwa wananchi walikuwa wamejizatiti, mabomu ya machozi ni kama hayakufua dafu ndipo risasi za moto zilianza kutumika. Mpaka sasa wameisha kamatwa viongozi sita wa CHADEMA

Wananchi bado wanaendelea kujikusanya na kutiana hamasa! naona makundi makubwa makubwa ya watu sasa yanatoka kwenye nyumba zao na wameanza kujikusanya wakiwa na lengo la kuendelea na maandamo!

ntaendelea kukupa habari, maana macho yanawasha!!

  • Thanks
Reactions: jme
hao ndo wana ufahamu wa haki zao, wengine mpaka katiba ianze kutumika ndo watazinduka
 
Leo kuanzia saa mbili asubuhi Makamanda na wanachama wa CHADEMA na wananchi wasio na vyama vya siasa walikusanyika katika mtaa wa Nyasura kwa ajili ya kuanza maandamo ya kupinga Bunge la Katiba kuendelea na vikao vyake. Wananchi walikuwa wengi kama 1200 na ilipofika saa tano kamili maandano yalianza kuelekea stendi ya zamani ambapo ilitalajiwa ufanyike mkutano mkubwa, polisi walikuja na kuanza kulusha mabomu ya machozi na kwa kuwa wananchi walikuwa wamejizatiti, mabomu ya machozi ni kama hayakufua dafu ndipo risasi za moto zilianza kutumika. Mpaka sasa wameisha kamatwa viongozi sita wa CHADEMA

Wananchi bado wanaendelea kujikusanya na kutiana hamasa! naona makundi makubwa makubwa ya watu sasa yanatoka kwenye nyumba zao na wameanza kujikusanya wakiwa na lengo la kuendelea na maandamo!

ntaendelea kukupa habari, maana macho yanawasha!!
--------------------------------------------------------------------------------

Samahani wana JF, bado najitahidi kutafuta picha kwani aliyekuwa na camera tumepotezana na simu yake haipatikani mpaka sasa maana askari walimuandama sana baada ya kumuona anachukua tukio la kuteswa kwa raia moja (mama), mama huyo alikuwa akipita tu hakuwa anajua lolote akakutana na hawo askari wakaanza kumpiga na kumshika shika maeneo maalumu, askari walishutuka wakamwona jamaa akipiga picha wakamwandama, sijui kama ameisha kamatwa au la!
 
Aiseee!!!

Hizo risasi zilipigwa hewani au zilielekezwa kwa waandamanaji?
 
nimepita Bunda jana, sikuamini kuwa ndio anapotoka Wassira, yaani pamoja na kelele zote zile kumbe kashindwa kuweka hata maji?
 
Pamoja sana makamanda, watashindana lakini hawatashinda.
 
Inabidi tufanyie CBA muda, risasi na mabomu ambayo Chagonja anayaachia hovyo hovyo
 
nimepita Bunda jana, sikuamini kuwa ndio anapotoka Wassira, yaani pamoja na kelele zote zile kumbe kashindwa kuweka hata maji?

Maji amuwekee nani wakati yeye anaishi Dar es salaam na kazi anafanyia Dodoma? Bunda anaenda tu kuwasalimu wazazi na kuomba ridhaa ya wana Bunda ya kuendelea kuishi Dar.
 
Back
Top Bottom