Maandamano ya CHADEMA Bunda mabomu yapigwa

Maandamano ya CHADEMA Bunda mabomu yapigwa

wamethubutu hao siyo mbeya kwa sugu ohoooo sugu raisi wa mbeya ohoooo....halafu tunawachia polisi waandamane loh!!
 
maoni yangu niliyoyatoa kwa viongozi wa chadema Bunda hawakuyazingatia lakini kama kweli polisi wametumia risasi za moto na kama kuna mtu ameuwawa itakuwa mwanzo wa machafuko Tanzania nzima, mimi nilichokuwa naofia ni mageuzi ya kumwaga damu sasa kama kuna damu imemwagika Bunda hilo litakuwa ni kosa kubwa sana kwa Polisi maana uwenda zitamwagika damu nyingi sana kabla ya ccm kuondoka madarakani. wenye masikio na wasikie maana sisi kina gogo la shamba kazi yetu ni kushauri tu,yale yenye busara na hekima
 
Sasa mkiandamana bunda mtasaidia vipi kusitisha vikao hivyo huko dodoma.

Ni uwendawazimu.
 
Ni huko huko, sisi hapa Tanzania ya CCM - MAANDAMANO YOYOTE NI MARUFUKU, na yeyote atakayeipinga katiba tunayoiandika ataishia shimo la tewa.

attachment.php
 
Nakubaliana na wewe

Samahani wana JF, bado najitahidi kutafuta picha kwani aliyekuwa na camera tumepotezana na simu yake haipatikani mpaka sasa maana askari walimuandama sana baada ya kumuona anachukua tukio la kuteswa kwa raia moja (mama), mama huyo alikuwa akipita tu hakuwa anajua lolote akakutana na hawo askari wakaanza kumpiga na kumshika shika maeneo maalumu, askari walishutuka wakamwona jamaa akipiga picha wakamwandama, sijui kama ameisha kamatwa au la!
 
Bunda.Jumla ya watu sita wamekamatwa na Police. Maandamano yalianzia Nyasura. Gafla kindi Ia Polisi Zaidi ya miamoja na magari takribani manne walifika na kufyatua risasi na mabomu ya machozi kutawanya watu. Hadi Sasa sintofahamu inaendelea.
 
Hakuna aliyejeruhiwa au kuuwawa? Maana vita havina macho!

Ni mapema kujua hiyo maana kila mtu amekimbia, labda baadae kidogo ndo tumeanza kurudi eneo la tukio, lakini wananchi wanaendelea kujikusanya kwenye maeneo tofauti tofauti ili waendelee na maandamo ambayo kwa sasa hayatakuwa na sehemu ya kukutania, ili mradi kila mtu amalize kiu yake ya kuandamana. Changamoto ninayoiona kwa aina hii ya maandamo ni kuwa polisi ambao wana gari moja na maandamo sasa yanaanzia sehemu nyingi nying tofauti tofauti na yanakomalizikia kila kundi linajua lenyewe!!
 
Agizo la Pinda linafanya kazi ngoja wapigwe tuuuuuu kama wanakaidi.
 
mbona nimempigia mdogo wangu hapo bunda anaishi maeneo ya machinjioni amesema hakuna vurugu yeyote.
 
Hata misri yalianza hivi

Wacha misri libya mambo yalikuwa kama hivi nihatari mtakuja kuleta tabu kwa wazee wa mama zetu na watoto hao polisi watakimbia na hao viongozi watakimbia tutaachwa mm na wewe kwenye mitaa
 
Wacha misri libya mambo yalikuwa kama hivi nihatari mtakuja kuleta tabu kwa wazee wa mama zetu na watoto hao polisi watakimbia na hao viongozi watakimbia tutaachwa mm na wewe kwenye mitaa

Tabu zipo kila siku.
 
Hahah huko ndo musoma line mpk jamaa wamewekewa kanda maalum ya kijeshi ujue jamaa mziki wao sio wa kitoto!
 
Ni mapema kujua hiyo maana kila mtu amekimbia, labda baadae kidogo ndo tumeanza kurudi eneo la tukio, lakini wananchi wanaendelea kujikusanya kwenye maeneo tofauti tofauti ili waendelee na maandamo ambayo kwa sasa hayatakuwa na sehemu ya kukutania, ili mradi kila mtu amalize kiu yake ya kuandamana. Changamoto ninayoiona kwa aina hii ya maandamo ni kuwa polisi ambao wana gari moja na maandamo sasa yanaanzia sehemu nyingi nying tofauti tofauti na yanakomalizikia kila kundi linajua lenyewe!!

Kwa vile hatukukuomba utujuze ila umeamua kutoa taarifa endelea tu mkuu tukiona kimya ni mawili huenda utakuwa ume-RIP au unanyea debe ila yote heri, usinichoke mkuu naomba nijuze ile familia ya wale marehemu wa maandamano ya Arusha chadema imewafanyia nini?
 
Back
Top Bottom