KAYGREKO
Member
- Jan 18, 2013
- 38
- 33
MAANDAMANO YA AMANI + VIONGOZI WA DINI + DIASPORA
Nianze na ukweli ambao wengi tutakubaliana. Afrika hatuna mazowea ya kuwa na maandamano ya amani. Na hata zile nchi zenye uzoefu wa maandamano ya amani, huanza kwa amani na mwishowe huzuka fujo. Kwa nchi yetu ya TZ, na hasa baada ya yaliyotokea 29/10, kuitisha maandamano ya amani NI KUDANGANYANA.
Viongozi wa dini sehemu yoyote duniani huwa wana nguvu na uwezo wa kiajabu wa kusikilizwa na kufuatwa na wafuasi wao. Lakini wanapojisahau na wakawa wanaweka mbele maslahi yao ya kibinadamu kwa kuitumia dini, hapo hata Mungu huwapa uelewa wafuasi wao wa kutowafuata, japo wataendelea kuhudhuria misikitini na makanisani.
Nyumbani TZ kuna wanaoelewa vibaya kuwa sisi tunaoishi huku ughaibuni (diaspora), wote tunashabikia yatokee machafuko. Wanasahau kuwa SIYO WOTE TULIOPO UGHAIBUNI TUNA MSIMAMO HUO. Huku tupo wengi hatuzingatii vyama wala dini. Tuna ndugu na jamaa zetu TZ, na hatufurahishwi kuona ndugu zetu wanadhurika.
Facebook
www.facebook.com