Kizibo
JF-Expert Member
- Jul 3, 2018
- 4,554
- 10,327
Nimekaa nikatafakari, nikagundua haya maandamano ya 9D ni myego mkubwa sana kwa pande zote mbili, serikali na Gen Z wote.
1 Gen Z tusipoandamana kama tunavuohamasishana mitandaoni, au serikali ikifanikiwa kuzima au kuzuia hayo maandamano, maanake Gen Z tutakuwa tumepoteza pambano. Kitakachofuata..tutaishi kwa tabu sana. Watawala watatufanya chochote watakavyojisikia. Watatuteka, watatuua, watachota mali za umma vile watakavyo na hatutakuwa na mtetezi.
Serikali ikitudhibiti Gen Z, maanake kwa miaka yote, yoyote atakaethubutu kuinua mdomo ni kuuawa tu.
2 Ikiwa Gen Z tutaandamana kwa wingi, kisha serikali ikaua tena kama ilivyoua siku ile ya MO29, kipi kitafata kwa serikalli?? Jumuia za kimataifa watachukua hatua gani?? Au wataacha tuuane tu kwa kuwa ni swala la mambo ya ndani (Home affairs)
Na je, Gen Z watakaosalimika na wanachi watakao kuwa wamepoteza watoto, wazazi, ndugu jamaa na marafiki wataridhika na kukubaliana na swala la kuuliwa kwa wapendwa wao kwa mara ya pili?? Au ndo utakuwa mwanzo wa watu kutafuta na kuingiza siraha nchini kimagendo na kuanzisha ugaidi na uasi msituni ili kulipiza??
3 Ikiwa serikalli itaacha maandamano yawepo na watu waandamane kwa amani, kitakachofata ni MAFURIKO YA RAIA KARIBIA WOTE KUINGIA BARABARANI. sasa hapa ndo serikali na ccm wataona ni kwa namna gani watu hawapo upande wao.
Hata wazee na watoto watajaa barabaarani. Matokeo yake serikali itaanguka mapema asubuhi.
Kwa ujumla, swala la 9D limekaa kimtego na kimkakati sana.
Nawasilisha