kwamagombe
Senior Member
- Aug 25, 2009
- 154
- 42
kumekuwa na vita kubwa ya polisi na askari katika mji wa songea baada ya wananchi kupamba moto na kushindwa kuzuia hisia zao kwa kile wanachokisema polisi hawatoi ushirikiano kwa mauaji yanayoendelea katika manicipal ya songea. taarifa ambazo ninazo wananchi wawili wamepigwa risasi na polisi na wananchi wamempiga mawe polisi ambayo yupo katika hali mbaya.
wapi tunakwenda?
Dogo usifanye mzaha.Songea iko mkoa gani?
Hivi hawa polisi wako juu ya sheria hata wawapige risasi raia wasio na silaha? Kuwa polisi wa namna hii ni laana na aibu kwa taifa.
Hali ni tete kuna hiace katika harakati za kukimbia imetumbukia kwenye korongo na abiria ila hakuna aliefariki ni majeruhi tu.
Balaah na RPC anazidi kutema pumba ati hao wanaouana ni watu na wapenzi wao.
kuchoma kituo cha police si ujanja, maana hasara na kwetu sis walipa kodi. Nasisitiza maandamano si kufanya uhalifu otherwise hayatakuwa na credibility
taarifa nilizo zipata kwa mtu aliye eneo la tukio ni kwamba, ofisi ya mkoa ccm imepigwa mawe na kuvujwa, kituo kimoja cha polisi, hajataja ni kipi kimesha vunjwa, barabara za kutoka na kuingia mji wa songea zimefungwa na raia, polisi wamesha zidiwa nguvu na waandamanaji, kwa sasa nao wanapata mkongoto wa mawe,
ntaendelea kuwajuza.
Tujuze mkuu,vp mapambano hapo songea yamefikia wapi?????Ahsante kwa taarifa, kwakweli ni masikitiko makubwa kwa wananchi pamoja na hao askari waliopoteza maisha yao.
Hili suala la polisi kutumia mabavu kila mara kwa raia wasiokuwa hata na jiwe ni upumbavu mkubwa sana, na sijui kama haya ndiyo mafundisho wanayokwenda kupata chuoni CCP kwa muda wote wa mwaka mmoja.
Kama wananchi wameandamana hadi kwa mkuu wa mkoa na wanachotaka ni mkuu wa mkoa atoke kuwasikiliza, tatizo lilikuwa wapi hadi FFU wanaamua kupiga risasi za moto hadi kuua raia? kama wameshindwa kuwalinda raia hadi wanauawa kila siku bila msaada wao, huo ubabe wa kuwaua raia wema unatoka wapi? mbona wameshindwa kupambana na hao wauaji?
Kumbe Dr. Mwakyembe hakukosea kwamba jeshi la polisi la Tanzania, ndilo jeshi la polisi pekee duniani linalosubiri kuletewa ushahidi mezani kama vile mahakama zinavyosubiri kuletewa ushahidi ili zifanye kazi. Na hii tabia ya polisi kuwaonea wananchi ipo siku watachoka na wataamua kukabiliana nao bila kujali risasi za moto ama mabomu, ikizuka majimaji ya pili huko wasije kuwalaumu wananchi.
Haya madhara ya kuwekana katika kila sehemu kwa interests binafsi! Huyu jamaa hajui analofanya wala kuongea. RPC hafai kabisa.Hali ni tete kuna hiace katika harakati za kukimbia imetumbukia kwenye korongo na abiria ila hakuna aliefariki ni majeruhi tu.
Balaah na RPC anazidi kutema pumba ati hao wanaouana ni watu na wapenzi wao.
Haya ndiyo yanayojiri Songea kwa sasa