Hayo ndo mafunzo ya polisi wale wasiokua na kazi (FFU)waliyopata pale ccp moshi tuwalaumu wale waliowapa mafunzo huenda ndo waliwaelekeza njia ya kuzima maandamo ya raia wasiokua na silaha ni kutumia silaha za moto tu
Mi napendekeza hawa askari wasiokua na kazi (FFU) wawawepeleke somalia wakambanane na Al shabab maana hapa bongo hakuna kazi ya kuwapa
Ndugu yangu;
Jeshi la Polisi siku hizi ukimuona Askari amevaa sare za FFU siyo kile kikosi tulichokizoea miaka yote ambao walikuwa na kazi ya kutuliza ghasia.
Hawa siku hizi ni askari wale ambao wapo vituo vya polisi ndio wamevalishwa magwanda yale ili wafanye kazi ya FFU. Hawana uzoefu wowot na ndio maana vitendo vya kialifu vinaongezeka siku hadi siku. Hawa walishazoea kukaa vituoni na kupokea milungula toka kwa vibaka na wapiga debe wa madaladala, sasa wakipewa pikipiki wanajiona wamefanikiwa sana na wamepanda cheo kwa kukaa katika pikipiki tu. Siku wakipangiwa kukaa katika patrol (defenders) hapo ndio usiseme!!!!!!!!!!! balaa tupu anaona amekuwa mkuu wa majeshi!!!!!!!!!
Na huu mchezo ulianza toka ilipoanzishwa kitengo cha pikipiki (TIGO)
ukitaka kuhakikisha nisemayo:- chunguza utendaji wa kazi wa askari TIGO na fuatilia jinsi wanavyoua raia pasipo makosa. Mimi nawaomba ndugu zangu wasamaria wema tusiwalaumu Askari kwa kuua raia katika matukio kama haya kwa sababu hawa askari wanaokaa katika Defender na pikipiki wengi wao walishazoea kukaa vituoni na kushika fimbo na filimbi. Leo unampa Bunduki na alisha sahau kuitumia miaka mingi. Hivyo akiishika badala ya kutishia yeye anafyatua. Wengi wao wanakuwa hawakudhamiria kuua lakini kutokana na umbumbumbu wa kutumia Bunduki wanafikia hapa.
Na pia leo wanatembea mitaani na kukutana na watu wengi, hivyo wanatamani kupata pesa kwa kutumia Bunduki waliyopewa. Mfano tukio la Mbeya la juzi kifo cha mwanafunzi ambaye alikuwa yupao bar. Kulikuwa na sababu gani kwa askari kufyatua risasi.
Ni umbumbumbu tu ule. Inabidi IGP aliangalie vizuri jeshi lake na askari vinginevyo watakuwa wanamuharibia CV yake. Kwani uozo kama huu ukitokea raia tunamuangalia IGP atasema nini. Ukizingatia kamada wa Mkoa naye ametoa pumba, je na IGP atasema nini.
kuna sababu kubwa sana ya Jeshi la Polisi kuangaliwa upya na hawa makamanda wa mikoa wabadilishwe kila baada ya muda fulani kwani wanazoeana na askari wa chini kisha lawama zitaenda kwa Serikali na IGP.
Tulitegemea baada ya mauaji ya Arusha na Zanzbar, jeshi la Polisi litajirekebisha na kutafuta mbinu nyingine ya kupambana na wananchi wasio na siraha za moto. Kumbe bado wanaendeleza mchezo ule ule wa kutumia silaha za moto.
je hapa kuna tofauti gani na mapambano ambayo Babu zetu walikuwa nayo kati ya Wakoloni na Wafrika waliopinga kutawaliwa. Mkoloni alikuwa na Bunduki na Mwafrika alikuwa na Fimbo. Tena ndugu zangu Wangoni ndio usiseme kwani wao Mkoloni akipiga Risasi wao silaha yao ni kusema
"MAJI, MAJI, MAJI......"
Je tunarudi kule enzi za vita vya Maji Maji??? (Mkoloni na Kinjekitile, Mkoloni na Isike, Mkoloni na Mirambo n.k)
Ni wakati sasa kwa JEshi la Polisi Tanzania Kufanya
"TAFAKARI NA KUPATA MBINU YA KUPAMBANA NA RAIA WASIO NA SILAHA"
MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
Sasa kutokana na ulimbukeni huu