Inafadhaisha sana kusikia maneno makali yanayohatarisha amani ya Nchi hii yanatoka vinywani mwa viongozi waliopo madarakani. Hivi karibuni viongozi wa3 kwa nyakati tofauti wametoa kauli zinazohusu utumikaji wa Jeshi la wananchi kupindua serikali iwapo bunge litaidhinisha muundo wa muungano wa Serikali 3.
Baada ya wajumbe wa bunge maalum la katiba kumaliza wajibu wao, itabidi katiba watakayoipitisha ipigiwe Kura na wananchi wote kukubali ama kukataa mapendekezo yao. Sasa tayari Rais wa Jamhuri ya Muungano Jakaya Mrisho, Waziri wa Sera Wiliam Lukuvi, pamoja na Kapteni mstaafu wa JWTZ John Komba wamejitokeza hadharani kutoa matamko rasmi kuwa Bunge likiidhinisha muundo wa Serikali 3 JWTZ litapindua nchi. Kwa kauli hizi tunamjengea nini mwananchi wa kawaida tunaetarajia apiga kura kukubali mfumo wa S3?
Kama kweli humu nchini kuna taasisi za kupigania haki za binadamu, ni kwanini mpaka leo zimekaa kimya mpaka hapo kauli za Kikwete, Lukuvi na Komba zianze kutekelezwa kwa mapigano na vifo vya raia ndio taasisi hizo zijitokeze? Suala la kulinda amani ya nchi hii si la UKAWA peke yao.
Taasisi zote zilizopo nchini ziwe za dini, haki za binadamu, vyama vya wafanyakazi, vyama vya wanafunzi, taasisi za kisheria kwanini mmekaa kimya mpaka muone Komba na wenzake wamevaa Kombati za Kijeshi kuingia nyumba hadi nyumba kukata vichwa vya watu ambao wanaunga mkono Serikali 3?
Ni kwanini yasiitishwe maandamano nchi nzima ya taasisi zote zijiorodheshe kuingia barabarani kukemea ushenzi wa vitisho hivi vya wapuuzi wachache walioshindwa kujenga hoja za kidiplomasia na hata waone wana nguvu za Kijeshi kufanya wayatakayo!
Nipo tayari kuingia barabarani dakika yoyote kuunga mkono upingaji wa Kauli za kishenzi zinazohatarisha amani ya Nchi hii.
Huku kukemea kwa mtu mmoja mmoja akiwa amejifungia chumbani kwake hakitasaidia wala kuwashtua hao wapuuzi wanaojisikia kuropoka hovyo. Ni vyema dunia ipate taarifa kuwa watanzania wameamka sasa toka usingizi mzito.
Napendekeza taasisi zote kwa Dar es Salaam tukutane uwanja wa JANGWANI tarehe 28th April, 2014. Mikoani wananchi waende viwanja vikubwa vya wazi mfano viwanja vya Furahisha pale Mwanza. kwanini tarehe 28, kwakuwa bado wajumbe watakuwa Dodoma kujadili Katiba. Sababu ni kukemea kauli za kishenzi za viongozi. Suluhisho, wote waliotoa kauli hizo washughulikiwe ikiwezekana wavuliwe nyadhifa zao zote na kichaguliwe kisiwa wawekwe detention kwa uangalizi. Sheria itakayotumika kuwahukumu zitatungwa hapohapo JANGWANI maana sheria ni za wananchi waamualo ndilo.