Maandamano makubwa kupinga ujio wa Dk Slaa Kigoma Mjini

mkigoma

JF-Expert Member
Jul 26, 2011
1,180
309
Nipo hapa mwanga naona gari linapita likitangaza Maandamano ya kupinga ujio wa Dk Slaa mjini kigoma, Maandamano hayo yataanzia mwandiga hadi viwanja vya community center ambapo ndipo Dk Slaa anategemea kufanya mkutano wa hadhara kesho, Maandamano yatafanyika tarehe 8.12.2013 kesho jumapili. Maandamano yataanza saa 2 asubuhi. Gari kwa sasa limeelekea maaneo ya ujiji.

Ccm beana hivi mlishawahi kusikia CDM inafanya maandamano ya kupinga ujio wa Kinana na yakaruhusiwa na Polisi?
 
Hakuna tatizo kama maandamano yenyewe yamepata baraka (kibali) kutoka mamlaka zinazolinda usalama (polisi), na pia waandamanaji wasivunje sheria. Kuandamana ni haki yao! Hata hivyo CHADEMA wanatakiwa kupokea maandamano hayo na kuwasikiliza!
 
Aache wafanye yao, Lakini M4C haina masikio wala direction, yenyewe ni kama kimbunga inapita popote na wakat wowote bila kujali che wala chi, Slaa usiogope twende tu tuendeleze mapambano.
 
polisi kama wameruhusu maandamano na siku hiyohiyo dr Slaa ana kikao wanataka watu wauane. vita iliyoanzia kongo ikpitia Burundi na Rwanda naona sasa RPC anaikaribisha Kigoma. nimeamini vita ya wenyewe kwa wenyewe itaanzia Kigoma na Zito atakuwa ndo mwanzilishi.
 
Reactions: mmh
kweli CCM sasa wamechanganywa sana na ninachopenda wanaangaika lakini kigoma ni cdn na nccr waacheni wapoteze muda wao tuu kwani wakorof tayali wamekamatwa jana
 
kweli CCM sasa wamechanganywa sana na ninachopenda wanaangaika lakini kigoma ni cdn na nccr waacheni wapoteze muda wao tuu kwani wakorof tayali wamekamatwa jana

CCM inaingia vipi kwenye matatizo ya kujitakia ya Chadema?

Mwenyekiti wa Chadema wa Mkoa wa Kigoma alishamshauri Dr. Slaa aahirishe safari yake, lakini Slaa amebisha. Hapo msitafute mchawi...
 
Mkuu u are a great thinker, hapo 100 100
 
Ccm hemu ccm hemu aaaaa hali ni mbaya kwenye hiki chama kikongwe kila mbinu ya kuuiua chadema imeshindikana
 
maandamano ni haki yao...acha waeleze hisia zao lakini maamuzi yatasimama kwa mujibu wa katiba ya chama!
 
Mkuu hebu tuhabarishe vizuri hiyo hayo matangazo ni watu gani wanaopinga mkutano wa Dr. Slaa?
 
Ni sawa,Chadema tusipanic maandamano ni haki ya kila raia,tuwaache waandamane,tuwasikilize wanasema nini lakini maamuzi yafanywe na vikao halali vya Chama,sioni shida yoyote katika maandamano!
 
CCM inaingia vipi kwenye matatizo ya kujitakia ya Chadema?

Mwenyekiti wa Chadema wa Mkoa wa Kigoma alishamshauri Dr. Slaa aahirishe safari yake, lakini Slaa amebisha. Hapo msitafute mchawi...

Dakitareeeee akili mgando dakitareeee!!
 
CCM inaingia vipi kwenye matatizo ya kujitakia ya Chadema?

Mwenyekiti wa Chadema wa Mkoa wa Kigoma alishamshauri Dr. Slaa aahirishe safari yake, lakini Slaa amebisha. Hapo msitafute mchawi...

Ahairishe ili kiwe nini? Mwache mzee wa watu akijenge chama na hao wanaompinga lazima wajue kuwa siyo lazima wawe cdm waende nccr, tlp au ccm na cuf.Ni mawazo ya kijinga kung'ang'ania chama kwa kuleta fujo.
 
Sasa ndo naanza kuwaelewa baadhi ya member humu wanaodai kuwa kigoma kwa shughuli maalum! Hivi nani anagharamikia upuuzi huu? na kwa faida gani? je, haya tunayoyasikia kwa sasa yana faida gani kwa wana kigoma? Anyway kila la kheri ktk mission yenu lakini kumbukenk jambo moja" wanakigoma siyo wajinga kiasi hicho mnachofikiri, siku.moja ukweli utajulikana na watawapiga kwa.mawe".
 
Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…