Maandamano makubwa kupinga ujio wa Dk Slaa Kigoma Mjini

mkigoma

JF-Expert Member
Jul 26, 2011
1,180
309
Nipo hapa mwanga naona gari linapita likitangaza Maandamano ya kupinga ujio wa Dk Slaa mjini kigoma, Maandamano hayo yataanzia mwandiga hadi viwanja vya community center ambapo ndipo Dk Slaa anategemea kufanya mkutano wa hadhara kesho, Maandamano yatafanyika tarehe 8.12.2013 kesho jumapili. Maandamano yataanza saa 2 asubuhi. Gari kwa sasa limeelekea maaneo ya ujiji.

Mkuu sixgates

Hawa Chadema wanatapata tu wawatishie maisha na hawa hapa chini, tuliwaambia Zitto ni zaidi ya Lema, Mbowe, Mnyika, Lissu, na wengine wote hawakutaka kutusikia.

1453392_1494386134120749_1478911311_n.jpg
1476616_369232366556744_1162302594_n.jpg
LIVE KUTOKA KIGOMA.Kinachoendelea KIGOMA muda huu na hata kwenye kwenye Maandamano Makubwa ni hiki wanachama wa CHADEMA wakiandamana kupinga ujio wa Dr SLAA na viongozi wenzake mkoani. Ukweli ni Kwamba Dr. Slaa amekutana na wakati Mgumu akiwa Kigoma. Picha zingine zitakuja na saa mbili Usiku ITV, TBC NA STAR TV wataonesha hali ya leo Kigoma walivyojitokeza Kupinga Ujio wa Dr. Slaa.

Ndugu zangu

Ili tuendelee tunahitaji fikra mpya za kujenga, kama kila kijana mwenye wazo jipya atapingwa kwenye hivi vyama vyetu vya siasa hatutafika mbali.

Viongozi wa juu wa Chadema wamekuwa wakiendesha ufisadi na ubabe kwenye matumizi ya ruzuku ya chama. Kwa muda mrefu imekuwa kila anayejaribu kuhoji matumizi ya pesa za ruzuku ya chama anapewa jina la Msaliti au anatumiwa na CCM. Kwao Usaliti na Uasi vina maana moja nayo ni "Mtu yeyote anayehoji jambo lolote linaloonekana kugusa maslahi ya viongozi wa juu au kutaka kugombea nafasi zao"

CCM imekuwa ikitumika kama kichaka cha mafisadi hao wa Chadema kujificha kwa kuwasakizia CCM kila jambo baya linalitokea Chadema. Sasa wananchi wameshawajua. Napendekeza OPARESHENI TIMUA DR.SLAA NA MBOWE iendelee nchi nzima. Hawa wazee ni walevi wa madaraka wakipewa nchi tutauza mpaka soksi.

Shime wanachadema na wazalendo wote wanaojitambua fukuza wabinafsi hao wajifunze kuwa upepo mzuri unategemea matendo mene na si jina la chama. Hongera wanakigoma kwa kumtimua Dr. Slaa. Mwanza tunajiandaa kumfukuza Mbowe ambaye tumesikia anakuja tarehe 14 mwezi huu na atafikia kwenye Hoteli ya Vijana wa Lowasa akina peter Makere Pale Goldcrest.

Haiingii akilini Peter Makere ni mfanyakazi wa mmoja wa wafadhili wa Friends of Lowasa halafu huyo huyo ndiye Lema amempa Uenyekiti wa M4C kanda huu ni unafiuki. Harakati za wanachama kukikomboa chama ni muhimu sana wakati huu.

MBOWE NA SLAA WAMESHINDWA KUWATENDEA HAKI WANACHAMA WAO HAWAWEZI KUWATENDEA HAKI WANANCHI.
 
Hakuna tatizo kama maandamano yenyewe yamepata baraka (kibali) kutoka mamlaka zinazolinda usalama (polisi), na pia waandamanaji wasivunje sheria. Kuandamana ni haki yao! Hata hivyo CHADEMA wanatakiwa kupokea maandamano hayo na kuwasikiliza!
 
Aache wafanye yao, Lakini M4C haina masikio wala direction, yenyewe ni kama kimbunga inapita popote na wakat wowote bila kujali che wala chi, Slaa usiogope twende tu tuendeleze mapambano.
 
polisi kama wameruhusu maandamano na siku hiyohiyo dr Slaa ana kikao wanataka watu wauane. vita iliyoanzia kongo ikpitia Burundi na Rwanda naona sasa RPC anaikaribisha Kigoma. nimeamini vita ya wenyewe kwa wenyewe itaanzia Kigoma na Zito atakuwa ndo mwanzilishi.
 
  • Thanks
Reactions: mmh
kweli CCM sasa wamechanganywa sana na ninachopenda wanaangaika lakini kigoma ni cdn na nccr waacheni wapoteze muda wao tuu kwani wakorof tayali wamekamatwa jana
 
kweli CCM sasa wamechanganywa sana na ninachopenda wanaangaika lakini kigoma ni cdn na nccr waacheni wapoteze muda wao tuu kwani wakorof tayali wamekamatwa jana

CCM inaingia vipi kwenye matatizo ya kujitakia ya Chadema?

Mwenyekiti wa Chadema wa Mkoa wa Kigoma alishamshauri Dr. Slaa aahirishe safari yake, lakini Slaa amebisha. Hapo msitafute mchawi...
 
polisi kama wameruhusu maandamano na siku hiyohiyo dr Slaa ana kikao wanataka watu wauane. vita iliyoanzia kongo ikpitia Burundi na Rwanda naona sasa RPC anaikaribisha Kigoma. nimeamini vita ya wenyewe kwa wenyewe itaanzia Kigoma na Zito atakuwa ndo mwanzilishi.

Mkuu u are a great thinker, hapo 100 100
 
Ccm hemu ccm hemu aaaaa hali ni mbaya kwenye hiki chama kikongwe kila mbinu ya kuuiua chadema imeshindikana
 
maandamano ni haki yao...acha waeleze hisia zao lakini maamuzi yatasimama kwa mujibu wa katiba ya chama!
 
Nipo hapa mwanga naona gari linapita likitangaza Maandamano ya kupinga ujio wa Dk Slaa mjini kigoma, Maandamano hayo yataanzia mwandiga hadi viwanja vya community center ambapo ndipo Dk Slaa anategemea kufanya mkutano wa hadhara kesho, Maandamano yatafanyika tarehe 8.12.2013 kesho jumapili. Maandamano yataanza saa 2 asubuhi. Gari kwa sasa limeelekea maaneo ya ujiji.

Mkuu hebu tuhabarishe vizuri hiyo hayo matangazo ni watu gani wanaopinga mkutano wa Dr. Slaa?
 
Ni sawa,Chadema tusipanic maandamano ni haki ya kila raia,tuwaache waandamane,tuwasikilize wanasema nini lakini maamuzi yafanywe na vikao halali vya Chama,sioni shida yoyote katika maandamano!
 
CCM inaingia vipi kwenye matatizo ya kujitakia ya Chadema?

Mwenyekiti wa Chadema wa Mkoa wa Kigoma alishamshauri Dr. Slaa aahirishe safari yake, lakini Slaa amebisha. Hapo msitafute mchawi...

Dakitareeeee akili mgando dakitareeee!!
 
CCM inaingia vipi kwenye matatizo ya kujitakia ya Chadema?

Mwenyekiti wa Chadema wa Mkoa wa Kigoma alishamshauri Dr. Slaa aahirishe safari yake, lakini Slaa amebisha. Hapo msitafute mchawi...

Ahairishe ili kiwe nini? Mwache mzee wa watu akijenge chama na hao wanaompinga lazima wajue kuwa siyo lazima wawe cdm waende nccr, tlp au ccm na cuf.Ni mawazo ya kijinga kung'ang'ania chama kwa kuleta fujo.
 
Nipo hapa mwanga naona gari linapita likitangaza Maandamano ya kupinga ujio wa Dk Slaa mjini kigoma, Maandamano hayo yataanzia mwandiga hadi viwanja vya community center ambapo ndipo Dk Slaa anategemea kufanya mkutano wa hadhara kesho, Maandamano yatafanyika tarehe 8.12.2013 kesho jumapili. Maandamano yataanza saa 2 asubuhi. Gari kwa sasa limeelekea maaneo ya ujiji.

Sasa ndo naanza kuwaelewa baadhi ya member humu wanaodai kuwa kigoma kwa shughuli maalum! Hivi nani anagharamikia upuuzi huu? na kwa faida gani? je, haya tunayoyasikia kwa sasa yana faida gani kwa wana kigoma? Anyway kila la kheri ktk mission yenu lakini kumbukenk jambo moja" wanakigoma siyo wajinga kiasi hicho mnachofikiri, siku.moja ukweli utajulikana na watawapiga kwa.mawe".
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom