Maandamano kupinga sheria iliyopitishwa- mifuko ya jamii (ppf/nssf) kuchukua 55 years | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maandamano kupinga sheria iliyopitishwa- mifuko ya jamii (ppf/nssf) kuchukua 55 years

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by rugumye, Jul 31, 2012.

 1. rugumye

  rugumye JF-Expert Member

  #1
  Jul 31, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wanajamii watu wengi hasa walio kwenye sekta binafsi wanaopenda kuandamana kupinga sheria iliyopitishwa na serikali Mnaombwa kutoa mawzo yenu hapa, ni kupinga sheria ya mifuko ya jamii kukalia michango ya wanachama mpaka wafikishe umri wa miaka 55. Inasadikika kuwa serikali yetu imekopa pesa nyingi kutoka katika mifuko hii kiasi kwamba mifuko imeathirika sana. Ili kuweza kupunguza usumbufu, serikali imelazimika kutunga sheria ili iweze kuchota mipesa hii bila matatizo. kama mipesa ile ya EPA iliyokuwa imetulia pale BOT.

  Uzoefu kutoka nchi za wenzetu mifuko hii inawasaidia sana wanachama kwaani wanaweza kukopa kujemgewa nyumba, mikopo ya pesa, na fursa nyingi sana tofauti na hapa Bongo. Mfano mimi nilichangia NSSF kwa miaka 8, lakini pesa niliyopata haikuwa na interest (faida) hata kidogo. Nilichopata ilikuwa jumla ya michango yangu niliyokuwa nimechangia tu huku mifuko ikiwa imewekeza pesa yangu kwenye majengo marefu na miradi mingine mingi. (Ushahidi ninao kama NSSF wakiutaka).

  Hivyo tusipo simama wenyewe tusifikiri bunge lina jipya kwaani sheria ilipitishwa na hao hao wabunge.

  Wajumbe tunaomba mawazo yenu lini tuandamane juu ya swala hili. kuna watu watatafuta kibari kutoka polisi. Ni maandamano ya amani bila fujo.

  KARIBUNI.
   
 2. Msolopagazi

  Msolopagazi JF-Expert Member

  #2
  Jul 31, 2012
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 659
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Yanafanyika lini na wapi?
   
 3. N

  NG'ONGOVE Senior Member

  #3
  Jul 31, 2012
  Joined: Apr 28, 2012
  Messages: 151
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tujuze haraka tuanze kuelekea huko
   
 4. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #4
  Jul 31, 2012
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,356
  Likes Received: 3,123
  Trophy Points: 280
  Kama kweli wamefanya mabadiliko kwa ajili yetu mi nadhani sisi ndio wenye uamuzi.....wapitishe karatasi ni wangapi wanataka wapate mafao ambayo ni haki yao mpaka miaka 50....nadhani hakuna atakayekubali kwani hizo hela inatakiwa zimsaidie mhusika pale tu aachapo/aachishwapo kazi.....nisubiri miaka hiyo ili iweje?
  Ktk kitu ambacho kiwete,serikali na ccm watajuta ni kugusa mahali nyeti sana km hapo sio kwa manufaa ya mfanyakazi ila kwa manufaa ya kifisadi ya viongozi
   
 5. BUBE

  BUBE JF-Expert Member

  #5
  Jul 31, 2012
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 844
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Sheria hii ni ya kipuuzi na kandamizi kwa maoni yangu. Huwezi kumwambia mtu ambaye anafanyakazi kwa contract ya miaka 1 au 3 akimaliza anatafuta kazi kwingine na akikosa anaugulia yeye na wanawe kwamba asubiri miaka 55! Wakati huo watoto wake watakuwa chokoraa, yeye atageuka chapombe na inawezekana akafa kihoro within 3 years baada ya kukosa kazi. Serikali na whoever came with that idea hawakufanya consultations na watu husika! Hiyo wamwambie muajiriwa wa umma ambaye once employed anakuwa na uhakika wa kukaa kazini (sometimes hata akiiba -ilmradi asipelekwe mahakamani.asigundulike). Makampuni binafsi hata ujuzi ukipungua unapigwa chini kwa kuwa kila mara wanataka kushindana kibiashara. Hata mtu akiumia kazini anaweza kuvumiliwa kwa muda kisha anapigwa chini. Waulize mifuko ya afya ya jamii kwa mfano, kwa nini huduma inaweza kukatwa pale tu unapokuwa huendelei kuchangia?
  Mbaya zaidi ni kwamba makampuni ambayo yanapewa mikopo ya fedha zetu hizi huwa hayashinikizwi kuwaajiri watoto/wadogo zetu bali wana uhuru kuajiri watu kutoka pakstan thailand na kwingineko. Hii sheria imetungwa usiku, na kupitishwa usiku (gizani) sidhani kama watu makini wangeweza kujaidili hali halisi na kuja na mapendekezo ya sera/sheria ya namna hii
   
 6. Paul Ndugulile

  Paul Ndugulile Member

  #6
  Jul 31, 2012
  Joined: Jul 15, 2012
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Hii sheria ni kandamizi, hakuna ajira iliyo bora hapa Tz sekta binafsi wala Makampuni ni mengi yanaajira za manyanyaso ukimaliza miaka miwili umejitahidi sana.Hivyo kusubiri miaka 55 ndipo nilipwe mafao yangu ni unyanyasaji,Pia muda wa kuishi umepungua sambamba na maradhi ya kuambukiza ni dhahili wengi hatufiki umri huo.Mbona ninyi watunga sheria hamjaweka mnapostaafu mkae miaka 100 ndipo mlipwe mafao yenu? Au ninyi sio wazalendo wa Nchi hii! Sheria hii ni kwa wanyonge tu.
   
 7. g

  gabz Member

  #7
  Jul 31, 2012
  Joined: Jul 30, 2012
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yabidi kushiriki maana serikali hii bila migomo mambo hayakwendi kwa kweli.....let stand together as one and say NO to this system oppression.
   
 8. Ernesto Che

  Ernesto Che JF-Expert Member

  #8
  Jul 31, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,117
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  tunaandamana lini hebu jamani tujulisheni TUCTA mpo wapi??
   
 9. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #9
  Jul 31, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  nasikia waliipitisha kimya kimya halafu mkuu wakaya akasaini ikawa kazi ya kulimbia tu taifa ambapo aliachiwa dada Irene aseme tu sbabu watz wengi ni watu wa ndio mzee...
   
 10. SASATELE

  SASATELE Senior Member

  #10
  Jul 31, 2012
  Joined: Sep 12, 2011
  Messages: 169
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  A loud public outrcy is necessary in this situation!! jamani kama wewe ni mfanyakazi na hujawahi kuona umuhimu wa kuandamama angalau tujumuike katika maandamano haya ya amani
  Ni lini na wapi? I can't wait!
  Your right will not come in a silver plater!!
   
 11. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #11
  Jul 31, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Dawa hapa ni

  1.Kuruhusu mtu anayeona mfumo huu haumfai kutochangia kabisa, awe na uhuru wa kujiwekea akiba yeye mwenyewe bila ya kushurutishwa kuweka katika mifuko hii, kwani wengine tushaanza kuona element za mifuko hii kutumika kama njia za kuwachangisha wananchi kwa manufaa ya wachache. Kwa hiyo kama mtu hataki asilazimishwe, si mafao yake bwana?

  2.Soko huria kuruhusu mashirika tofauti kuweza kuingia katika huduma hii, kuleta ushindani na kuondoa ukiritimba wa mashirika haya ya umma.

  3. Hata kama mashirika ya umma yakikataza kutoa maslahi kabla ya miaka 55, kuwe na mianya ya mtu kuweza kupewa mikopo au kutoa kiasi cha fedha kwa sababu maalum kama za ugumu maalum wa maisha, masomo, ujenzi etc.

  Haiyumkiniki mtu ambaye hajafika miaka 55 anaumwa, anahitaji hela za kumfanyia operesheni, hela hana zaidi ya hizi alizochangia kwenye mifuko hii, halafu mnamwambia hawezi kuchukua mpaka afikishe miaka 55.
   
Loading...