Maandamano: Hali iliyotoweka sasa yarudi tena! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maandamano: Hali iliyotoweka sasa yarudi tena!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Dec 24, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Dec 24, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  WanaJF:

  Baada ya JKI kuingia madarakani miaka mitano iliyopita, mivutano baina ya vyama vya siasa vya upinzani na serikali (yaani polisi) kuhusu maandamano ilionekana kutoweka kabisa.

  Wengi waliipongeza serikali ya JK kwa kuiondoa mivutano hiyo ambayo ilikuwapo kwa takribankipindi chote cha Mkapa. Itakumbukwa yule IGP Mahita daima alikuwa anavutana na wapinzani, wakati huo CUF (iliyokuwa na nguvu kubwa) kuhusu maombi yao ya kufanya maandamano.

  Mahita aliibua ile kauli yake maarufu dhidi ya CUF: “Kama nyie ngangari, basi mie ni ngunguri.”

  Askari wake walikuwa wanatembeza virungu dhidi ya wafuasi wa CUF na kuwaumiza vibaya, akiwemo hata mwenyekiti wao Lipumba ambaye aliwahi kuvunjwa mkono.

  Miaka mitano ya JK tumeona maandamano yakiruhusiwa bila pingamizi na polisi wakiyalinda, na yalifanyika kwa amani, hadi watu wakafikia kusema; “kumbe ni polisi ndiyo huwa wanaanzisha vurugu kwenye maandamano.”

  Baada ya uchaguzi huu tunaona tena hali ya wakati wa Mkapa na Mahita inaanza kujirudia polepole – maandamano ya wapinzani – hasa ya Chadema (chama cha upinzani ambacho sasa ndiyo chenye nguvu) yanakataliwa kwa sababu zisizo na msingi.

  Tumeshuhudia kule Arusha wiki hii, maandamano ya Chadema yakikataliwa eti kwa kisingizio kwamba idara ya polisi haina askari wa kuyalinda – huku ikipeleka kwenye uwanja wa mkutano askari kibao kwa lengo la kuyazuia maandamano.

  Kulikoni serikali ya JK sasa? Inaogopa nini? Kwa nini isiendeleze tu sera yake ya awali ya kuyaruhusu maandamano na kuyalinda kama ilivyokuwa katika miaka yake mitano iliyopita?
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Dec 24, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mi nadhani ni woga mkubwa umemwingia JK kutokana na kwamba huenda hakushinda uchaguzi.
   
 3. babayah67

  babayah67 JF-Expert Member

  #3
  Dec 24, 2010
  Joined: Mar 28, 2008
  Messages: 493
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  SI Kuwa huenda hakushinda bali HAKUSHINDA!!!!!!!!
  :redfaces::redfaces::redfaces:
   
 4. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #4
  Dec 24, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,175
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280

  JK aliruhusu maandamano kwa lengo la kuwafurahisha wazungu anakoendaga kuhemea ili waTZ tusife na njaa. si unajua wazungu wanaheshimu demokrasia? jk alikuwa anajifanya naye ni mmoja wao.

  sasa wazungu wanamuona kama mvurugaji wa demokrasia na serikali yake ina kashfa za rushwa kubwa-kubwa. wazungu wameamua kumtosa. hawezi kuruhusu tena maanadamano kwa sababu hayana faida tena kwake yeye binafsi na utwala wake.
   
 5. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #5
  Dec 24, 2010
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  kwa sasa hahitaji tena kura zenu, hata akitoa kipondo hana shida na nyinyi, si mlimchagua?
   
 6. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #6
  Dec 24, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,496
  Likes Received: 2,742
  Trophy Points: 280
  Hakushinda.................... Huoni hata kulihutubia taifa anashindwa hata siku ya uhuru. Hivi zile hotuba za mwezi bado zipo?? Matatizo amejitafutia mwenyewe kwa kulazimisha matokeo. Sasa roho inamsuta.
   
 7. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #7
  Dec 24, 2010
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  mwacheni jamani mtoto wa watu kwa sasa bado yuko kwa Obama anakula raha kidogo,atakapopumzika basi atapata nguvu za kuhutubia, sio kazi rahisi jamani kuhutubia kila mwezi maana mbaya zaidi haoni chochote alichokifanya tangu aingie madarakani zaidi ya bei za vitu kupanda maradufu, msishangae jamaa anakuja na wazo la kuibinafisisha IKULU walau kwa miaka mitatu ya term yake.
   
Loading...