Maandalizi ya kushinda uchaguzi

Nov 6, 2016
73
185
MAANDALIZI YA KUSHINDA UCHAGUZI.

Na Comrade Ally Maftah

Uchaguzi ni mchakato unaohitaji maandalizi ya muda mrefu yenye umakini mkubwa, maandalizi hayo yanahusisha kujenga jumuia inayokupa nguvu kifikra na kiuchumi, vifuatavyo ni vitu muhimu vya kuzingatia katika kujenga ushawishi

1. Jenga uaminifu kwa wapiga kura wako kwa kuwaambia kuhusu Imani yako na itikadi yako kisiasa.

2. Jipe mwonekano unaotafsiri jambo linalohusu jamii inayokuzunguka, inawezekana ukawa na mwonekano wa upatanishi, upambanaji, kuwainua watu kifikra au kiuchumi.

3. Shiriki katika matukio mbalimbali yanayopewa heshima katika aina a jamii utakaoiomba kura.

4. Toa michango katika mambo ya kimaendeleo katika jamii hiyo.

5. Andaa wasifu wako unaoeleza kuhusu elimu na ujuzi ulionao ikiwemo na njia unazotumia kupata kipato chako.

6. Kuwa na kauli mbiu ambayo itakutambulisha wewe katika kampeni zako

ZINGATIO ; KAMPENI KUBWA YA MGOMBEA HUFANIKA KABLA YA HARAKATI ZA KUGOMBEA NAFASI KUTANGAZWA, MWANASIASA MZURI NI YULE ANAEKUWA ANAJIANDAA NA UCHAGUZI KABLA YA UCHAGUZI WENYEWE, KITAALAMU WANASEMA MWISHO WA UCHAGUZI NDIO MWANZO MZURI WA KAMPENI ZAKO

NIMEKUTUMIA RASIMU YA KITABU CHANGU CHA SIASA KAZI MAARIFA, KITABU KAMILI KITATOKA TAREHE 15 MAY 2024

NDIMI
Comrade Ally Maftah
Mjumbe Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam
Mjumbe Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam
Msanii na Mdau wa Basata.
Mwandishi na Mdau wa Maktaba Kuu.
Mwanzilishi na Mmiliki wa CAM STORE - DUKA KUU
JITU LA MIRABA
CHALINENEE
1714525754638.jpg
 
Mnaandika weeeee alafu mnakuja kuiba kura au kulazimisha matokeo kwa ubabe. Ujinga mtupu!
 
Uchaguzi ni mchakato unaohitaji maandalizi ya muda mrefu yenye umakini mkubwa,
Nini ambacho huwa kinasababusha wagombea wengi wa upinzani kushidnwa kujaza fomu vizuri na wengi wao kuenguliwa na wasimamizi wa uchaguzi?
 
Back
Top Bottom