Wakuu,
Kuna anayefahamu maana ya msemo 'waja leo waondoka leo'? Kama sijakosea watu kuutumia kuzungumzia mji wa Tanga.
Maana yake ni nini? Ningependa kujuzwa tafadhali.
Chanzo cha msemo huu ni wimbo wa Remmy Ongala, nafikiri unaitwa mdundiko. Ukiusikiliza ndio anamuongelea mpenzi wake anayeelekea kuishi Tanga na anakuja Dar na kurudi Tanga siku hiyo hiyo.Wakuu,
Kuna anayefahamu maana ya msemo 'waja leo waondoka leo'? Kama sijakosea watu kuutumia kuzungumzia mji wa Tanga.
Maana yake ni nini? Ningependa kujuzwa tafadhali.
Huu ni msemo wa kukushawishi usiondoke. "Waja leo waondoka leo?"
Wakazi wa Tanga hawafurahii mgeni aliyekuja aondoke. Tabia na ukarimu wao mara nyingi unamshawishi mgeni asitake kuondoka. Na hata akiondoka atamani kwenda Tanga tena. Hivyo msemo huo uko katika mfumo wa swali la kukushangaa wewe mgeni unayekuja na kutaka kuondoka haraka haraka. Ukiingia Tanga utaona kibao cha kukukaribisha,lakini ukiondoka hutaona kibao cha kukuaga.