JustineKitenge2016
Member
- Jul 17, 2016
- 46
- 62
Mwanzoni nilipofeli kidato cha nne mwaka wa majanga 2012 nilihisi ndo mwisho wa kuiona degree kutokana na maneno ya kukatishana tamaa kutoka kwa baadhi ya ndugu na ukilinganisha wanafunzi wengi marafiki zangu walifauru kuendelea na masomo ya kidato cha tano, lakini namshukuru mungu sikukata tamaa nilipambana mwanzo mwisho kuanzia certificate mpaka diploma na leo hii nimechaguliwa kuendelea masomo ya degree mwaka 2016/2017 namshukuru sana mungu kwa jambo hili limezekana. Mimk nawahasa wanajamii forum ambao walikua kwenye hali kama yangu cha nsingi ni kumuomba mungu na kusoma kwa bidii hakuna jambo lisilowezekana