Maana halisi ya Rastafari

Rasta ni harakati,mfumo wa maisha unaojali asili na usawa na hasa kumhusu mwafrika mnyanyaswa,AMANI na UPENDO na maisha ya kiasi ndo msingi wao,na km ujuavyo amani na upendo ni vitu vinaasili ya Mungu na imani ndo maana watu wameikoleza harakati kombozi hii na imani na wakakolezea na kusoma na kufuata agano la kale
 
Haile selassie was a devote christian and a leader of ethiopia tawaedo Orthodox church. .n alivyoenda jamaica he said to his archbishop abune yesehaq " go to jamaica, ths people dnt understand our culture" he said ths after being praised n being called God. . .that mean he denied he is not God. .then why should rasta pray to him?
Definetly true na huyo bishop alikuja akambatiza Bob na familia,Haille alikuwa muumini wa etiopian orthodox na Nesta pia alibatizwa huko kabla hajafa
 
Hii Imani niNoma nakumbuka Bob marley alikataa kukatwa mguu uliokuwa na Cancer hadi ikapanda mwilini akadanja....

Justine Kalikawe naye alikataa kumeza dawa za Hospital anang'ang'ania michicha na mboga za Majani hadi umauti ukamkuta kwa kuugua... hii Imani ni noma.... ila ni vizuri kuwa na imani kwani huwezi tenda mabaya na upole unawafanya wapate wanawake wa Kizungu kwa Urahisi sana.... mimi nilitaka niwe Rastafarian ila nywele zikakataa kufugika zikanyonyoka zote... na Bangi ndio sijawahi ivuta
Ulitaka kulimbukia usichokijua maana ulidhani urasta ni kufuga dread
 
According to tradition Haile Selassie was offspring of King Solomon and Queen Sheba,ukifatilia historia ras Tafari mvt in Jamaica ambao waliamini Haile Selassie ni Massiah yote ilikuwa ni katika ukomboz wa mtu mweusi na hata mwenye Haile mpaka last time alikuwa ni ethiopian orthodox na anaheshimika na Marastafari wote na yeye mwenyewe alisema yeye sio Mungu but Massiah of God..,historia yake ni ndefu sana kuanzia asili ya neno Ras Tafari na movement ilivyoanzia Jamaica..
Jamaa hakuwahi jiita massiah bro,orthodox wanaamini juu ya Yesu kuwa ndo massiah na hawana tofauti sana na wakatoliki,sasa km Selassie alikuwa muumini wa imani inayoamini kuwa Yesu ndo Massiah inawezekanaje yy ajiite massiah,acheni kudanganya watu,huyu alikuwa mfarume mtiifu wa imani yake ya Ethiopian orthodox
 
Haile Selassie ni katika uzao wa King Solomon uko Israel(fatilia historia ya Ethiopia na Israel),tunamtambua Jesus kama massiah wa uzao wa Daudi,msikilize Alpha.
Pia reggae is abt message,hizo nyingine ni ubabylon,kupitia conscious message inakupeleka kutambua dunia,jins tunavyoishi na kwa nini na maisha ya baadae.
Haile Salassie hakuwa Mungu na alikiri mwenyewe akiwa exile yeye sio Mungu na katika maisha yake alikuwa mfuasi wa Ethiopian orthodox..
Rastafari sio kwamba hawatumii agano jipya,linatumika sana na waimbaji wengi wamelizungumzia ispokuwa wanabezi katika A.kale kutokana na iman ya uzao wa asili Haile Salassie katika a.kale kupitia King Solomon
Hakuna uthibitisho wa kimaandiko kuwa Selassie alikuwa mmoja wa uzao wa solomoni,japo waisraeli na waethiopia wanamuingiliano wa kihistoria na kuna mchanganyiko wadamu kiasi kuna waisraeli weusi,lkn hata km ana blood link haimaanishi chochote kwa yy kuonwa mtakatifu ama astahiliye kuabudiwa maana hata solomoni mwenyewe hakuabudiwa,jamaa anaheshimiwa km mfalme mtetezi wa uafrika mlezi wa harakati za kumkomboa MTU mweusi,hausiki chochote na kuabudika maana hata yy mwenyewe alikuwa muumini na alimtambua Yesu km massiah maana ndoimani ya orthodox hyo
 
Tambua uwepo wa yesu na mohd lkn usifuate mafundisho yao. Hapohapo uwe ustadh au mchungaji! Sielewi uno na uno nshike upi?
Hili ni fundisho la mtaani la kubumbwa hasa watu waliofuata urasta kwa kusumwa na uvutaji bangi,orthodox dhehebu kongwe ambalo sellasie aliabudu wanamtambua Yesu km bwana na mwokozi,sellasie alibatizwa ktk jina la Kristo km batizo zilivyo kumkili Kristo,na alikuwa muumini wa dini hyo inayomtambua na kufuata mafundisho ya kiKristo maana orthodox ni uKristo hawanabtofauti kabisa na wakatoliki maana wanamuheshimu na kumuadhimisha hata Mariamu kwa nafasi ya Kuwa mama wa mwokozi km wakatoliki
 
Mkuu kama umesoma bandiko lote kwa utulivu utaelewa kuwa Haile Selassie alichaguliwa na waamini wa Raistafari kuwa kiongozi wetu, hilo halina maana kuwa yeye ndie muanzilisha, Urasta ulikuwepo tangu Karne ya kwanza ukiwa chini ya binadamu mweusi Nimrodi mmoja ya uzao wa Nuhu,

Ukaendelea kuenezwa na falme za akina Solomoni na hadi kuingia Ethiopia na kuweka masinagogo pale, Wayahudi walipoanzisha dini yao ya uyahudi yari walikuta Urastafari upo ukiabudiwa katika Nazareti,

Warumi nao walipoivamia Yuda na kuanza kueneza utawala wao walifika mpaka Ethiopia nakukuta tayari kuna masinagogi,

Karne ya 19 urastafari ulishamiri zaidi Jamaica hasa baada ya harakati za binadamu mweusi kujikomboa kutoka utumwani
Tukubaliane Haille Selassie alikuwa mkristo muothodox
 
Kwanza ili tumfahamu vema Nimrodi nivema tukaanza kurejea nyuma kwanza kuyajua haya,

Wazungu 90% ni Majini:


Kwakutumia historia ya binadamu kibiblia, ukichambua kila uzao na sambuli zake unaweza kubainisha wazi hilo nilisemalo, japo laweza kuwa zito kwa wengine.


Kwa wale muaminio biblia mnaweza kukubaliana na mimi kuwa sababu kuu ya Mungu kuiangamiza dunia enzi za Nuhu, ni kutokana na wanadamu kumuasi mungu, maasi yalikuwa yakufuru hasa yakihusisha mwingiliano wa majini na binadamu, wanyama na binadamu nk na baada ya angamizo hilo, manusura walikuwa ni Nuhu, wanawe, mke wake, na kila kiume kibaya na chema aliviokoa mke na mme. Mwanzo 7:1-11


Hapa tunaona kuwa na majini yaliokolewa na Nuhu, Sasa tukirejea katika masimulizi yetu tunaona sasa baada ya Nuhu kuokolewa na safina, wanae watatu wakiume ambao tayari walikuwa wameoa (enzi za gharika) mmoja wao Yafethi alikuwa kaoa jini, wakati wawili Shemu na Hamu wao biblia inasema walioa mahali ambapo si chukizo mbele za Mungu. Mwanzo 10:1-7


Uzao wa wana wa Nuhu ndio unatupatia ukweli wa nikisemacho, kwanza tunaona kuwa wana wa Yafethi alieoa jini ni, Gomeri (Ujerumani), Magogu (Cambridge UK ), Madai (Hispania), Yavana (Italia), Tubali au Yunani (Ugiriki), Mesheki (Lebano) na Tirasi (Ufaransa), Mpaka hapotumeona uzao wenye ushirika na majini wa Yafethi

Sasa tuangalie uzao Hamu unaotajwa kuwa Mungu aliupenda na kuupa baraka tele, uzao huo ni Kushi (Ethiopia), Misri (Misri), Kanaani (Israel) na Putu (Libya)

Mwanzo 10:21-23
Tunasoma yakuwa wana wa Shemu ambe ni sehemu ya kipenzi cha Mungu, ni Elamu (Saudi Arabia), Ashuru (Syria), Arfaksadi (Kuweit), Ludi (Jordan), na Aramu (Qatar)

Mpaka hapo tumepata mwangaza kuwa uzao wa Yafethi wenye tokezo la majini/uovu ndio uzao wa mataifa karibu yote ya Ulaya. nauzao wa Hamu na Shamu ndio uzao uliopewa neema na muumba hii ni kwamujibu wa maandiko ya kiroho.

Kwamaandiko hayo tunaamini kabisa kuwa Mashariki ya kati, na Afrika ndio maeneo muhimu ambayo mungu aliwabarikia watu wake.


Hata ukitumia Kuruani takatifu hayo yote yanabainisha wazi kabisa.

Kwamsaada zaidi rejea Mwanzo 4:16-24, Ufunuo 16:13-15, Ufunuo 20:7-8, Ezekieli 27:12-14, Ezekiel 38:1-9


Kwakupanua wigo wa mjadala nje ya biblia hasa wale wenzangu waaminio Freemasonry ijapokuwa watetezi wake hupinga kuwa si ushetani/ujini, watambue kuwa uzao wa asili wa freemasonry ni Magogu (Cambridge UK) japo katika historia inasema ni Scotland UK

Haya ndugu zangu nawakaribisha katika tafakuri njema
Wapi maandiko yanaonesha Nuhu aliokoa majini,andiko toka kitabu gani,
 
Iko hivi.
Hallelu YAH, Hallelu JAH, Asifiwe MUNGU, BWANA Asifiwe, Praise THE LORD .

YAHWE, JAH , JAH, MUNGU, BWANA MUNGU, THE LORD, THE ALMIGHTY GOD, MWENYEZI MUNGU. Ndiyo huyo huyo ni tofauti ya Lugha na mahali tu.
Hivi unajua hata jina Yahwe lilikosewa kimatamshi ndo likaandikwa hivyo,awali jina la Mungu kwa waisraeli halikutamkwa sababu nitakatifu sana,lilisomwa Mara moja tu kwa mwaka tena na kuhani,nalo lilikuwa halijaandikwa Yaweh Bali zilikuwa tu ni herusi zisizotamkika,wakati wa ukristo na ufasiri wa maandiko kutoka lugha asili kuja za sasa ndo kimakosa ya pronounsiation likatamkwa YAHWEH lkn kiasili haliko hivyo na mpaka sasa wayahudi wanataja herufi tatu tu
 
Nyama ina ubaya gani kwa Rastafari?
Kiasili binadamu hakuumbwa kula nyama,angalia hata mfumo wa uyeyushaji chakula,sisi kiasili ni vegetarian siyo canivorus angalia hata meno yetu yanakupa ushahidi,nyama tulianza kula baada ya shida ya ghalika ambapo mimea yote iliteketea,
 
Mkuu mbona swali lako limejibiwa vema katika uzi huu pale juu tu?

Hebu tulia soma vema utaona kuwa,
GABRIEL HAILE SELASIE I aliyekuwa kiongozi wa nchi ya Ethiopia ni moja kati ya watu waliochangia kukuza imani ya Rasta ulimwenguni na ndipo jumuiya ya Rastafariani ilipoamua kumteua kuwa kiongozi wa Rastafarian ulimwenguni.
Kuna kitu fikiria kutoka ktk jibu lako,
Haille Selassie alikuwa Orthodox(Mkristo)
Kateuliwa na marasta duniani kuwa kiongozi wa marasta(ambao wanaamini haileselasie ni massiah)
Inamaana ukisema Haille Selassie ni massiah unamaana ni massiah kwa kuteuliwa na si kwa msingi wa rasta kuwa ni Yesu aliyekuja Mara ya pili,
Lkn pia hata kumpa ukabila la yuda inamaana ni jambo la kupewa tu,
Yy alikuwa Mkristo wa thehebu la orthodox,Mkristo mtiifu kabisa kwa Kristo anakuaje tena yy ndo messiah tena,
Jamaa alikuwa mfalme wa kawaida tu aliyepigania uafrika na umoja wetu,ndo maana nasema Rastafarian is just a Blackman revolutionary movement,baaaaasi siyo dini km mlivyoichomekea vitu kibao,
Sema msingi wa upendo ndo umefanya muone na kuifanya imani ama dini,maana Upendo ndo msingi wa mafundisho ya Mungu maana hata Mungu mwenyewe ni Pendo
 
Hili swali lingejibiwa kwa weledi basi urastafari ungefahamika vizuri:
1)....mkuu naomba ni fahamu nini maana ya kutambua uwepo wa Yesu, na mnatambua kwa level gani,

kwanini mnautumia bible katika imani yenu..?

2)....unasema rege ni sehemu ya ibada na unatumia kuwasiliana na Mungu, kwanza mungu yupi pili rege inakuunganisha vipi na mungu wakati jumbe zake zinatofautiana kuanzia za matusi, mapenzi za wanaharakati n.k ,mungu wako ni mwanaharakati..?

3)...fafanua kuhusu kipengele hiki kina muhusu nani kwa jina na kwa nini apewe vyeo hivi.. "MHESHIMU KING OF KINGS, THE LION OF JUDAH, ELECT OF GOD, RAS TAFARI MAKONEN, HAILE SELASSIE, THE POWER OF THE TRINITY, KING MESIAH FROM THE ROOT OF KING DAVID IN A SOLOMONIC LINEAGE."

4)...nanukuu .."kumwabudu Haile Selassie" so huyu ndo mungu wenu maana anaye pasa kuabudiwa ni Mungu pekee au nyie mnaabudu kila kiyu mpaka sungura...?

5)...kwetu sisi unapozungumzia bible ni agano jipya na agano la kale ndo unapata biblia so kwa nini
mnasema mnazingatimafundisho mengi ya bible na mnabagua agano jipya...? nukuu "mafundisho mengi ya bible hasa old testament"....

majibu tafadhali...
 
Back
Top Bottom