Maana halisi ya Lowassa kuitosa CCM na madhara yake

Maana halisi ya Lowassa kuitosa CCM na madhara yake

masopakyindi

Platinum Member
Joined
Jul 5, 2011
Posts
18,770
Reaction score
14,862
Ni wazi sasa lile jipu lilokuwa linauma limepasuka.

Lowassa kaitosa CCM!

Hili kwa viwango vyovyote si jambo dogo. Nyimbo za mshikamano, makundi na amani ndani ya CCM hazina maana sana kwa hivi sasa. Si uongo CCM imepigwa body blow!

Kwa upande wa pili, Lowassa haeleweki, sijui ni kibri au ushujaa wa tukio hilo, hilo litaeleweka baadaye.
Hata hivyo suala hili limeipeleka demokrasia nje ya viwango vilivyozoekeka, ingawaje Lowassa katumia demokrasia yake mwenyewe.

Sisi bado tuna kumbukumbu nzuri tu za wale walio madarakani, na wenye madaraka makubwa, kutaka kuitosa CCM. Huu ni mchezo hatari wa kisiasa, na ifikapo hapo, script za kisiasa zinagoma. Tunakumbuka ya kina Mwaikambo, mwenyekiti wa baraza la wadhamini wa chama, alipotaka kuhama CCM.

Ndipo inaingia ile kitu inaitwa realpolitik. Unalindwa , umekuzwa, umelelewa na state, sasa leo unaitosa state.

Tukirudi kwenye chama tawala, hasa mwenyekiti wake.
Pengine kama Lowassa atashinda uchaguzi Oktoba,CCM na mwenyekiti wake watakuwa na hali mbaya sana, kwa vigezo vyovyote vile.
Na watu na wanachama itakuwa sawa kujiuliza, huu mtandao umetufikishaje hapa?
 
Lowasa anatamaa ya uongozi, anashida gani hata asipokuwa rais maana kma ni Mali anazo, sasa shida ni nini? Unajua mtu mwenye nia ya kweli huongozwa na muumba wake. Kma ingekuwa ni kweli lowasa anataka awakomboe watz mambo yake yangenyoka tu bila hata kutumia gharama yoyote.
 
Tatizo sasa hivi si hili mkuu
Tatizo ni kwamba kakifikishaje chama chake hapo bila hatua muafaka kuchuliwa?
Boli liko kwa waliombeba.
 
lowasa anataman ikulu hata kwa kujitoa muhanga, kama si tamaa asingeenda cdm na kashfa zote walizomtwika. anadhan huko ndo atapatia urais kumbe nako hapati hata asimamishwe kugombea
 
Wazee wa busara inabidi waingilie kati! Tunaanza kuona free fall ya CCM ikitekelezwa na mtu mmoja tu! Mwenyekiti yuko Ausralia akila maraha, sijui anategemea nini? Hivi haioni hatari inayojiri?
 
Mimi nimekuja kugundua kuwa Lowasa anataka ajenge historia tu ndani ya Tanzania kuwa alipigana na aliweza.
Kwa sababu kama ni utajiri anao na anaweza akala maisha yake yote yaliyobaki.
 
Mimi nimekuja kugundua kuwa Lowasa anataka ajenge historia tu ndani ya Tanzania kuwa alipigana na aliweza.
Kwa sababu kama ni utajiri anao na anaweza akala maisha yake yote yaliyobaki.
Hizo ndoto za urais zinaweza kuleta machafuko nchini.
Maana piga ua, lakini jamaa lazima aende Ikulu, ingekuwa wakati wa zamani hii ni sawa na uhaini kwa CCM.
 
Akili ya kulelewa na ccm ni akili ndogo. Hayo yako huko CCM ilikobaki. Wengine tunasema hilo liccm sio baba wala mama yangu.
Kwa taarifa yako kila mtanzania alikuwa CCM at one point.
 
Wazee wa busara inabidi waingilie kati! Tunaanza kuona free fall ya CCM ikitekelezwa na mtu mmoja tu! Mwenyekiti yuko Ausralia akila maraha, sijui anategemea nini? Hivi haioni hatari inayojiri?

Mtavuna mlichopanda.
Kama mlipanda matikiti mtavuna matikiti, msitegemee Nazi!!!!
 
Kingunge aliwashauri mkae chini muyamalize mukashupaza shingo zenu ngumu kwa kiburi cha ulevi wa madaraka - CCM itatawala milele!
 
Lowasa anatamaa ya uongozi, anashida gani hata asipokuwa rais maana kma ni Mali anazo, sasa shida ni nini? Unajua mtu mwenye nia ya kweli huongozwa na muumba wake. Kma ingekuwa ni kweli lowasa anataka awakomboe watz mambo yake yangenyoka tu bila hata kutumia gharama yoyote.

Kutumia neno kama hilo ni ukomo wa ufinyu wa kufikiri! Kama mtu ni mwana taaluma unasoma mpaka no more school, kama ni mwana riadha unacheza mpaka utwae medali ya dhahabu ya olympics na kuvunja rekodi zote katika wigo wako; kama ni bodia unapiga ngumi mpaka utwae mkanda wa juu kabisa katika uzito wako; na kama ni mwanasiasa unakwenda mpaka ukamate the highest prize in the game; Ikulu! jamani EL ana tofauti gani na binadamu wengine?!

Wazushi, eti ana pesa nyingi apumzike; ngapi! ulijuaje; kama ni wingi wa pesa mbona kina Azam; Dewji; Rostam na Mengi ambao tunaweza kufahamu utajiri wao kifedha mbona bado wanapambana kila kesho wanafungua biashara hii na ile; kwa nini Mengi haambiwi arudi Machame au Shanty town Moshi apumzike?!!?
 
44 Lakini aliyaangalia mateso yao,Aliposikia kilio chao.

45 Akawakumbukia agano lake;Akawahurumia kwa wingi wa fadhili zake;

46 Akawajalia kuhurumiwaNa watu wote waliowateka.

47 Ee BWANA, Mungu wetu, utuokoe,Utukusanye kwa kututoa katika mataifa,Tulishukuru jina lako takatifu,Tuzifanyie shangwe sifa zako.
 
Duuu kumbe kauli ya Merehemu CAPTAIN KOMBA YA KWENDA MSITUNI ILIKUA NA MAANA NYINGINE
 
44 Lakini aliyaangalia mateso yao,Aliposikia kilio chao.

45 Akawakumbukia agano lake;Akawahurumia kwa wingi wa fadhili zake;

46 Akawajalia kuhurumiwaNa watu wote waliowateka.

47 Ee BWANA, Mungu wetu, utuokoe,Utukusanye kwa kututoa katika mataifa,Tulishukuru jina lako takatifu,Tuzifanyie shangwe sifa zako.

Ha ha ha! Lowasa alionekana huko Nigeria kwa Nabii TB Jushua hivi karibuni. Na Nabii huyo alimtabiria mambo mazuri sana hakuna mfano.
 
Back
Top Bottom