Maamuzi ya Prof Ndalichako yanashangaza

Maamuzi ya Prof Ndalichako yanashangaza

Kuna watu tunachangia tu na kurusha makombora probably bila kuwa na uhakika sana na alichokisema Prof. Ndalichako
 
huyu kiumbe ndio maana mzee wa msoga alimtimua ila kwakuwa hatukujua tukawa tuna mtetea,cha ajab mkuu wa kaya aliyeingia madalakan akiwa na details kibao za nchi hii kuanzia bandarin,wizaran,halmashauri nk amemludisha kazn!,anavuluga kila kitu na kila kukicha!

Mkuu wa kaya alipoingia sijui alikuwa na kisas gan maana wengi ambao mzee wa msoga aliwapenda yy aliwafukuza kwa kuwaita majipu na wale ambao mzee wa msoga liwafukuza yy aliwaludisha kazn kama ma-boss,ILA KWAHUYU MAMA MZEE ALIKoSEA KUMLUDISHA NA HATA YY KASHAJUA HILO ILA SIJUI NI NN KINAMZUIA KUMTIMUA au aliyoyasema mh wa jimbo la mtama yalikuwa sahh
namnukuu"anafukuza hovyo kwakuwa hakuwateua yy,ngoja tuone kama na atakaowateua atafukuza hovyo"
 
Wakuu acheni mzaha kwenye elimu.
Mzaha UPI?? Ww toa point zako zieleweke maana imeshakuwa ni mjadala wa kitaifa hata kama unamuunga mkono tupo ambao hatuungi mkono hasa kuweka limit yalazima form6...

Kama anataka diploma zifutwe ..
 
If it is true, it will be the first and only country in the world to have this derailing Idea.
 
Leo nakuunga mkono mkuu..huyu mama atupelekako sasa ni kule tulikotoka...hadi aliyepata kadigrii kake bils form 6 ajiangalie wakti kuna watu wanesota hadi kufikia hpo na wengine ni maprofesa wamejiendeleza ns kufika huko. Kwa hali hii mtoto wa maskinj kujiendeleza ndo itakuwa basi tena

Very true mkuu,kuna watu wengi wamekuwa maprofesa na madaktari bila kupita form 6 huyu mama hajielewi
 
wacha waisome namba du ila katika matamko yote hili na mimi chungu kwangu ksb na mimi ni mmoja wao
 
Waziri wa elimu Ndalichako kwa kuendelea kutoa matamko yako ya utatanishi juu ya elimu ya Tanzania ikiwepo la kuwazuia watu kujiendeleza kielimu ni kujivunjia heshima
Naunga mkono hoja, amekurupuka
 
Mzaha UPI?? Ww toa point zako zieleweke maana imeshakuwa ni mjadala wa kitaifa hata kama unamuunga mkono tupo ambao hatuungi mkono hasa kuweka limit yalazima form6...

Kama anataka diploma zifutwe ..
Diploma za technician zinakubalika.Umesoma hilo tamko au umehadithiwa.
 
Wakati wenzetu wanaenda hivi sie tunarudi kule kweli aliyetuloga kafa :-


*Finland Will Become the First Country in the World to Get Rid of All School Subjects*

Finland’s education system is considered one of the best in the world. In international ratings, it’s always in the top ten. However, the authorities there aren’t ready to rest on their laurels, and they’ve decided to carry through a real revolution in their school system.

Finnish officials want to remove school subjects from the curriculum. There will no longer be any classes in physics, math, literature, history, or geography.
The head of the Department of Education in Helsinki, Marjo Kyllonen, explained the changes:
“There are schools that are teaching in the old-fashioned way which was of benefit in the beginning of the 1900s — but the needs are not the same, and we need something fit for the 21st century.“
Instead of individual subjects, students will study events and phenomena in an interdisciplinary format. For example, the Second World War will be examined from the perspective of history, geography, and math. And by taking the course ”Working in a Cafe," students will absorb a whole body of knowledge about the English language, economics, and communication skills.

This system will be introduced for senior students, beginning at the age of 16. The general idea is that the students ought to choose for themselves which topic or phenomenon they want to study, bearing in mind their ambitions for the future and their capabilities. In this way, no student will have to pass through an entire course on physics or chemistry while all the time thinking to themselves “What do I need to know this for?”
The traditional format of teacher-pupil communication is also going to change. Students will no longer sit behind school desks and wait anxiously to be called upon to answer a question. Instead, they will work together in small groups to discuss problems.

The Finnish education system encourages collective work, which is why the changes will also affect teachers. The school reform will require a great deal of cooperation between teachers of different subjects. Around 70% of teachers in Helsinki have already undertaken preparatory work in line with the new system for presenting information, and, as a result, they’ll get a pay increase. The changes are expected to be complete by 2020.

Sent from my Samsung Galaxy smartphone.
 
Ukistaajabu ya marehemu Joseph Mungai utayaona ya Prof. Joyce Ndalichacko.
 
Very true mkuu,kuna watu wengi wamekuwa maprofesa na madaktari bila kupita form 6 huyu mama hajielewi

Mfano mzuri ni Dr. Bana, Prof. Mathew Luhanga (former VC UDSM) na wengine zaidi ya 20. Hii ni kwa mujibu ya maelezo ya Dr. Bana mwenyewe.
 
MH.NDALICHAKO HII SIYO NECTA
Kwa kipindi cha miaka tisa alifanyakazi ya katibu baraza la mitihani japo marachache nyuma alioneka akifanya masuala ya utafiti na shirika la elimu la aghakhan.Siukatai uwezo wake mkubwa kipindi hicho cha nyuma ingawa amepata bahati baada ya kutoka masomoni anakutana na fursa ya uwaziri......

Siku zote unapoipata fursa ni lazima umuonyeshe aliyekupa kuwa hajapoteza...kwa kipindi kirefu umekuwa ukijishughulisha na matukio badala ya matatizo yanayoikabili sekta ya elimu...

Najaribu kutafuta nini umefanya ili baada ya miaka miwili mitatu tukukumbuke kwa kusema hiki ni cha fulani au unataka tuseme baadae matatizo haya kayaleta ndalichako.......

UTATA WA MH.NDALICHAKO
Kuna vitu Mh waziri amevifanya mpaka unajiuliza huyu ni waziri au nani kasema? Baadhi ni:-

1: Masomo ya sayansi lazima
Hivi waziri ulishindwa kutengeneza miundo mbinu bora kuboresha maslahi ya walimu wa sayansi na kuandaa walimu wakutosha motisha n.k wala ilikuwahaina haja kulazimisha wenyewe wangeenda....

Mfano mzuri jiulize kwanini raisi magufuli ni mwalimu mzuri wa sayansi mzuri aliacha kazi ya ualimu akaenda kiwandani baadae kwenye siasa...sababu zilizomtoa yeye na wengine zinawatoa pia......

2: Ubora wa baadhi ya vyuo vya elimu ya juu....
Kimsingi huwezi ukatibu tatizo hili kwa kusema wachuo fulani wakienda chuo fulani warudie mwaka mmoja nyuma kwa kuwa ubora tofauti ilihali hawa maprofesa ndiyo hao hao kilachuo......

Lakini nikukumbushe kitu ulikuwa huna haja kuwaambia warudie mwaka kwani kila chuo kikuu upo utaratibu wa KUSAP na KUDISCO sasa hivyo ndiyo vilikuwa vipimo kuwa wana ubora au la kuliko kusema asiyetaka arudi kwao(huu ni ubabe).....

Ulichotakiwa kufanya nikuuangalia upya mfumo mzima wa elimu ya juu ikiwezekanafumua wote......

3: Utoaji adhabu kwa wanafunzi
Hili jambo naona mara ya tatu unalirudia kana kwamba waalimu awajitambui vile..kifupi kwa sheria ya adhabu mashuleni hakuna mwalimu mwenye muda mchafu wa kuweza kuitekeleza kila mwalimu anamambo yake ya kufanya......

MWISHO
Kama utaendelea kuwa waziri wa kuzindua na matamko ukifikiri bado upo NECTA na kusahau kuwafikiria walimu tutegemee kushuhudia waziri mbovu ndani ya wizara ya elimu baada ya Magreth Sitta na Mungai kutokea
Ni ukweli kabisaa mpka nkauliza ukiwa t.o toka uanze mpka kumaliza ina maana una maamuzi sahihi kwenye kila kitu
 
Anasema eti kuelekea Tanzania ya viwanda Sayansi ni lazima
nimejiuliza USA na China huko kote walilazimisha wanafunzi wote kusomea Sayansi?
au hii yetu ni 'ubunifu mpya'?
Sayansi inatakiwa iwe option sio lazima kama namuandaa mwanangu aje arithi biashara zangu au ofisi yangu ya sheria sayansi itamsaidia nn,kujenga tz ya viwanda kinachotakiwa ni kufufua vyuo vya maendeleo ya jamii,kufungua vyuo vingi vya ufundi kila kona na kuviboresha,
 
maisha ni magumu sana lakini kila siku tukiamka kuna tamko jipya la kuongezea ugumu wa maisha kwa Mtanzania, matamko makampuni yanafungwa kukwepa gharama kubwa za uendeshaji, madawa hospitalini hakuna , pesa hakuna MATAMKO YANATOSHA KILA MTU ANATAKA KUONEKANA ANATOA TAMKO NA SISI WATU WA CHINI TUWAFUATE.
 
Back
Top Bottom