Maamuzi niliyoyafanya juu ya mke wangu.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maamuzi niliyoyafanya juu ya mke wangu..

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by jamii01, Nov 6, 2011.

 1. jamii01

  jamii01 JF-Expert Member

  #1
  Nov 6, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 1,836
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Siku chache zilizopita niliaweka post yangu kuwa mke wangu habebeki,nashukuru wachangiaji mbali mbali na inbox mlizokuwa mnanitumia nimesoma comments zote zaidi 126,nashukuru sana.

  Kama nilivyotoa haadi ya kuwa leo nitatoa feedback baada ya kuchambua maoni tofauti na message nyingi mlizokuwa mnanitumia nimefanya maamuzi haya Ijumaa kama ifuatavyo..kama nitakuwa nilikosea mtanisamehe.

  1.Mke wangu bado atabaki kuwa mke wangu katika hari yoyote ya maisha hiwe ya shida au tabu..nakumbuka nimetoka naye katika hari ya chini sana bado tukiwa wachumba.hivyo pesa isiwe kigezo cha kututenganisha leo zipo kesho hazipo.zaidi nikiona ametoka nje ya ndoa hapo maamuzi yatakuwa mengine.

  2.Nimeamua kumchukua mtoto wangu na kwenda kukaa kwa wazazi wangu chini ya uangalizi wa wazazi wangu..japo mke wangu atahusika pia.

  3.Nimeamua kumchukua mke wangu na kuishi naye ughaibuni hii itategemea kama atakubali kuacha kazi au la..japo hajanipa jibu nimpe mda wa kutaakari..

  4.Nimemwambia aondoke nyumbani akaishi na wazazi wangu au wazazi wake baada ya kuacha kazi nikifanya utaratibu wa VISA na makazi pia..

  5.Haijalishi atakataa kuacha kazi au la nyumbani asiendelee kukaa..nyumba nimeagiza wakae ndugu zake fulani kwa ajili uangalizi..ila baadhi ya vyumba vitafungwa.

  6.Matumizi yote ya pesa haitapitia tena kwake awasiliane na wazazi wangu pesa ndiyo ataipata pale kwa sababu mtoto yuko pale japo mikoa ni tofauti umbali utakuwa shida pia.

  7.Kuhusiana na matumizi yake binafsi mshahara wake hupo atumie huo,kwa sababu sijawahi kuugusa wala kumuuliza huwa anafanyia nini..


  Ndugu zangu haikuwa rahisi hata kidogo kutoa maamuzi ya namna hiyo kwa mke wangu na wazazi wangu kuwapa taarifa..niliongea na mke wangu online via skype zaidi ya masaa 4 hakuamini nini kilichotokea ghafla..ameniuliza maswali mengi sana huku akitokwa na machozi..nilijaribu kumpa moyo nikimwambia nimwitaji zaidi kuwa naye karibu kuliko ilivyo sasa japo aliuliza taarifa zilikuwa za ghafla sana..


  NAWASHUKURU SANA..
   
 2. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #2
  Nov 6, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  kha!!??
   
 3. h

  hayaka JF-Expert Member

  #3
  Nov 6, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  hongera kaka, cha muhimu kudumisha ndoa hakikisha unammbeleza akubali kuja kuishi na wewe.
   
 4. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #4
  Nov 6, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  ni kweli ushauri ulipewa mwingi sana lakini naamini ulichanganya na zako......................
   
 5. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #5
  Nov 6, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Inafurahisha kuona jukwaa linawanufaisha watu kwa maoni na ushauri. Bravo JF and let us keep it up
   
 6. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #6
  Nov 6, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  bila shaka una maanisha mbayuwayu kaka!
   
 7. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #7
  Nov 6, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180

  Uamuzi mzuri kama nadharia ya mbayuwayu ilipewa nafasi. Hata hivyo mbona 4 na 7 vinapingana mkuu. Kwa nini asiache kazi baada ya wewe kuwa na uhakika wa VISA na makazi. Yaani asubirie visa ili hali hana kazi. Hatuombei mabaya, vp ikitokea 'ukavuta kamba' kabla ya kupata makazi na visa na hali yeye kisha acha kazi?.

  Angalia upya hapo mkuu!
   
 8. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #8
  Nov 6, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Isije tena ikawa ile stori ya Theone na Mama Theone wakuu mnaikumbuka ile kitu? samahani kwa kuwakumbusha lakini?
   
 9. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #9
  Nov 6, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Mmmh.....kuacha kazi??? Alafu hiyo namba 6 dah.......!!! Anyways, ni mikakati tu muhimu maelewano na matokeo mazuri. M/Mungu awarahisishie zaidi!!
   
 10. the grate

  the grate JF-Expert Member

  #10
  Nov 6, 2011
  Joined: Sep 24, 2011
  Messages: 205
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hongera kwa kufanyia ushauri wa hapa jamvini kazi
   
 11. N

  Ngereja JF-Expert Member

  #11
  Nov 6, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 796
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Mimi nitakushauri ifuatavyo kuhusu hicho kipengele namba 7. Maadam ni mkeo, endelea kumtumia pesa (ziwe kidogo kama dolla 200 hivi) ili kuonyesha kuwa unamjali licha ya kwamba ana mshahara wake.
   
 12. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #12
  Nov 6, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,280
  Likes Received: 1,720
  Trophy Points: 280
  Mh; kuna mambo hukusema kwenye first thread; kama mlitoka nae kwenye shida imekuwaje amebadilika na kutojua kutunza fedha. Any way the truth unajua mwenyewe. Nakuombea strategy zako zi work ili ndoa yenu idumu.
   
 13. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #13
  Nov 6, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 542
  Trophy Points: 280
  hapo kwenye saba sielewi ,wewe umesema umeamua aache kazi aamie ughaibuni ...huo mshahara wa kutumia atautoa wapi akiacha kazi?
   
 14. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #14
  Nov 6, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Hongera Mkuu kwa uamuzi wa busara. Tambua kwamba mke siyo kitunguu inapatikana sokoni. Umeshamkongoroa komaa naye ni wa kwako.
   
 15. m

  mareche JF-Expert Member

  #15
  Nov 6, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 475
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  mke mkeo tu haibiwi hahahahahaha
   
 16. king'amuzi

  king'amuzi JF-Expert Member

  #16
  Nov 6, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  nakupa hongera naamini hayo yatakuwa ni maboresho ya mgogoro wenu kuliko kulimwaga.
   
 17. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #17
  Nov 6, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,148
  Likes Received: 3,337
  Trophy Points: 280
  Uamuzi mzuri umeuchukua.
   
 18. DASA

  DASA JF-Expert Member

  #18
  Nov 6, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 1,031
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Uamuzi sio mbaya sana ndugu, lla bado kuna uwalakini na mambo fulani ambayo kwa mtazamo wangu yataleta madhara kwa ndoa yako unayoipenda.

  1. Mkeo kupatiwa hela na wazazi wako nadhani sio vizuri, itamjengea imani na roho mbaya kwa wazazi: Mi nafikiri kwenye hili bora umtumie hela yeye mwenyewe na umuamrishe kiasi fulani cha pesa yeye ndio apeleke kwa wazazi. kama hii itashindikana labda uamue hiyo awali ambayo mi binafsi nadhani sio salama.
  2. Suala la mke kuacha kazi pia sidhani kama ni sahii sana labda utuambie huko ughaibuni unategemea kukaa kwa muda gani. kama ni miaka 2 au 3 bora mkeo aendelee na kazi yake kama kawaida. kumbuka kumleta huko mkeo utajiongezea gharama za maisha.
   
 19. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #19
  Nov 6, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Ingependeza saana kama tungekua tunapata feedback kwa woote kama hivi.... Hongera Mkuu...
   
 20. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #20
  Nov 6, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mkuu kama ungetukumbusha thread yako ilihusiana na nini ingependeza ili nasi tujifunze pindi tutakapokumbana na hili
   
Loading...