Heri kufanya uamuzi wa kuendelea mbele kuliko kurudiana na moja x wake,kurudiana na x ni kosa la jinai kwenye mapenzi.i dnt advyz ha ku-go back 2 any of da x....lyf goz on...
kwa ushauri wenu, mdada huyu anapaswa kui handle vipi situation hii?...
natamani kumwambia ajaribu wa tatu, lakini mapenzi ni sumu, hayaonjwi!
kwani namuogopea asijejipa matumaini sana kwa huyu watatu
halafu matokeo yake huko mbele ya safari abakie akiilaani bahati yake...
mind you, tafsiri ya abuses huenda inatofautiana baina ya mtu na mtu, au jamii na jamii....
mwenyewe ananisisitiza -" better the devil you know,...!"-
...halahala jamani, mbu mie nasubiriwa na jibu langu jumatatu asubuhi...khaaa!?
Mkuu...kumshauri kuhusiana na hili ni pata potea kwani huwezi jua yatakayotokea kesho na keshokutwa.
Ushauri wako unaweza mletea shida mbeleni na akakulaumu wewe kwa yatakayompata.
Nadhani itakuwa vyema kama utamweleza pros n cons za lolote atakaloamua then yeye ndio achague pa kuenda.
Kumbuka....mshauri mbaya ni adui.
...what if?....maana kwa maelezo yake nilivyomuelewa, namuona kana kwamba kuna udhaifu wake anaoujutia
ambao (japo hakutaka kunifafanulia) anaamini angeujua na kuusahihisha hapo awali, labda wasingefikia huko...
mind you,...anawafahamu vizuri sana hao walitangulia kuliko aliyenaye sasa...
mapenzi ambayo sio serious kivile kama hao waliotangulia.
Sasa Mbu ushauri gani tena anataka wakati hapo kwenye RED ni kama ameshaamua kwamba anaowajua na matatizo yao ni chaguo bora zaidi. Kwahiyo hapo ni kiasi tu cha yeye kuchagua kati ya A na B.
Kama angekua hajaamua kwamba ''Zimwi alijualo halitamla likammaliza'' ushauri wangu ungekua kutokuangalia nyuma unless ANA UHAKIKA kwamba huyo anaetaka kumrudia amebadilika kitu ambacho hakiwezekani!!! Binafsi naona kwamba ni rahisi zaidi kuwa na matumaini na huyoo mpya kwasababu hajaonyesha matatizo so far....kwahiyo kuna uwezekano mkubwa akawa one of the good guys.Tofauti na hao ambao tayari anajua ni wanyanyasaji na hana uhakika kama wameacha/badilika.
Either way yeyote atakaemchagua kuna uwezekano wa kuja kujuta hapo baadae...sasa aamue kama majuto yapi yatakayomla zaidi....Kurudi alipojua kabisa uwezekano wa kuumizwa ni mkubwa au kujaribu bahati sehemu iliyokua na matumaini.
dah hapo pagumu mana kuna watu ambao kwenye mapenzi wanaudhaifu wao binafsi,anaweza akaachwa au kuachana na mtu but baadaye yupo radhi kurudiana,cha msingi we mwambie tu aungalie moyo wake upo upande ganu na wewe usitie neno asije akakulaumu baadaye.
Hili sredi nashindwa kulichangia kwakuwa Mbu kafanya makusudi akalitoa Jumamosi wakati anajua ntakuwa nimeshautwika mtungi.
I'll be back........On Monday!!
teh teh teh heri unyamaze tu wajukuu wasije wakasema babu leo hana busara.Hili sredi nashindwa kulichangia kwakuwa Mbu kafanya makusudi akalitoa Jumamosi wakati anajua ntakuwa nimeshautwika mtungi.
I'll be back........On Monday!!
....swadakta bro,
hebu nibainishie basi hizo pros & cons kwenye sakata kama hili nami nijifunze kidogo.
kumbuka, maelezo yangu hapo juu ndio kikomo cha uelewa wangu
juu ya sakata hili pia...
Ipo hivi mkuu...watakiwa kumuelezea kuwa yanaweza tokea haya.
Kwa haraka haraka...
kwanini arudiane na mmoja wao.
1.anawajua vyema so atakuwa amepata namna ya kudeal now.
2.watakuwa wamejifunza mapungufu yao hivyo kwasasa watakuwa wamebadilika.
3.wamekutana na wanawake wengi baada yake lakini wamegundua yeye ndio anafaa kuwa mama watoto.
4.Watakuwa wamepevuka zaidi hivyo kujua majukumu yao kwenye mahusiano hivyo ajiandae kula bata.
5.Jamaa alienae sasa hivi haeleweki expire date yake ni lini....
6.Zimwi likujualo halikuli likakwisha....
7.
Kwanini asirudiane nao.
1.wanamtesa kihisia na kimwili...tabia hii si njema na bado hata kwenye ndoa hawajaingia.
Twagemea makucha halisi ya mtu huwa yanaonekana akiingia ndoani...wameanza toa kichapo mapema hii...akiolewa je.
2.wameachika kwa wanawake wengine kwa tabia hii...so wanarudi kwake kwani hakuna mwanamke awezae vumilia kuumizwa.
3.Wanadai wamebadilika na si rahisi kutambua kama kweli kwani twajua jasiri haachi asili.
4.Tayari ana mahusiano na mtu mwingine...ajali hisia zake.
5....
6...
Huu sio ushauri ila ni mwongozo wa nini chaweza kutokea akichagua kwenda njia yoyote....atapoenda popote...matokeo yake anayajua na itakuwa ni uamuzi wake na sio wako.
Ngoja niwahi mpirani...