Mjue Lee Kuan Yew- Maamuzi magumu 10 kutoka kwa mtu aliyeiona kesho ya nchi yake

MSEZA MKULU

JF-Expert Member
Jul 22, 2011
3,763
5,591
images

Wakati watanzania tunamlilia NYERERE mimi nasema Hapana Tunapaswa kumlilia NYERERE WA KARNE YA 21, Atakayemalizia kile ambacho nyerere alikiachia njiani alipong'atuka. Mjue mtu huyu jaPO KWA KUPAPASA utajua tunamuhitaji nani.....

Duniani HUwezi kuzungumzia mapinduzi ya uchumi in ASIA bila kumtaja BAba wa taifa wa SINGAPORE LEE KUAN YEW, ukiona uzito mjifunze waziri wake mdogo tu DR GOH KENG SWEE.

hebu tujifunze Maamuzi au mambo kumi ambayo nakwenda kukusaidia wewe, mimi, taifa hata viongozi wetu kutoka kwa mtu huyu wa kuheshimika sana duniani aliyeipatia nchi yake uhuru mwaka 1965 ikiwa hoi kabisa.




1:INALIPA KUWA NA AKILI

Screen-Shot-2015-03-10-at-2.37.10-pm.png

Miongoni mwa maamuzi magumu aliyochukua tangu mdogo, ni kusoma na kuwa mtu mwenye maarifa ya kutosha. alikuwa miongoni mwa wanafunzi 150 bora kabisa kielimu SINGAPORE. MWanasheria msomi kabisa katika nchi hiyo mwenye DOUBLE FIRST CLASS HONOUR kutoka Cambridge. Gazeti la amerika TIMES linamuelezea kama "Mtu mwenye akili nyingi asiyevumilia hali ya chini au kati kwa gharama yoyote ile"

2:WAKATI MWINGINE UNAPASWA KUFANYA MAAMUZI YASIYO YA KAWAIDA KUTIMIZA MALENGO YAKO.

lky1.jpg

Ilimbidi afaye maamuzi magumu yasiyozoeleka kwa faida ya SINGAPORE, Alikuwa na mzigo moyoni mwake kwa nchi yake. Kuna baadhi ya maamuzi hadi kesho watu wameshindwa kuyatafsiri. Ilibidi ailingilie maisha ya binafsi ya kila raia tena kwa ukali, " tusingefika hapa kama tusingingilia maisha ya kila mmoja wewe ni nani? jirani yako ni nani?unafanya nini? na anafanya nini? kwa nini huko ivyo? utatokaje hapo?"

3:ONGEA KWA MAMLAKA NA KWA KUMAANISHA
ch_1_1_1.jpg

HAkuwa mtu wa kuchekacheka kwa vitu vyenye tija kwa taifa. Alipokuwa akiongea ni vigumu kutokusikiliza hata kama ni mgeni unapita na hayo mambo hayakuhusu. Tafuta video akiwa waziri mkuu utaelewa ninamaanisha nini.
angalia hii clip fupi utaelewa namaanisha ninihttps://www.youtube.com/watch?v=RBzCxnRZFBM#action=share

4:USIPIGIE MAKOFI KILE AMBACHO WENGI WANAFIKILIA
lee-kuan-yew-tribute-2.jpg

Pamoja na kuwa kiongozi wa mfano alikuwa na udhaifu wa kutokuchagua maneono ya kuongea.
Muda mwingi aliongea vitu ambayo KISIASA WENGI WALIONA HAYUKO SAHIHI ila yeye hakuwahi kujali hilo. Kuwa na uwezo wa kutokujali sana watu wanafikiri nini na kujielekeza kwenye FACTS ni kitu utajifunza kwa mtu huyu.
"Nimeshutumiwa kwa vitu vingi maishani mwangu, lakini hakuna hata adui wangu aliyewahi kunishutumu kwa kutokusema ninachofikiri na kuamini"


5:KUWA KIONGOZI WA KUHESHIMIWA, LAZIMA UWE KIONGOZI WA KUOGOPWA


LKY-TCC.jpg

SIku zote alifahamika kama mtu mwenye NGUMI YA CHUMA, alikili kabisa yeye aliusambaratisha upinzani kabla haujaibuka na kuota mizizi. alichukua PRINCIPLE ya mwanzilishi wa siasa hizi za kisasa kutoka ITALY MACHIAVELLI THE PRINCE, "kiongozi mzuri ni yule anayeogopwa".

6:KITU CHA KWANZA KWANZA, USIWE MNAFIKI ISHI UHALISIA
a9cf26b2388e492e8bc6e37aed27bdd8.jpg

lee-kuan-yew.jpg

Inahitaji mtazamo wa kiuhalizia kutatua matatizo halisi ya dunia au nchi. Alikuwa muwazi kiasi kwamba kusema mambo ya uganga, uchawi wakimashariki ya mbali ni "uchafu usiovumilika".Aliwahi kuamuru nyumba aliyojenga IBOMOLEWE kupisha Mji ukue watu wajenge majengo marefu yenye faida kwa taifa, bila kujali familia wala watoto wake watasemaje. Ni kama maamuzi ya kuihamishia ikulu DODOMA ili Ikiwezekana pale panaponyima majengo marefu kujengwa ili uchumi ukue tena kwa mipango.


07; USIRUDI NYUMA HATA KAMA UNAENDA KABURINI
MTE5NDg0MDU1MDM1MjgyOTU5-1024x1024.jpg

Anafahamika kwa kauli yake maarufu
'Even from my sick bed, even if you are going to lower me into the grave and I feel something is going wrong, I will get up''.

Ni hii morali 'NEVER SAY DIE' aliyokuwa nayo mpambanaji huyu kufanya umasikini na matatizo ya taifa lake kuwekwa kwenye kumbi za makumbusho sio kwenye maisha ya raia wake. na hili alilifanikisha.

8; WASOMI WAOANE ILI TAIFA LIPATE IDADI KUBWA YA WATAKAOWASAIDIA WASIO NA ELIMU
1402_VALENTINE_MALAYSIA_620_435_100.JPG

Miongoni mwa mambo tata ya mtu huyu, ni kuhitaji walikwenda vyuo vikuu wadada kwa wakaka kuona ili nchi iwe na kizaki cha watu weredi. lengo ni kuwa na watu wakutosha wakuwasaidia masikini wengi wasiona uelewa wowote. Kama hili likipuuzwa aliona kama taifa litakoswa kizazi cha kubeba njozi zake.

9;ISHI MAISHA YA AFYA KIASI NA KUJITAWALA

eaed257aadba080da7e5b5ef8317ee86.jpg

ja1exercise263e.jpg

lee-kuan-yew-swimming.jpg

Hata katika uzee wake alikuwa mtu wa mazoezi, aliamini katika mazoezi yote ya ubongo na mwili. kutibu stress na hali ya kukurupuka kimaamuzi Alikuwa mtu wa kufanya TAFAKULI/MEDITATION. Hata wakati akiwa yu dhaifu wa kiafya kabisa alikuwa anapanda ngazi kwa miguu badala ni kutumia lifti. Alikuwa aigizi ni maisha yake.

10;ONYESHA MAPENZI YA KWELI SIO KWA TAIFA TU BALI PIA KWA MKEO NA FAMILIA

Singapore-Founding-Father-Lee-Kuan-Yew-CambridgeUniversity16.jpg

2.jpg

2006-lee-wife-ap.jpg

2006-lee-wife-ap.jpg

Wananchi wa SINGAPORE wanavingi vya kujifunza kwa familia ya mzee huyu, sio tu mahaba kwa taifa ila kwa familia na mke wake. Mahusiano masafi ya kuigwa yasiyo na skendo. kama ni mpenzi wa love stories fuatilia maisha ya wapenzi hawa hususani wakati mwanamke huyu anakaribia kupoteza maisha 2010 baadae mwaka jana lee nae akafariki.
mfano wa mazungumzo ya wapenzi hawa dakika chache kabla ya kufa kwa mke,


Lee Kuan Yew: “We have been together for most of our lives. You cannot leave me alone now. I will make your life worth living in spite of your physical handicap.”

Kwa Geok Choo : “That is a big promise.”
Lee Kuan Yew: “Have I ever let you down?”

“We have never allowed the other to feel abandoned and alone in any moment of crisis.” Lee Kuan Yew



MWISHO,
beautiful-singapore-wide-hd-wallpaper-download-images-free-new-best-desktop-background-pictures.jpg

TANZANIA HAIHITAJI UKAWA,CCM, WALA WANAHARAKATI,WALA KAULI MBIU MPYA KILA SIKU, INAHITAJI MTU MMOJA TU MWENYE ROHO ISIYO YA KURUDI NYUMA, ATAKAYELINYOOSHA TAIFA NA KULIONGOZA KWA MKONO WA CHUMA USIOSITASITA WALA KUJIPENDEKEZA.

HUYU LEE KUAN YEW MSINGAPORE MWENYE ASILI YA CHINA PIA NDIE BABA WA CHINA [HE IS THE FATHER OF MODERN CHINA] HII TUNAYOIPIGIA MAGOTI, WAO WALIJISHUSHA NA KUJIFUNZA KWAKE LEO WANATAWALA AFRIKA KWA MARA YA TATU.


SEMA CHOCHOTE .....
 
Haya!! its too late for Magufuli...
We are controlled by other forces!!
tatizo hata sisi wananchi tunanaridhika na mafanikio ya juujuu tu tunayoyaona.
maamuzi magumu bado na pia lazima yaendane na sambamba na national mind transformation
 
Bila sisi wananchi kutofata yale mazuri yanayooneshwa na Magufuli tutakuwa wanafiki
Twapaswa kufata kile asemacho kaunzia kupunguza matumizi yasiyo na tija
 
Dah...mkuu napenda sana kukufuatilia thread zako....heshima kwako@mseza mkulu
 
Mhe. Magufuli anataka kufanana na huyu bwana kwa karibu! Amini usiamini, Magufuli anaweza kupata Tuzo la Mo Ibrahimu muda ukiruhusu!
 
Mhe. Magufuli anataka kufanana na huyu bwana kwa karibu! Amini usiamini, Magufuli anaweza kupata Tuzo la Mo Ibrahimu muda ukiruhusu!
Huyu jamaa fuatilia documentary zake. Magufuli unaonyesha njia
Mhe. Magufuli anataka kufanana na huyu bwana kwa karibu! Amini usiamini, Magufuli anaweza kupata Tuzo la Mo Ibrahimu muda ukiruhusu!
Magufuli kujua anaowajua wapi kulinganisha na huyu mpiganaji tafuta documentary za
Mtu huyu Lee Kuan Yew au Mchina Deng Xioping utajua gharama ya kufanya nchi inayopokea misaada kuw nchi inayotoa msaadA
 
LKY alikua mbaraka sana kwa Singapore, pamoja na udikteka wake wa kumiliki vyombo vyote vya mawasiliano, mahakama zote kua chini yake na kuua wapinzani. Lakini bora tu wamefika hapo wenzetu kuliko kuendelea kua masikini
 
Back
Top Bottom