Maalumu kwa wanaume wanaotaka kuoa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maalumu kwa wanaume wanaotaka kuoa.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by mpungara, May 28, 2012.

 1. mpungara

  mpungara Member

  #1
  May 28, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 70
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  [FONT=&quot]HAYA KWA WOOOTE WANAOTARAJIA KUOA[/FONT]
  [FONT=&quot]
  Hivi jamani, mnazijua gharama anazoingia bwana harusi hadi anapooa? Katika hali ya kawaida kabisa, kama wewe ni mwanaume na unataka kuoa, jiandae kwa mambo haya:
  1. Kujitambulisha ukweni. Hapo utatakiwa uende kijijini alikozaliwa mkeo mtarajiwa ukajitambulishe huko. Kama mfano mkeo anatokea Mwanza, na mnaishi Dar, andaa nauli ya watu wawili, malazi kwa siku mbili, na utagharamia shuhuli hiyo ya utambulisho. We tenga 500,000. Hapo tuna assume mkeo atajitegemea. Otherwise 800,000 itakutoka.

  2. Kumtambulisha mkeo kwenu. Kama nyie nyumbani ni Arusha, utatakiwa umpeleke huko Ngarenanyuki. Sio umlete hapo Tabata mlipopanga. Hapo sio kwenu! Andaa nauli yako na atakaekusindikiza, nauli ya binti na mwenzie, na gharama za vinywaji na chakula siku hiyo. Utahitaji kama 700,000

  3. Kifuatacho ITV ni kuwaalika wakwe zako nyumbani. Uwatoe watu kama nane Mwanza, uwalete Arusha. Wale, walale, wajisaidie, kwa gharama zako. We acha ubishi, tenga 800,000 tu.

  4. Kwani we wazazi wako wanajua unakooa? Sasa je? Wasafirishe kwenda Mwanza! Watu watano. Utahitaji kuwa na 500,000. Beba pia ATM card yako, kuna imejensi.

  5. MAHARI ndio topic inayofuata sasa. Ukiwa mjanja, unganishia kwenye hiyo safari hapo juu uue ndege wawili. Pamoja na hayo, itabidi ubebe 2,000,000.

  6. Sasa kijana unaweza kumvisha mchumba wako pete. Nunua ya kawaida kabisa ya dhahabu. 350,000. Tukio lenyewe la kumvisha pete unaweza ita marafiki wawili watatu ukatumia 200,000. Au fanya sherehe kabisa. Mi simo

  7. Oke, sasa unaweza kuitisha vikao vya harusi. Tengeneza kadi za mwaliko wa kamati kwa 200,000, kikao cha kwanza gharama zote ni juu yako. Andaa 500,000. Swali la kwanza kwenye kikao: "We una shing ngapi?" Sema 1,000,000.

  8. Utahitaji 100,000 ya sms na simu kukumbushia michango. (Shukuru Mungu kuna cheka time)

  9. Wakati vikao vinaendelea, utatuma 200,000 kwa m-pesa ili mambo ya kimila yaendelee kule nyumbani. We unaelewa

  10. "Darling, sasa mi kwenye kitchen party ntavaa nini?" 300,000!

  11. "Darling, kuna mahali nimeona gauni zuri la send." 400,000!

  12. "Baby, rafiki yangu alinunua gauni la harusi China yani lilimpende..." 700,000!

  13. Wakati huo wewe mwenyewe hujajua utavaa nini, hujanunua pete za harusi, hujamvalisha best man na mkewe. Tuseme unahitaji kama 1,500,000 maana utalia lia sana. Kumbuka, gharama hizi huchangiwi na kamati. Wala hutarudishiwa.

  14. Siku ya send off lazma uende Mwanza. Utaenda mwenyewe? Ndugu wawili watatu na mshenga 600,000. Kwenye send off utatakiwa kutoa sijui blanketi la bibi, vitenge vya mashangazi, na vikorokoro kibao. Nunua hivyo vitu 300,000 uende navyo ili kupunguza gharama. Beba 200,000 za wale mashangazi watakaoibuka ghafla!

  15. Mshonee baba mkwe suti 100,000 mama mkwe yeye atavaa gauni la 50,000.

  16. Fotokopi hiyo hapo juu (namba 15) kwa wazazi wako. 150,000

  17. Watu watakaopenda kuvaa sare wajitegemee! Mimi sina hela! Ila utavishonea nguo vile vitoto kwa 80,000.

  18. Siku mbili kabla ya harusi, utaanza kupokea wageni. Unatakiwa uwatafutie malazi na chakula. Kwa ujumla utahitaji kama 500,000

  19. Jioni watoe auti mashemeji zako ambao hawajawahi kufika Dar ukawanunulie bia ili wakuone wa maana. 200,000

  20. Siku ya harusi bibi harusi na mwenzie na watoto na ma maids watatakiwa wakapambwe saluni. 200,000

  21. We na mwenzio mtaenda kunyoa hapo kwa nanii. Ndevu na nywele na black kibishi 40,000

  22. Siku ya harusi beba sadaka 10,000. Wakati huo umeshamtuma kijana akakulipie hoteli mtakayofikia baada ya harusi. Kamati haitoi hela hiyo, so utalipa malazi ya siku mbili 200,000

  23. Kama mtaenda honeymoon sehemu yoyote nzuri nzuri nje ya mji, si chini ya 800,000 kwa angalau siku 5.

  24. Wakati uko huko honeymoon, huna hata kumi, mwanakamati mmoja ambae hakuchanga anakupigia simu " Sasa tunavunja lini kamati?" Pesa yote iliyochangwa ilitumika kwenye harusi, sasa gharama za kuvunja kamati ni za nani?? 500,000!

  25. SASA MNAANZA MAISHA YA UNYUMBA. 14,180,000 poorer.
  KAZI KWENU MSIOOA/MTAKAOOA TENA.KAMA VIPI JIWEKE MAPEMA HAAA HAAAAAA HAAAAAA[/FONT]
   
 2. promiseme

  promiseme JF-Expert Member

  #2
  May 28, 2012
  Joined: Mar 15, 2010
  Messages: 2,715
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 135
  Mbona unawatisha wenzio wasioe? mbona hizo hela sio nyingi ni viji senti vyakula kuku Mwanza.
   
 3. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #3
  May 28, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kwa waislamu raha sana maandazi tu kitu kipo kwenye mabega ushabeba saa mingi.
   
 4. M

  Mbilimbili Senior Member

  #4
  May 28, 2012
  Joined: Mar 17, 2012
  Messages: 172
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hizo ni gharama za wenye nazo, nikiwa na 3,000,000 inatosha makorochocho yote. Naweka ki2 ndani!
   
 5. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #5
  May 28, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mnarudia mpaka inachosha.

  Leteni za wanaotaka kutoa talaka sasa.
   
 6. Blaine

  Blaine JF-Expert Member

  #6
  May 28, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 2,285
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  peleka bakuli la mchango
   
 7. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #7
  May 28, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  halafu baada ya mwaka mnaachana unaanza tena budget ya harusi ingine,...................poor man
   
 8. piper

  piper JF-Expert Member

  #8
  May 28, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 3,260
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kwa hali hii bora mtu ujibebee tu, am afraid but umeongeza chumvi zaidi man
   
 9. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #9
  May 28, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,047
  Likes Received: 3,078
  Trophy Points: 280
  Hamna discount babu?make hii pesa kwetu sie tunaotoka mashenzini akha ....vinginevyo tuanze kuoa kwa mkopo.
   
 10. Mwana Mtoka Pabaya

  Mwana Mtoka Pabaya JF-Expert Member

  #10
  May 28, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 11,746
  Likes Received: 8,006
  Trophy Points: 280
  Mengi uliyoorodhesha hayahusiani na NDOA bali sherehe ya HARUSI na upuuzi mdogo mdogo kwa wenye akili za kike.

  Ukitaka kuolewa na mimi unatakiwa ujue tu chechi limesimamia wapi, fanta na bia hazitakosekana kwa ajili ya ndugu zako na zangu pale nyumbani jioni ya siku hiyo na honey moon ndio gharama pekee ninayoiwaza. Hapo nitatumia 1,500,000 kwa Ndoa na chakula cha jioni na 1,500,000 kwa honey moon.

  Hayo makuu yenu mngeyafanya kama mnawaoa dada zenu kwani at least mnajua walivyolelewa kwa hiyo hamtajuta. Mahari 2m, nyoooo!
   
 11. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #11
  May 28, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160

  Mwana Mtoka Pabaya . . .angalau mambo ya msingi unatilia maanani (hanimuni na soda ya ndugu wa karibu). Hayo mengine ni kuchezea pesa tu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. M

  Morinyo JF-Expert Member

  #12
  May 28, 2012
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 2,475
  Likes Received: 464
  Trophy Points: 180
  Wanajenga kwanza kubomoa baadae
   
 13. Yummy

  Yummy JF-Expert Member

  #13
  May 28, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 1,801
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hahaaaa Lizzy hii imerudiwa kumbe,nimecheka sana....naona ikiletwa ya talaka nitahitaji mtu wa kunikanda mbavu zangu kabisaaaa
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #14
  May 29, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  ​cold soup.............imeganda hadi mafuta.
   
 15. N

  Neylu JF-Expert Member

  #15
  May 29, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 2,650
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Kwangu mimi nimeona ni mpya kabisa..Nilikuwa sijawahi kuiona kabla! Ila dah! Jamani hayo makadirio ya gharama yako juu sana..Sikubaliani kabisaaa...Ingekuwa ndio hivyo basi Matajiri tuu ndio wangeoa! Me nadhani kama mpenzi wako ( Mwanamke) akielewa hali yako ya kifedha uliyo nayo, huwezi ukagharamika namna hiyo..
   
 16. R

  RushwaNiAduiwaHaki Member

  #16
  May 29, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dah....sijaoa ila nimkecheka mpaka basi. Kwa gharama hizo, sidhani kama kuna haja ya kufuata huu utaratibu wa kizungu, ni kufuata utaratibu wa jadi na kufanya maboresho machache tuu, yaani tuifahamu sehemu ya nyumba ya ibada ni wapi. Mbwembwe nyingine si muhimu sana ni umaskini wa kujitakia.
   
Loading...