Maalumu kwa ushauri wa kombination inayofaa kwenda nayo Form five

Jamani mimi ninahitaji kwenda PCM ??
Je Nini kinahitajika ili niweze kufanya vizuri??? Na piaa kombi hii inaugumu kwenye somo gani???
Mtu akiweka bidii atatoka nayoo
Kwa muda huu ulio baki kama ujaanza tuition tafuta angalau usukume Ata topic moja ya physics japo uwezii kumaliza mana kama Utaenda shule za serikal nyingi hazina walimu wa physics
 
Hahaa Brother unatudhalilisha wana CoET kimsingi ni ngumu kupata Engineer Masikini na ndio maana namshauri dogo apige Izo but anyway Wachina wanakuja kama Contractors sisi wabongo tunakuwa ma engineer
 
Shukran Sanaa ..
 
Naombeni ushauri waungwana ndoto zangu kusoma CBG matokeo yangu ni kama yafuatavyo chem C,biology B, geography C, history C, civics C, kiswahili C, physics F, mathe F, but nimechagua hkl naweza kubadilisha combination???
 
CBJ itakuwa vigumu umefeli Maths na CBG kama sikosei kuna Maths kule inaitwa Basic applied Mathematics (BAM)
 
Naombeni ushauri waungwana ndoto zangu kusoma CBG matokeo yangu ni kama yafuatavyo chem C,biology B, geography C, history C, civics C, kiswahili C, physics F, mathe F, but nimechagua hkl naweza kubadilisha combination???

Kama sijakosea huwa inatakiwa isizidi point 9 kubadilisha combination ndani ya shule,yaani C tatu kwa masomo ya combi yako,possibility ya CBG iko sababu una point 8,hesabu utasoma huko huko sema utakaza msuli sana tu,PCB nadhani itakua ngumu maana una F ya Physics ambayo itakupa point 11 unakua umezidi 9,pia kama miaka minne umepata F inamaana miaka miwili F tena itakuhusu so nenda CBG. Mara nyingi maksi za A level huwa zinashuka grade moja ya o level au zinamaintain ukikaza sana unaweza zipandisha sasa hapo ukiingia na CBG inamaana utatoka na CCC au DDD ila kwa PCB una FCC kuipandisha hiyo F na kwa Alevel mmmh mlima mkubwa sana ndugu
 
Unamaanisha CBG?

Oh yes CBG-Nimesharekebisha,asante.CBG nayo haina issue sana siku hizi baada ya hawa watoto wa CBG kuzuiwa kusoma kozi za Pharmacy,Dental,nk (Sisemi watoto waache kuichukua ila imebanwa kiaina kwenye level ya vyuo vikuu vya TZ)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…