Maalum kwa anae hitaji milango tuu!

hakuna sababu ya kukejeli biashara ya mtu, kama huna jiyo pesa kaa kimya wenye nazo watanunua. HAKUNA ALIYELAZIMISHWA KUNUNUA.
Ila mkuu ungeweka picha na sio kusubiri anayehitaj tu, kuna mtu mwingine anaweza akavutiwa Nazo na kuamua kununua hata kama hakuwa na plan
 
Mleta uzi jitahidi kuwa polite hata kwa yule anayetumia lugha za kejeli juu yako. Mimi binafsi ni mtaalamu wa ujenzi, na nimeshafanya makampuni ya kikandarasi ya daraja LA kwanza. Bei aliyobandika Mkuu ni ya kawaida saana. Kuna wakati sie tulikuwa tunanunua mlango top pekee hadi 600,000 inategemea design na ubora Wa mlango wenyewe. Tembelea majengo ya NSSF, NHC ,PSPF au LAPF ujionee ubora wa Milango hiyo. Ki msingi ninachotaka kuwaambia hapa ni kwamba, kila mtu anunue anachoweza kukimudu. Kama mwonekano wa milango ya 200,000 unakutosha nunua huo. Ila amini kuwa kuna milango tena ya mbao tu inagharim zaidi ya 1M
 
Chief you need to learn to manage your (potential) customers...unapaswa kuwaelimisha kwanini bidhaa zako ni bora kuliko za wengine...dah
Watu wengine bwana, sasa anafanya bzness alafu akiguswa tu anaanza vita ya maneno. Be gentle & humble, jibu kistaarabu, apaswa aelezee kwa ufundi kitaalam avutie mtu japo ajaribu kununua ajionee, sasa kaitwa mwizi ktk kujibu anajumuisha kutukana watz wote, ajifunze
 
Hakuna ubora tofauti wa top za milango, au unajua wako mafara humu jf? Top ya mlango iwe half panel au long panel even plain, hauwezi ukauza laki 5!! Acha bwana. Au wewe unatumia mbao za 4×8 nini, lakini kama ni 2 by 6 au 2 by 8 haiwezekani kabisa. Ebu tuambie top moja inatumia mbao ngapi? Na hizo mbao wewe unanua elfu 80 au? Nenda zako na mifano ya kitoto, eti pipi!! Utapiga nayo sana picha. Kama uneingizwa mkenge ukajua ndio biashara hiyo, wenzako tumeifanya zamani sana. Mwivi mkubwa wewe!!
Kuna jamaa aliniambia 250k nikichukua kuanzia mitatu bei inapungua...
 
Back
Top Bottom