Maalimu Seif anazidi kutangatanga, hatulii lkn matokoeo ni yale yale!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,786
Baada ya kumaliza kuizunguka Dunia nzima kujaribu kuishitaki nchi yetu kwa Wazungu na bila mafanikio yoyote sasa loser huyo Maalimu Seif amehamia ICC, na hii ndiyo habari yake!

(Kwa hisani ya blogu ya Mpekuzi!)
Chama cha Wananchi (CUF) kimesema katibu wake mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad leo atakwenda katika Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa (ICC) kuwashtaki viongozi wa Serikali kwa madai walitumia mamlaka yao vibaya wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana na kisha kuwatesa, kuwakamata na kuwapiga wafuasi wa chama hicho bila makosa.

Chama hicho kikuu cha upinzani Zanzibar, kimesema taratibu zote za kufungua mashtaka hayo zimeshakamilika, ikiwa ni pamoja na kuweka wakili.

Mei 22 mwaka huu, chama hicho kilizindua ripoti yake ya uvunjwaji wa haki za binadamu Zanzibar wakati wa uchaguzi huo na kutangaza azma yake ya kwenda ICC kuwashtaki Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP).

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui alisema mpango huo umekamilika na Maalim Seif ambaye yuko nje ya nchi kwa ziara ya kueleza alichodai ‘figisufigisu’ zilizotokea katika uchaguzi mkuu, ataweka wazi kila kitu kilichotokea na jinsi ukiukwaji wa demokrasia ulivyoshika kasi nchini.

Mazrui alimtuhumu IGP Mangu kuwa anatumiwa na CCM kuwakamata viongozi wa CUF ili wasitimize azma yao ya kueleza ukweli wa yaliyotokea katika uchaguzi, huku akimtaka afute azma yake ya kumkamata Maalim Seif kwa maelezo kuwa “ataitumbukiza Zanzibar kwenye machafuko”.

Siku tano zilizopita, IGP Mangu wakati akihojiwa na Azam TV alisema Jeshi la Polisi wakati wowote litamburuza mahakamani Maalim Seif kwa kuhamasisha uchochezi Zanzibar. Iwapo CUF itatekeleza azima hiyo, itakuwa tukio la kwanza kwa Tanzania kupeleka viongozi wake kwenye mahakama hiyo.

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na naibu wake, William Ruto wameshafikishwa huko, lakini kesi dhidi yao zilikosa nguvu na kuondolewa.

Katika Uchaguzi Mkuu uliopita, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (ZEC), Salim Jecha Salim alifuta matokeo ya rais, wawakilishi na madiwani Oktoba 28, mwaka jana siku ambayo alitakiwa atangaze mshindi wa mbio za urais.

CUF ilidai kuwa ilishinda uchaguzi huo na Jecha alipotangaza uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20 mwaka huu, chama hicho kilijitoa na hivyo CCM kushinda viti vyote.

Mazrui ambaye aliambatana na viongozi wengine wa chama hicho alisema: “Mpango wa kuishawishi dunia kuwachukulia hatua wahusika wote wa ukiukwaji wa haki za binadamu na uvunjwaji wa demokrasia uko palepale, hautasitishwa kwa vitisho vyovyote.

“Lengo ni kuhakikisha unyama dhidi ya raia wasio na hatia unakomeshwa na uzingatiwaji wa sheria za nchi unatamalaki. Tunawaambia polisi kuwa tumechoshwa na figisufigisu maana zitazaa timbwiri.”

Mazrui alisema wanaotaka kuzuia mpango wa CUF kueleza ukweli na kwenda ICC, wanaandaa utaratibu wa kumkamata Maalim Seif aliyedai; “Ni kipenzi cha Wazanzibari”, akisisitiza kuwa jambo hilo ni hatari kwa sababu litaivuruga Zanzibar.

Akifafanua zaidi kile alichokiita mikakati ya CCM kupitia kwa IGP Mangu kuficha ukweli, Mazrui alidai kuwa polisi wamekuwa wakiwakamata wanachama wa CUF mara kwa mara.

"Niongeavyo hapa wanachama zaidi ya 400 wa CUF wamekamatwa na wengine wapo nje wa dhamana,” alisema.

Alisema ni jambo la ajabu kuona IGP Mangu akishindwa kutoa kauli yoyote baada ya Naibu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DDCI), Salum Msangi kuwatishia mawakili kuwatetea wananchi wanaokamatwa kwa tuhuma mbalimbali.

Alisema viongozi wa CUF hawatatishwa wala kunyamazishwa katika kudai haki ya ushindi wa Wazanzibari kutokana na uamuzi wao wa uchaguzi mkuu.

Katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Uchaguzi na Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Shaweji Mketto alisema endapo IGP Mangu ataendelea kuwatisha viongozi wa CUF, watajipanga kwenda kumtembelea ofisini kwake.

IGP Mangu ajibu
Alipoulizwa kuhusu kauli za CUF, IGP Mangu alisema tayari ameshatoa msimamo wa Jeshi la Polisi na walichokifanya viongozi wa chama hicho ni kumjibu tu.

“Ukipendwa sana ukafanya uhalifu tukuache? Tukikutuhumu unafanya makosa tutakukamata hatuwezi kuogopa umaarufu wako,” alisema huku akisisitiza kuwa jalada kuhusu Maalim Seif lipo kwa DPP (Mkurugenzi wa Mashtaka).

“Umesema hao CUF wamesema kuna wanachama wao wamekamatwa, sasa wamekueleza hao wanachama ni kina nani?… kama wamekamatiwa Zanzibar wapo maofisa wa polisi wa mikoa wanaoweza kuzungumzia hilo huko Zanzibar.”

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai alisema: “CCM hatuwezi kujiingiza katika hoja za IGP na CUF tumewaachia wenyewe. Kwa sasa tupo katika maandalizi ya kuhakikisha Rais (John) Magufuli anashinda kwa kishindo kuwa mwenyekiti wa CCM.” Alisema chama hicho hakina sababu ya kutumia Jeshi la Polisi kukandamiza wanachama na viongozi wa CUF.
 
Fikra finyu mtaona anazurura ...ila anautanabaisha ulimwengu juu ya ubaya wa ccm kudanganya dunia kuhusu democrasia ya kupatia misaada.
Pili anajisafisha ma lolote litalotokea wananchi watakapo sema imetosha..uvunjwaji wowote wa haki za binadamu na yakitokea machafuko...amejivua na dunia inamfahamu.
Yeye anajua ccm znz haindoki kwa sababu inawekwa na majeshi ya kikoloni ya tanganyika.
Na wakoloni hawaindoki kirahisi....ni mapambani ndani na nje. Ndo maana ANC WAALIKUWAPO HAPA TZ NA WAKIFANYA DIplomasia Dunia nzima..iliwachukua miaka 50 ..vifungo umauti lakini hatimae haki ikasimama...
Hivyo aluta continua na maalim yupo mbele ya wazanzibari wote ukiondoa kina buthelezi wachache walokubali kuuza nchi yao kwa ndururu..ndio hao wanaelekea dodoma ..kwa mabwana zao wanao waweka madarakani.
 
Kumbe anapenda kutawaliwa, huko anakozunguka kutaka usaidizi walitutawala miaka mingi. Kwa sasa Tanganyika inatosha.
 
Maalim SEIF naona kaamua kuwa VASCO DA GAMA.Msafiri anayezunguka dunia yote kwa gharama za ruzuku ya CUF kwa visingizio vya hapa na pale.Kabuni mradi wa kujiingizia kipato kupitia safari zisizoisha nje ya nchi ya Zanzibar.CUF jamani hela ya ruzuku haitakiwi kuishia tu kubomolewa kwa ajili ya safari.
 
Hivi Maalimu anajua ICC inashughulikia makosa ya aina gani?. Huyu mtu kwanza ni mgonjwa katoka kwen operation ya mgongo juzi tu. Badala apumzike apone yuko kiguu na njia. kweli madarak ...... Kutapatapa hakutamsaidia. Umri umeenda mwe...
 
Mazombi wanao fadhiliwa na serikali kupiga na kunyanganya ni jinai inayo tambuliwa na ICC
 
Bora vasco dagama kuliko vibaraka...kina vuai ni sawa na buthelezi kwa makaburu....
Wanaenda kupiga makofi wakichagua mwenyekiti wao kutoka bara na rais kutoka bara..
Hata hawaoni soni nchi mbili kuungana ..wao wamekua wasindikizaji tu...huwezi kumlinganisha yeye na akina vuai ..
 
Maalim Seif kwa sasa ni kama mwanamke aliyeachika kwa mumewe na sasa anapita huku na huko kumchonganisha mumewe. Hatafanikiwa. Kosa kalifanya mwenyewe kususia uchaguzi
Yule Sultan Jamshad ndo anayemtia kichwa acha aendelee kutangatanga.
 
Maalim Seif kwa sasa ni kama mwanamke aliyeachika kwa mumewe na sasa anapita huku na huko kumchonganisha mumewe. Hatafanikiwa. Kosa kalifanya mwenyewe kususia uchaguzi
NAFSI YAKO INAKIRI KWAMBA SEIF NDIYE MGOMBEA ALIESHINDA KWA KURA HALALI
 
Asisahu kuwaambia Tanzania imepata Rais anaekemea Rushwa, uzembe, anaetaka kweli kweli Rasirimali za watanzania, zitumike kuwanufaisha watanzania
 
Baada ya kumaliza kuizunguka Dunia nzima kujaribu kuishitaki nchi yetu kwa Wazungu na bila mafanikio yoyote sasa loser huyo Maalimu Seif amehamia ICC, na hii ndiyo habari yake!

(Kwa hisani ya blogu ya Mpekuzi!)
Chama cha Wananchi (CUF) kimesema katibu wake mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad leo atakwenda katika Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa (ICC) kuwashtaki viongozi wa Serikali kwa madai walitumia mamlaka yao vibaya wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana na kisha kuwatesa, kuwakamata na kuwapiga wafuasi wa chama hicho bila makosa.

Chama hicho kikuu cha upinzani Zanzibar, kimesema taratibu zote za kufungua mashtaka hayo zimeshakamilika, ikiwa ni pamoja na kuweka wakili.

Mei 22 mwaka huu, chama hicho kilizindua ripoti yake ya uvunjwaji wa haki za binadamu Zanzibar wakati wa uchaguzi huo na kutangaza azma yake ya kwenda ICC kuwashtaki Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP).

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui alisema mpango huo umekamilika na Maalim Seif ambaye yuko nje ya nchi kwa ziara ya kueleza alichodai ‘figisufigisu’ zilizotokea katika uchaguzi mkuu, ataweka wazi kila kitu kilichotokea na jinsi ukiukwaji wa demokrasia ulivyoshika kasi nchini.

Mazrui alimtuhumu IGP Mangu kuwa anatumiwa na CCM kuwakamata viongozi wa CUF ili wasitimize azma yao ya kueleza ukweli wa yaliyotokea katika uchaguzi, huku akimtaka afute azma yake ya kumkamata Maalim Seif kwa maelezo kuwa “ataitumbukiza Zanzibar kwenye machafuko”.

Siku tano zilizopita, IGP Mangu wakati akihojiwa na Azam TV alisema Jeshi la Polisi wakati wowote litamburuza mahakamani Maalim Seif kwa kuhamasisha uchochezi Zanzibar. Iwapo CUF itatekeleza azima hiyo, itakuwa tukio la kwanza kwa Tanzania kupeleka viongozi wake kwenye mahakama hiyo.

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na naibu wake, William Ruto wameshafikishwa huko, lakini kesi dhidi yao zilikosa nguvu na kuondolewa.

Katika Uchaguzi Mkuu uliopita, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (ZEC), Salim Jecha Salim alifuta matokeo ya rais, wawakilishi na madiwani Oktoba 28, mwaka jana siku ambayo alitakiwa atangaze mshindi wa mbio za urais.

CUF ilidai kuwa ilishinda uchaguzi huo na Jecha alipotangaza uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20 mwaka huu, chama hicho kilijitoa na hivyo CCM kushinda viti vyote.

Mazrui ambaye aliambatana na viongozi wengine wa chama hicho alisema: “Mpango wa kuishawishi dunia kuwachukulia hatua wahusika wote wa ukiukwaji wa haki za binadamu na uvunjwaji wa demokrasia uko palepale, hautasitishwa kwa vitisho vyovyote.

“Lengo ni kuhakikisha unyama dhidi ya raia wasio na hatia unakomeshwa na uzingatiwaji wa sheria za nchi unatamalaki. Tunawaambia polisi kuwa tumechoshwa na figisufigisu maana zitazaa timbwiri.”

Mazrui alisema wanaotaka kuzuia mpango wa CUF kueleza ukweli na kwenda ICC, wanaandaa utaratibu wa kumkamata Maalim Seif aliyedai; “Ni kipenzi cha Wazanzibari”, akisisitiza kuwa jambo hilo ni hatari kwa sababu litaivuruga Zanzibar.

Akifafanua zaidi kile alichokiita mikakati ya CCM kupitia kwa IGP Mangu kuficha ukweli, Mazrui alidai kuwa polisi wamekuwa wakiwakamata wanachama wa CUF mara kwa mara.

"Niongeavyo hapa wanachama zaidi ya 400 wa CUF wamekamatwa na wengine wapo nje wa dhamana,” alisema.

Alisema ni jambo la ajabu kuona IGP Mangu akishindwa kutoa kauli yoyote baada ya Naibu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DDCI), Salum Msangi kuwatishia mawakili kuwatetea wananchi wanaokamatwa kwa tuhuma mbalimbali.

Alisema viongozi wa CUF hawatatishwa wala kunyamazishwa katika kudai haki ya ushindi wa Wazanzibari kutokana na uamuzi wao wa uchaguzi mkuu.

Katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Uchaguzi na Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Shaweji Mketto alisema endapo IGP Mangu ataendelea kuwatisha viongozi wa CUF, watajipanga kwenda kumtembelea ofisini kwake.

IGP Mangu ajibu
Alipoulizwa kuhusu kauli za CUF, IGP Mangu alisema tayari ameshatoa msimamo wa Jeshi la Polisi na walichokifanya viongozi wa chama hicho ni kumjibu tu.

“Ukipendwa sana ukafanya uhalifu tukuache? Tukikutuhumu unafanya makosa tutakukamata hatuwezi kuogopa umaarufu wako,” alisema huku akisisitiza kuwa jalada kuhusu Maalim Seif lipo kwa DPP (Mkurugenzi wa Mashtaka).

“Umesema hao CUF wamesema kuna wanachama wao wamekamatwa, sasa wamekueleza hao wanachama ni kina nani?… kama wamekamatiwa Zanzibar wapo maofisa wa polisi wa mikoa wanaoweza kuzungumzia hilo huko Zanzibar.”

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai alisema: “CCM hatuwezi kujiingiza katika hoja za IGP na CUF tumewaachia wenyewe. Kwa sasa tupo katika maandalizi ya kuhakikisha Rais (John) Magufuli anashinda kwa kishindo kuwa mwenyekiti wa CCM.” Alisema chama hicho hakina sababu ya kutumia Jeshi la Polisi kukandamiza wanachama na viongozi wa CUF.
Umetuhabarisha sawa na ahsante lakini sioni uhusiano/ulinganisho wowote na maudhui ya kichwa chako cha habari. Waombe moderators wa kusaidie.
 
Hata sijui kama Maalim seif anajua hiyo mahakama ina shughulika na makosa ya aina gani teh teh.

Hivi Lissu na Lowasa kwanini mnampotosha maalim seif...
 
Niliwashauri wakati ule wana CUF kususia uchaguzi baada ya uchaguzi mtakuja kuwa watumwa,mwisho watu wataanza kuwapuuza,hawakuwa na sababu ya kususa kama walivyowabana kijani kwenye uchaguzi wa mwanzo wangekwenda nae raundi ya 2 bila kususa,
sasa yametimia
 
Asisahu kuwaambia Tanzania imepata Rais anaekemea Rushwa, uzembe, anaetaka kweli kweli Rasirimali za watanzania, zitumike kuwanufaisha watanzania

Angewambia Barrick na wenzake walipe 18% Vat kila gold wanayo safirisha...
Hapa tunakamuliwa sisi wauza mikate...hao wanaogopwa
Akiwaweza hao ndo tutajua kweli anajali maslahi ya nchi kufaidi na mali zake....
 
Maalim Seif kwa sasa ni kama mwanamke aliyeachika kwa mumewe na sasa anapita huku na huko kumchonganisha mumewe. Hatafanikiwa. Kosa kalifanya mwenyewe kususia uchaguzi
Matusi hayo Mkuu kuwa na Busara katika Matamshi yako Hizi ni Siasa tu ndugu.
 
Angewambia Barrick na wenzake walipe 18% Vat kila gold wanayo safirisha...
Hapa tunakamuliwa sisi wauza mikate...hao wanaogopwa
Akiwaweza hao ndo tutajua kweli anajali maslahi ya nchi kufaidi na mali zake....
Siku ilo likifanyika, na hao Barick wakatishia kufunga migodi, mtakuja mnaruka ruka, na kukosoa, nakumbuka zamani mlikua mnasema, Kwanini Utalii inashangia kidogo, wekeni kodi huko, Leo wameweka kodi, mnakuja kutugeuka, kukejeri
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom