Maalim Seif, vipi tena? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maalim Seif, vipi tena?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pundamilia07, Feb 1, 2009.

 1. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #1
  Feb 1, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  *Akumbushia machungu ya kutemwa kwa Dk Bilali

  Na Salma Said, Zanzibar

  KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad amemtaka Rais Jakaya Kikwete kuacha kutamka maneno ya kuwagawa Wazanzibari kwa vile hawagawanyiki.

  Vile vile amesema kutokana na kauli hizo za Kikwete wanachama wa chama chake wataingia katika uchaguzi mkuu wa mwaka kesho, wakiwa wamejitayarisha kupambana na mazingira yoyote yatakayojitokeza.

  Kiongozi huyo aliyewania urais wa Zanzibar mara tatu bila mafanikio, alikuwa anazungumzia kauli ya Kikwete akiwa ziarani kisiwani Pemba kuwa, wapinzani wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) itawachukua muda mrefu kupata nafasi ya kuongoza nchi hiyo au wanaweza wasiipate kabisa.

  Rais Kikwete alisema, "Tutamwendeleza kila mtu kwa sababu dhamana ya maendeleo ni yetu katika serikali. Hawa wengine hawana serikali. Kazi ya wabunge wao na wawakilishi wao ni kufoka tu. Sisi ndio wenye dhamana ya serikali na wala hatubagui."

  Jana akihutubia mkutano wa hadhara katika Viwanja vya Kibandamaiti Mkoa wa Mjini Magharibi, Maalim Seif alisema kauli hiyo ni ya kuwagawa Wazanzibari wote hata wa Chama Cha Mapinduzi visiwani humo, ambao mwaka 2000 walimchagua Dk Gharib Bilali, lakini chama hicho kilipoketi Dodoma kikawaletea Amani Karume ambaye alikuwa ameshika nafasi ya tisa.

  Sasa Maalim Seif, uko tayari kumchagua Dk. Bilal kuwa rais wako 2010?

  Alisema kwamba viongozi wa CCM Tanzania Bara wamekuwa na utamaduni wa kuwagawa Wazanzibari kwa malengo ya kurudisha nyuma maendeleo ya Zanzibar na kuididimiza kisiasa na kiuchumi.

  "Viongozi wa Tanzania Bara wapo katika mkakati wa Mwalimu Julius Nyerere wa kuitokomeza Zanzibar, tunamwambia Kikwete kachelewa Wazanzibari hatugawiki tena ng'o tena namwambia akome akome akome kutuletea fitna katika nchi yetu, afanye chokochoko huko huko bara," alisema Maalim Seif huku akishangiliwa na umati wa watu waliohudhuria mkutano huo.

  Niko hoi bin taaban!!!!!! siasa na wanasiasa wetu!!!!!

  Alisema kwamba, Wazanzibari hawapo tayari kuona umoja wa kitaifa ukivurugwa kwa kisingizio cha mapinduzi, kwa vile mapinduzi ya Zanzibar yalifanikishwa na Wazanzibari wenyewe na ndio wanaopaswa kuyalinda na sio yeye Kikwete.

  Hamad alisema kauli zilizotolewa na Rais Kikwete wakati wa ziara yake Zanzibar haziashirii kuwepo uchaguzi huru na wa haki Zanzibar, kwa vile wapinzani wasitarajie kukamata madaraka ya dola na wengine wataishia kutafuta nafasi hiyo hadi mwisho wa maisha yao.

  Je, Maalim atagombea kwa mara ya nne?

  Alisema CUF imejifunza mambo mengi tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi, baada ya kuvurugwa kwa uchaguzi mwaka 1995, 2000 na 2005 na sasa umekuwa ni utamaduni wa kudumu wa CCM.

  Maalim Seif alisema ameshangazwa na kauli ya Rais Kikwete kwa vile inakwenda kinyume na ahadi yake ya kuhakikisha anawaunganisha Wazanzibari kwa kumaliza mpasuko wa kisiasa aliyoitoa Desemba 30, 2005.

  Ala, Maalim vipi hapa, Kikwete siamesema kuwa habagui, na atajengea barabara hadi Mtambwe, anawagawa vipi sasa?

  Alisema kauli ya Rais Kikwete kuwa Wazanzibari wana haki ya kuchagua madiwani, wawakilishi na wabunge, lakini hawana haki ya kumchagua rais ni kauli inayokwenda kinyume na misingi ya demokrasia na utawala bora.

  Hii Chumvi ya Uvinza!!!!!

  "Napenda kuwaambia wananchi sasa rangi sahihi ya Rais Kikwete inakuja juu, lakini tunamueleza kuwa ngoma itakavyopigwa ndivyo tutakavyocheza," alisema Maalim Seif na kuongeza kuwa Wazanzibari wamechoshwa na matatizo ya kisiasa.

  Ni kweli wazanzibari wamechoshwa na matatizo ya siasa zenu nyie viongozi, hebu waacheni wapate muda wakujitafutia maendeleo badala kuendelea kuwavuruga

  Alisema Wazanzibari hivi sasa wanaishi katika lindi la umasikini na viongozi waliopo madarakani kazi yao kubwa ni kukusanya mapato ya serikali na kutumia kwa maslahi yao binafsi, huku wakiacha wananchi wakiteseka.

  Hapooooo, Maalim ulikuwa Waziri Kiongozi, kwahiyo ndiyo maana huachi kugombea urais wa Zanziibar kula kukicha.
  Kama vile una uchungu na pesa za walipa kodi, Serikali ya CCM inakulipa kila mwezi kutumia pesa hizo walipa kodi, kataa warudishie.


  Alisema hivi sasa Zanzibar wananchi wanakabiliwa na tatizo kubwa la ufisadi wa ardhi, lakini Rais Kikwete ameshindwa kukemea vitendo hivyo licha ya kuwa ni tatizo kubwa hivi sasa kwa Unguja na Pemba.

  "Wazanzibari wamepokea ujumbe wake, lakini tunaamini anataka mikono yake iwe na damu kama Rais Mkapa alivyoondoka na damu mikononi, lakini Wazanzibari tunakusubiri njoo, tulikuamini kwa kauli yako ya kushughulikia mpasuko wa kisiasa, lakini sasa tumekufahamu tunakwambia njoo," alirudia kusema Maalim Seif huku akishangiliwa.

  Mwafaka!!!!!! Rudini mezani mkaelewane, 2009 hii. uchaguzi kesho, jenga image yako kama kiongozi mbadala na si vitisho.

  Akihutubia katika mkutano huo mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba alisema CUF imesikitishwa na kauli ya Rais Kikwete kwa vile inakwenda kinyume na ahadi yake ya kumaliza mpasuko wa kisiasa wa Zanzibar.

  Alisema kwamba, tangu mapema alijenga wasiwasi na uwezo wa utendaji wa Rais Kikwete na kumbatiza jina la msanii na alipata matumaini mapya baada ya hotuba yake ya kwanza kuahidi kushughulikia matatizo ya Zanzibar.

  Prof. Lipumba kumbe wewe ni padri, sikulijua hilo, ushabatiza wangapi yakhe?

  Lipumba alisema katika mikutano mitatu ya Rais Kikwete na mabalozi aliyoifanya kuanzia 2006 hadi 2008, alikuwa akiwaeleza kuwa ameshafikia hatua nzuri katika kushughulikia mpasuko wa kisiasa wa Zanzibar kitendo ambacho ni kinyume na kauli zake.

  "Tunamshukuru Kikwete kwa kuweka mambo wazi kwa vile sasa katudanganya basi tena, kwa vile wanasema wao ndio wanaoamua na rais atateuliwa na yeye nashukuru ametupa muda wa kuweza kujipanga, tena kujipanga kweli kweli, tumechoka na bakora za CCM," alisema mwenyekiti huyo huku akishangiliwa.

  hamjachoka tu, bali mpo hoi kwa bakora za CCM

  Aliwataka vijana, wanawake na wazee kujipanga kukabiliana na vitendo vyovyote vinavyozorotesha demokrasia kwa kuanzia na uchaguzi mdogo wa uwakilishi unaotarajiwa kufanyika Mei 23 katika Jimbo la Magogoni .

  Mkutano huo ulitawaliwa na vilio vya wanawake kwa vile ulibeba ujumbe wa kuwakumbuka wanachama wa CUF waliouawa Januari 26 na 27 mwaka 2001, hali iliyofanya baadhi ya wanawake kumwaga machozi baada ya kusomewa utenzi kukumbusha majina ya watu waliokufa katika vurugu hizo.

  --------------------------------------------------------------------
  Jamhuri ya Pemba inanukia
   
  Last edited: Feb 2, 2009
 2. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #2
  Feb 2, 2009
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  sioni ubaya kwa aliyosema Maalim Seif.I like this guy,i wish kama Tanzania Bara kungekua na mtu wa aina ya Maalim Seif CUF wa kushirikiana na akina Mbowe,CCM ingekua inajiaandaa kupleka salam kwa akina KANU,na UNIP.

  Kikwete alionyesha bonge la udhaifu,hakutakiwa kuongea kama makamba.engetamka makamba hayo aneno ningeelewa but of all the people,Kikwete? I cant believe it?

  Na maalim Seif ameitumia nafasi hiyo kujijenga zaidi.Safi sana Seif,keep it Rolling!
   
 3. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #3
  Feb 2, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  That is politics na ndio maana maendeleo yabnakuwa duni sana kwa sababu viongozi tuliona nao wanaendekeza malumbano ya kisiasa namna hii
   
 4. Piemu Esquire

  Piemu Esquire Member

  #4
  Feb 2, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sakata la Zanzibar ni la wazanzibar wenyewe. Mambo ya kung'ang'ania watu wenye kutaka kufanya maamuzi yao wenyewe waachiwe waamue. Kumbukeni mambo ya Ujerumani Mashariki, USSR, Yugoslavia, Bulgaria, Czechoslovakia, nk Siyo jambo la kufumbia macho kabisa.

  Karne hii hata kama ni kaya inataka uhuru wake yenyewe ipewe.Mambo ya kulazimsha Miungano ambayo haina ridhaa ya wananchi WALA TIJA kwa nchi husika hatuna budi kuondokana nayo.

  Acheni kuendekeza historia ya kuungana tena kwa umasikini uliokubuhuu-Si lazima kukumbatiana bila hiari a wenye nchi.Maalim Seif usidai hayo unayoyasema waambie wazanzibar wadai nchi yao kutoka mikononi mwa hao waliohodhi madaraka. Hakuna mtu mwenye hati miliki ya Zanzibar zaidi ya wazanzibari wenyewe.

  Waambie wadai Nchi yao na siyo maneno maneno mengine.Zanzibar ni nchi yenye maamuzi yake na inayohitaji kuheshimiwa popote duniani. Nilishangazwa sana na mijadala ya Bunge la Jamhuri kupoteza muda kujadili mambo ambyo yako wazi tena hasa.

  Lakini nawaambia wanasiasa siku itafika ambapo kila aliye na dhamana ya kuongoza anacha uongozi na ndipo kizazi kiteule kitarudisha himaya zao zilizoporwa na wendawazimu wachache.
   
 5. N

  Ndivyo Ilivyo JF-Expert Member

  #5
  Feb 2, 2009
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 243
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Katika hotuba hii Mimi Seif amenipa moyo ameonekana kubadili mtizamo sasa. Hii ni nzuri. Lakini inabidi anendelee na yafuatayo:
  -kuhuburi na kushadidia Umoja wa Wazanzibari
  -kupinga kwa nguvu zote aina yoyote ya njama za kuwagombanisha Wazanzibari.
  -kuacha kuwania nafasi ya Urais wa Zanzibar. Bali atafute kada madhubuti kutoka CUF na aendelee kumpigia debe kwa uchaguzi wa 2010.
  -Akubali kuwa wakati sasa umefika wa kuwacha damu mpya ya uongozi ichukue nafasi ya kuiendeleza Zanzibar (iwe kutoka CUF au CCM) hivyo awache kuongea mambo ya Bilali (hiyo ni historia) Yeye na Bilali ni Mawaziri Viongozi wastaafu- wabakie wastaafu.
  -Akitekeleza hayo watu watakuwa na mtizamo tofauti kwa Seif . Atarudisha heshima yake upya miongoni wa Wazanzibari , na asakheri watasahau yote yale yasiyopendeza aliyofanya huko nyuma.
   
 6. J

  Jujuman JF-Expert Member

  #6
  Feb 2, 2009
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 248
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakika wakati wakuiacha Zanzibar yaelekea ulishapita lakini kuna tatizo moja la Msingi ambalo ni lazima liwekwe wazi na wa kuliweka wazi ni Ndugu zangu Wazanzibri. Mpaka sasa kuna kauli tatu toka Visiwani

  1. Kuna wanaotaka kubaki kwa Muungano(ufanyiwe marekebisho)

  2. Kuna wasiotaka Muungano (hawana haja ya marekebisho) na

  3. Kuna wanaosubiri liwalo na liwe, kwa hali hiyo sirahisi kupata ufumbuzi wa swala muhimu kama hili , hivyo ni juu ya WAZANZIBARI kuja na kauli moja kauli iliyonyooka kwamba SISI WAZANZIBARI TUMEAMUA KWA ZAIDI YA ASILIMA HAMSINI NA MOJA (51%) kwa AJILI ya Muungano au DHIDI ya Muungano.

  Tukipata kauli hiyo tutatupilia mbali UJINGA wote wa so called MWAFAKA Time and Money waste, na viagenda vya ujanja ujanja ati MPASUKO WA SIASA ZNB what a POLITICAL JOKE?? Hivyo ndugu zangu Wazanzibari tupeni Kauli THABIT huku Bara tuko wengi sana kuwaunga mkono juu yalile mtakaloamua wanaowawekea Mikwara ni WANASIASA tena wa pande zote. ZANIBARI na TANGANYIKA ni majirani na ndugu Jiographial and Historical kwa hiyo UHUSIANO wetu haukuhitaji FITINA na ULAGHI wa WANASIASA.

  Leo ndugu zetu wa visiwani mnawaweka Watanganyika wote katika Tenga moja na kuwaona WAKOLONI wa visiwa vyenu. Mimi binafsi nitapenda kuiona Zanzibar ikichukua kiti chake UN kwani kufanya hivyo kutarudisha kiti cha TANGANYIKA.
   
  Last edited: Feb 2, 2009
 7. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #7
  Feb 2, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Naona mnayumba tu,Muungano utakatika tu wacha safari hii alete ndege sio vifaru, ikiwa Super Power Russia imebwaga manyanga itakuwa hawa wanye jeshi linalotembea miguu chini na wastaafu kuonekana kupanda baiskeli.

  Maalim anasema kwa kujiamini kabisa kuwa anamkaribisha Kikwete na vitisho vyake, lakini mafuta hayatolewi ikiwa Muungano utakufa na ufe.

  Halafu Muungano huu hauwasaidii Zanzibar hata kidogo zaidi unawasaidia viongozi wa Tanganyika na CCM yake ambao ni mafisadi wa kutupwa kuanzia kofia mpaka kiatu.

  CCM wanatumia nguvu kuulinda Muungano kwa nguvu zao zote kwani Muungano huu ndio unaowaweka madarakani kwa huko Bara na ndio ukaona hata Raisi wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM huwa anachaguliwa kwenye kikao DODOMA, yaani pale Zanzibar hata ukitokea wa kwanza katika tiketi yao basi ukifika Dodoma wanakupiga na chini, ndipo hapo inaposemwa kuwa Karume alitokea wa Tisa lakini akatokea wa kwanza Dodoma. Kumbuka tu CCM Zanzibar walikaa kikao chao na kumchagua Bilal kuwa anafaa kuwa Raisi wa Zanzibar.

  CCM wasahau kupata ushindi Zanzibar hilo wandugu halina ubishi kabisa kabisa, wanachotumia ambacho ni maarufu ni kuuwa kwanza na kujitangazia ushindi wa kishindo, si mnawasikia wakisema uwa tesa. Na siku mkisikia CCM imeangushwa na kukubali kutofanya ujeshi basi, nawapa mwaka tu mtasikia CCM inavyosambaratika hapa Tanganyika kila mmoja ataingia mitini, maana kulia hakutawasaidia tena.
   
 8. AljuniorTz

  AljuniorTz JF-Expert Member

  #8
  Feb 2, 2009
  Joined: Jan 6, 2009
  Messages: 544
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Huyo ndio Maalim ambae kila siku watu wa kisonge hawataki kumsikia but ki ukweli yupo katika nyoyo za watu wengi sana kwa kuwa anawapenda wananchi wake na anaona mbali ktk mambo ya maendeleo ya nchi na wananchi wake.
   
 9. M

  Mkandara Verified User

  #9
  Feb 2, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Yote tisa.. Maalim Sief anazungumza kwa sababu Ulaji haupo! Akipewa kijinafasi tu atasahau azma ya Wazanzibar..He is pure Politician, tuliyaona haya alipokuwa Waziri kiongozi sidhani kama Waunguja wamesahau...
   
 10. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #10
  Feb 2, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135

  Ndivyo Ilivyo,

  Hili la kumwambia Maalim asigombee urais hapo hamtaelewana, yeye ana malengo yaliyojificha kwenye hili la kugombea urais, hawezi kabisa kukubali.
   
 11. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #11
  Feb 2, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Maalim Seif na baadhi ya wenzake wa karibu wana madeni makubwa kutokwa kwa watu mbalimbali ambapo wamekuwa wakipewa fedha kwa ajili ya chaguzi zilizopita. Ahadi ya kurudisha pesa hizo ilikuwa ni kwamba wakishapata serikali tu watayalipa madeni hayo. Hayo madeni yaliedelea kukopwa hadi kwa wananchi wa kawaida kabisa.
  Kwa mfano kuna kiongozi mmoja mkubwa hapo ndani ya CUF ambaye Mkapa alimpa ubunge wa kuteuliwa, wakati wa uchaguzi wa 1995 alitoa pesa yake 700m/= akitumaini ingerudi haraka baada ya kukamata serikali lakini haikuwa hivyo. Sasa sijui alilipwa vipi kutoka kwenye ruzuku haijaeleweka kwani hivi vyama haviweki mahesabu wazi for some reasons, wanaficha, halafu wakati huohuo wanataka serikali ili waongoze nchi.
   
 12. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #12
  Feb 2, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Mkandara wacha iyo ,mbona anapokea mshahara kama Waziri kiongozi mstaafu na ulinzi anapewa na yote ambayo ni haki yake kupewa kutokana na cheo alichokuwa nacho anafanyiwa ibaki yeye mwenyewe tu kuwashukuru na kusema basi.
  Huyu usimfananishe na Zitto ambae makeke yake siku hizi ni kupiga makelele lakini Maalim mwisho tena mwisho katika kumtaja mtu kwa jina na huku akimnyooshea kidole,hilo ni jambo ambalo hulipati kwa viongozi wetu au wabunge wetu wa upinzani.Seif kwa anavyojiamini kiongozi yeyote yule wa serikali akienda upande kuvuka mipaka na kufanya mambo yasioeleweka basi Seif hashindwi kumwita mtu huyo MPUMBAVU na imeshatokea mara kibao kwenye mikutano ya hadhara akiwaita viongozi hao wa serikali ya Mapinduzi WAPUMBAVU,ni shujaa kwa upande wake na anastahili kupongezwa kwa kukemea na hapo umeona amemwambia Kikwete direck...Akome...sijui unalichukuliaje neno hili ikiwa mtu au mdogo wako anakwambia ukome ,mara nyingi humaliziwa na shika adabu yako na Kikwete ametajiwa neno 'akome' hilo mara tatu.
   
 13. N

  Ndivyo Ilivyo JF-Expert Member

  #13
  Feb 2, 2009
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 243
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa mantiki hiyo ataendelea kuwa Seif yule yule. Lakini ajue wazanzibar anayejitia kuwasemea wanabadilika , na hayo anayowaasa wenziwe kuhusu Zanzibar inafaa ajiase mwenyewe kwanza. Kwa kweli sasa Wazanzibari si watu wa kudanganyika tena. Na aanze kuiangalia vizuri hiyo CUF yake kwanza.
   
 14. N

  Ndivyo Ilivyo JF-Expert Member

  #14
  Feb 2, 2009
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 243
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kupanda jukwaani na kumuambia kiongozi wa Taifa akome akome akome. Tena mbele ya Wazanzibari na wanavyolichukulia neno hilo si kitendo cha ushujaa, bali ni cha utovu wa adabu (nidhamu) Usitake turudi pale pale. Hayo pia ni jumla ya maneno yanayotumiwa katika lugha za wachapa tende au- wale walio katika ugomvi wa wake wenza.
   
 15. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #15
  Feb 2, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Sasa mbona unajikanyaga Seif na madeni wapi kwa wapi,kama huyo mtu alikopesha Chama Cha CUF basi ni kwa mapenzi yake,hivyo kwa mapenzi yake hayo hayo ndio mpaka leo bado yupo CUF na hatujamsikia kupiga makelel ila unampigia wewe.Wanasema pilipili wamekula wengine wewe inakuwashia nini nilifikiri utazungumzia ruzuku wanazopewa kutoka serikalini ,anaekopesha anazo na kama hana basi na uwezo wa kukopesha pia utakuwa haupo,si umeyaona mabenki siku hizi hayatoi mikopo,tuendelee !
   
  Last edited: Feb 2, 2009
 16. M

  Mkandara Verified User

  #16
  Feb 2, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mwiba,
  Mkuu wa ngu yaani wewe unataka kiongozi anayeweza kusema fulani ni MPUMBAVU!.. hiyo sifa gani ya uongozi kama sio ujuha wake..Na nakuhakikishia hakuna mtu mbaguzi kama Sief ukisoma taarifa zake zote ni habari za Utenganishi mtupu.. Akiwa Pemba atawazungumza Waunguja kuwa wapumbavu na kusema mengi yanayohusu Waunguja..Kama unakumbuka uchaguzi wa 2000 kabla ya matokeo kutangazwa Unguja kuliwaka moto na Wapemba..kulikuwepo na Ubaguzi wazi kabisaaa, Wapemba waliona wamechukua nchi..
  Trust me, mkuu wangu kama sio Sief mimi nadhani CUF ingekuwa na mvuto zaidi kwa wananchi hata wale walioko CCM...Amini maneno yangu kesho CUF wakimchagua kiongozi mtu wa shoka toka Unguja, CCM hana ubavu kabisa lakini kuwepo kwa Sief ni kuwakoroga Wanzanzibar..
  Yes, anapokea hizo ruzuku kwa nini asistaafu kama zinatosha!..Analia na Muafaka kati ya CCM na CUF hii inawahusu nini Wazanzibar kwani tatizo la Zanzibar ni CCM au ni katiba nzima ya Muungano..Muafaka unatakiwa ktk kuunda katiba inayoitambua Zanzibar kama nchi ndani ya Muungano..matatizo yote ya Zanzibar yanatokana na Katiba ya Muungano sio swala la siasa kati ya CUF na CCM..Kunelea kupika majungu ya vyama ni kuwapotosha wananchi ktk malengo ya Wazanzibar..
  Na ndio maana Kikwete amekandya uongozi wa CUF kwa sababu anaelewa kuwa wajinga wanategemea matatizo yao yanaweza kuboreshwa na siasa za vyama hivi.
   
 17. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #17
  Feb 2, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Inaonyesha hujui siasa upo tu na jazba,si umeona Mkandara aliposema kuwa Seif ni pure politician sijui ulimuelwa vipi? Na mkwere kakosea Pemba siku hizi kwa shida zilivyozidi hakuna tende kuna maziko saa nane,arudi akanyweshwe.
   
 18. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #18
  Feb 2, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Siasa gani wewe za kupambana na kutoa matusi. Iweje vyovyote vile Kikwete ni Rais wa Nchi. Jemadari Mkuu wa Majeshi na mengineyo Huuwezi kusaimama na kumwambia akome mbele ya Watu ambao wanasema kuwa ni Rais wao na Jemadari wao Mkuuwa Majeshi. Na tuyaache hao. Kwani walioropokwa ni watu wa kupuuzwa tu katika baadhi ya lugha zao. Ziko kauli Seif anatoa ni nzuri kamakweli anazisema kwa dhati na kwa hilo mbnona tunampongeza lakini sio atoe maneno ya utovu wa nidhamu na tumpiguie makofi.
   
 19. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #19
  Feb 2, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Nimeona umeewa kuwa mwanasiasa ,nami nikuulize hivi Mpumbavu ni kitu gani ?Au ni sifa anayostahili nani ? Usije ukaniambia kuwa mpumbavu ni mkichaa au mwendawazimu ingawa unaweza kufananisha.Hivyo ukishaielewa maana yake hutamuona Seif kuwa ni **** au kiongozi yeyote atakae kuwa na ushujaa wa kutumia maneno makali katika lugha ya kiswahili na wanasheria wanalijua hilo.
  Hakuna anaeweza kuhimili kama Seif na hilo viongozi wa CUF wanalijua kuwa kwa sasa hakuna mtu ambae ataweza kushindana na Seif si kuwa watu hawapo watu wapo lakini wananchi kwa sasa huna la kuwambia na si kwa lolote lile bali Seif ameshinda mara zote tatu,hilo sidhani kama utalikataa,ni jambo maarufu linalojulikana ,na kilichofanyika hivyo itikadi ambayo imejengeka ndani ya wananchama wa CUF na uongozi wao ni kuwa kwa kuwa Seif hakuwahi kushindwa basi haina haja ya kubadilisha spare tyre ,wacha hilohilo mpaka lipasuke au life ,sasa usijidanganye au kudanganywa ikiwa Seif ataondoka watu watakuwa na mvuto sijui hata wa CCM wataweza kumkubali hayo ni madanganyio ya kitoto kwani system nzima ya CCM haiko tayari kuondoka kwenye madaraka ,sasa hata akiwekwa malaika hali itakuwa ileile kilichofanywa kwa Seif kitafanyika kwake.

  Kuhusu ubaguzi kwa Seif hilo sio kweli ,alipokuwa Waziri alileta uwiano wa vijana wa Unguja na Pemba kwa nafasi za nje,hali ilibadilika baada ya yeye kuondoshwa na wapemba kibao kurudishwa wakati huo Mapuri yule mliemlinda na kumpeleka Uchina ,alikuwa na ubaguzi wa hali ya juu hata kitabu chake alichokitunga kilichomwa moto hadharani na mmemuona alivyoleta kasheshe hapo Bongo na waandishi ikabidi kumkomalia na wakawa hawaandiki habari zake.Seif hajawahi kwenda Unguja na kuwasema watu wa Unguja hivi au vile utata ulitokana kuwa watu wa Pemba waliweza kustand na POLICE na kuhakikisha mamluki hawaruhusiwi na hawapigi kura kwa nini wenzao wa Unguja hawakuweza ? Hilo ndilo lilokuwa mvutano na Seif hakuhusika kabisa na hilo ,hayo ni ya wananchi wenyewe tena hadi leo mvutano huo upo kuonyesha kuwa Pemba waliweza kuonyesha ushujaa kwa kiasi chao.
  Hicho ni kisa kirefu Ndugu Mkandara,maana hata Mbunge wa CUF Unguja alionekana kwenye kideo akiwarudisha na kuwalisha maneno wananchi waliokuwa tayari kulinda masanduku na kuvaana na polizei akiwapa siasa za kiwoga hayo hayakufanywa na wabunge wa Pemba,waliwaachia wananchi watoe hasira zao na kweli walizitoa na ushindi ulipatikana. Sema mengine.
   
 20. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #20
  Feb 2, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Aloo wacha hilo tukishaanza kuitana Jemedari .Mkuu wa Majeshi ,Raisi sijui Mheshimiwa ,tutaibiwa mpaka nywele,nadhani unasikia redio au kuona kwenye TV anaitwa Obama,mwengine Brown ,Bush au George Bush ,hapatangulizwi rank katika siasa fuatilia mikutano ya kampeni nchi zilizoanza demokrasi,maana ukishaanza kuweka vyeo mbele sijui mzee,karibu karib mheshimiwa hivi utaweza kumuuliza na kumdai ?

  Ndio maana mafisadi wamekomba mabenki kwani wafanya kazi wakisikia ombi linatoka kwa muheshimiwa ,ombi kaleta mzee basi hata haulizi mzee gani yeye ataingia woga na kusaidi bila hata ya kusoma na kuchunguza saini tarehe na mihuri ,si umeona majina ya makampuni kwenye ushahidi Huku lililosajiliwa Kilimanjaro Limited lililopewa mkopo Kilimanjaro Company. Upo ?

  Unajua kwenye majukwaa ukimwita Raisi,au Mheshimiwa Raisi saa ingine inaleta kama dharau ni bora umwite mtu kwa jina lake Kikwete ,Karume ,maana ile tone ya kutaja rank mwanzo pia uitazame.

  Seif yupo online mbali ya kutaka kumjengea hoja kua alikosea hilo sidhani kama linawezekana maana aliyoyafanya Kikwete Pemba na mengine kuyasema Unguja yanajulikana na kwa bahati yaliandikwa ,kama yalivyovuja ya Pinda na kuandikwa, Pinda kawaomba samahani WaTanzania wote nafiki Mheshimiwa Raisi Kikwete ipo haja nae kama Muungwana akawaomba radhi wananchi wake walioko Pemba na Unguja kwani hakukagua kabla ya kurapu kwenye majukwaa na ndipo hapo alipowakanyaga kwenye donda.Kikwete ni mtu Muungwana sana kuliko Pinda hivyo naamini anaweza kutumia fursa za kila mwezi akagusia tu japo ababaishe ila itaeleweka.
   
Loading...