Maalim Seif Sharrif Hamad Leo tena Kitope baada ya Kuzuiliwa

5523

JF-Expert Member
Nov 13, 2014
1,724
1,631
Ndugu wanaukumbi nadhan hatujambo asubuhi hii.

Nikiwa Njiani kuelekea Kitope ambapo Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF na Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Shariff Hamad kwa mara nyengine tena ameingia Kitope jimboni kwa Makamu wa 2 wa Rais Zanzibar (CCM) Seif Ali Iddi ili kukamilisha ahadi yake kwa wana kitope ambao walimtumia ujumbe mkubwa kwamba wanataka kurejesha kadi za CCM kwa vile wamechoshwa na Chama hicho.

Itakumbukwa mkutano huu ulikuwa ufanyike Jumamosi ya wiki iliyopita lakini CCM walitawanya Polisi uwanja wa mkutano na mbwa wakali ili mkutano huo usifanyike kwa vile ni moja ya ngome kuu ya CCM miaka yote.

Lakini kuzuia huko hakukufua dafu Maalim Seif juzi kati alitinga Ikulu ya Rais Kikwete na kwa msajili wa vyama kutaka kujuwa kwanini CUF inazuiwa kufanya mikutano baadhi ya maeneo Zanzibar na wanachama wake kupigwa na kuteswa na Janjaweed.

Habari zinazungumza msajili alikerwa na jambo hili kumtaka maalim Seif aendelee na mikutano kama kawaida kwa vile CUF ni cha siasa chenye usajili wa kudumu hivyo wanalazimika kufanya siasa Tanzania nzima na pia habari zinasema kama Zanzibar polisi watakuwa wameshindwa kusimamia mikutano ya CUF basi maalim atapewa ulinzi kutoka Bara.

Naandika haya nikiwa katika maeneo ya mkutano hapa Kitope, watu ni Nyomi na bado wanaendelea kumiminika kwa kweli CUF imekubalika Zanzibar si mchezo.

Baada ya muda mfupi nitakuwa natupia picha moja moja kwa kuweni karibu.
 
mjihadhari tu ccm wanapenda sana vurugu, wakishindwa kwa mbinu moja wanakuja na nyingine! vp chama cha hamad rashid(ADC) hakijaanza kupiga jalamba?
 
Yes,huyo msakatonge sijui anaitwa balozi iddi ni mnafiki tu.....wanzazibar chukueni nchi yenu.Ninavyo ona Tanganyika inakalia visiwa hivyo tu.....pia yule aliyeamuru watu kuuwawa kule pemba hata akiwa amekufa tutachimba kaburi lake na kutandika viboko mifupa yake.Haiwezekani watu wasio na silaha wanapigwa risasi za mgongoni...haiwezekani.
 
Mungu awatangulie ila huwa najiuliza kuhusu mbwa kutumika kung'ata watu pindi huko kugusana nae ni haramu. Polisi ni makafiri kwi kwi kwi kwi kwi
 
mjihadhari tu ccm wanapenda sana vurugu, wakishindwa kwa mbinu moja wanakuja na nyingine! vp chama cha hamad rashid(ADC) hakijaanza kupiga jalamba?

Hamad Rashid ni msaka tonge tu hana nafasi yeyote kwa Zanzibar, amefilisika kisiasa
 
Back
Top Bottom