Watu wengine tunaijua sana historia ya CUF (tangu KAMAHURU na CCW), Maalim Seif, Prof. Lipumba na UKAWA. Suala la madai ya ruzuku ndani ya CUF linaweza kuwa insignificant kwa sababu sheria na. 5 ya vyama vya siasa (1992) inatamka wazi kuwa determinant ya ruzuku za vyama ni proportion ya kura za wabunge na idadi/vichwa vya wabunge wa chama husika ndani ya Bunge, siyo kura za urais. CUF bara ina wabunge wawili wanaobaki wote wanatoka Pemba na mmoja Unguja. Kwa hiyo ruzuku nyingi ikipelekwa Zanzibar ni kwa sababu/rationality ya wingi wa viti vya wabunge kutoka Pemba/Zanzibar. Prof. Lipumba yeye anapenda kugombea urais tu; mikakati yake ya kujenga chama bara imekuwa si sahihi. Siamini kuwa kwa kiwango cha Profesa, Bwn. Lipumba alikuwa hajui anafanya nini! Maalim Seif yuko sahihi pia.
Aidha suala la mgawanyo wa ruzuku ndani na baina ya vyama washirika wa UKAWA lilikwishajadiliwa na kikundi cha watalaam washauri wa UKAWA na kufanyiwa maamuzi na Summit ya UKAWA. Hivyo ruzuku isingekuwa suala hata kusababisha Mh. Lipumba ajiuzulu kwa kisingizio hicho (kama unavyotaka kuaminisha umma). Si muda mrefu kila kitu kitakuwa hadharani na watanzania watapata fursa ya kujua sababu halisi za Prof. Lipumba kujiuzulu uenyekiti CUF.
Tusubiri kidogo