Maalim Seif: Ni afadhali nikae meza moja na CCM kuliko kukaa na Lipumba

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
2,002
5,534
Maalim Seif katika Mahojiano na Clouds asubuhi hii amesema kuwa hawezi kamwe kukaa meza moja na Profesa Lipumba.

Amesema ni bora akae na CCM kwani anawajua kabisa ni adui lakini si msaliti Lipumba na kusisitiza "Mimi siwezi kukaa na Msaliti"

Akaulizwa kuwa mbona hapo nyuma aliwahi kuwa na uhasama wa wazi kabisa na Sumaye lakini baadaye alikaa naye meza moja UKAWA?

Akasema uhasama wake na Sumaye ulikuwa wa tofauti za kichama na alimjua wazi kuwa ni adui kwani alikuwa CCM lakini kwa Lipumba ni tofauti kwani ni msaliti.

Maalim Seif: CUF kwa sasa inaendeshwa kwa pesa za michango ya wanachama. Matajiri hawaji CUF kwani wakiwajua TRA watawasumbua.

Unamzungumziaje Rais Magufuli?
Pamoja na kuwa ni mtu anayepigania haki, asiyependa Rushwa na Ubadhilifu lakini kuna watu hata wafanye nini hawachukulii hatua. Kwa nafasi yake hapaswi kuwa na double standards.

Unadhani kuna uhuru wa vyombo vya habari?

Hakuna uhuru wa vyombo vya habari. Sheria ya Habari ni mbaya kwa wanahabari. Si vema Waziri kupewa uwezo wa kufungia chombo cha habari.

Jecha alifuta uchaguzi kwa ubabe bila kushirikisha wenzake sababu hata katiba ya Zanzibar haimpi mamlaka ya kufuta uchaguzi

Lipumba si mwanachama wa CUF, na Magdalena Sakaya amesimamishwa uanachama, hivyo yote wanayofanya ni batili

Hakuna CUF ya Lipumba au CUF ya Maalim Seif, maamuzi yote ya chama yanafanywa na Baraza Kuu la chama.
 
Hawa wanyamwezi sijui wana nini usaliti umewajaa wepesi kudanganywa mnakumbuka marehemu mzee sita alikuwa anatumika weee kwa kuahidiwa hivi ila mpango ukikamilika wadau wanamtosa anabaki kulalamika haya akisahau wanamrudia tena wanamtumia mpango ukikamilika anatoswa matokeo yake mzee stress zikamjaa mpaka umauti umemfika

Tuje kwa uyu mnyamwezi lipumba naye anatumika mda ukifika watamtupa matokeo yake stress zimjae yamkute ya kumkuta
 
Seif ni Muongo sana!

Kakaa na 'Wasaliti' wengi sana lakin anajifanya kasahau!

2003 NCCR Mageuzi chini ya James Mbatia waliwasaliti CUF Zanzibar kwa kuwawekea Pingamizi na CCM ikachukua Majimbo yote ya Pemba lakin anasema hakainna Msaliti

Chini ya Rais Amani Karume SMZ iliua Wapemba zaid ya thelathini kwny Maandamano ya kupinga Uchaguzi lakin 2010 walikaa chini Wakazungumza

Prof Lipumba kisha confirm kesho atakwenda Clouds kujibu Madai ya Maalim

Maalim Leo kajichanganya tena amekiri kuwa yeye ndie aliekwenda kushtaki kwa Kawawa na Nyerere kuhusu Mzee Jumbe kusema Znz kuna Mgawanyiko baina ya Wapemba na Waunguja hivyo Sheikh Jumbe aliunda Mabaraza ya Usuluhishi wapatane lakin baada ya kushtaki kwa Nyerere walitumwa Bregadia Moses Nnauye na Alfred Tandau na wakarudisha Majibu kuwa Zanzibar Hakuna Mgawanyiko lakin Huyu Huyu Seif ndio huwa anasema Mapinduzi ya Zanzibar yameleta Mgawanyiko Zanzibar mpaka leo

Yeye ndio aliongoza Kundi la wa Znz kumpinga Jumbe kwny NEC kwa Wazanzibar hawataki Serikali 3 Leo anajifanya kuzipigania Hana lolote yeye yupo tayari kujifanya kupigania chochote cha Msingi apewe Madaraka

2010 alijipa Uasisi wa Maridhiano ili apate U Makamu wa Rais na Hakuna cha Maana alichofanya zaid ya blaa blaaa za kusema Znz ilitulia

Jana anasema Alikuwa kwny Ziara isiyo rasmi ya kutazama uhai wa Chama na ilianZia Kimara wakati kila Mtu anajua Ukizungumzia Kimara unazungumzia Chama gani, CUF na Kimara ni Kama Chai na Pilipili,

Kaulizwa Swali la Mtego kuhusu Uwepo wa Viongozi wanaoweza kuipeleka mbele CUF bila ya uwepo wake kaishia kutaja Wapemba wake peke yake bila hata ya kutaja Kiongozi mmoja kutoka Bara hata Mtatiro hayupo kwny orodha yake

Akategwa Tena na Masoud kuhusu Idadi ya Wanachama wa CUF Nchi nzima akataja ni laki mbili na nusu akimaanisha kwa Zanzibar peke yake mpaka akakumbushwa na Bara ndio akataja ni 1.5 Million

Huyu Babu apumzike Siasa alee Wajukuu!

Amekuwa Waziri wa Elimu 1977 wakati huo Rais Wetu Mpendwa Dkt John Magufuli yupo Kidato cha Pili lakin Leo ni Rais Jamaa bado anakimbiza Upepo

Lipumba Kama angekuwa anagawa Posho nene Na Vikao kwny Hotel za nyota 5 Kama CCM kipindi cha Maridhiano kwny Vikao vya Usuluhishi basi angekubali Wazungumze
 
Hawa wanyamwezi sijui wana nini usaliti umewajaa wepesi kudanganywa mnakumbuka marehemu mzee sita alikuwa anatumika weee kwa kuahidiwa hivi ila mpango ukikamilika wadau wanamtosa anabaki kulalamika haya akisahau wanamrudia tena wanamtumia mpango ukikamilika anatoswa matokeo yake mzee stress zikamjaa mpaka umauti umemfika

Tuje kwa uyu mnyamwezi lipumba naye anatumika mda ukifika watamtupa matokeo yake stress zimjae yamkute ya kumkuta
Usiingize kabila letu kwenye mambo ya kijinga.Kama una vinasaba vya ubaguzi usilete kwetu wanyamwezi. Hujiulizi ni kwa nini Mwalimu mambo yake makubwa alianzia kufanyia Tabora?
 
Maalim Seif katika Mahojiano na Clouds asubuhi hii amesema kuwa hawezi kamwe kukaa meza moja na Profesa Lipumba.

Amesema ni bora akae na CCM kwani anawajua kabisa ni adui lakini si msaliti Lipumba na kusisitiza "Mimi siwezi kukaa na Msaliti"

Akaulizwa kuwa mbona hapo nyuma aliwahi kuwa na uhasama wa wazi kabisa na Sumaye lakini baadaye alikaa naye meza moja UKAWA?

Akasema uhasama wake na Sumaye ulikuwa wa tofauti za kichama na alimjua wazi kuwa ni adui kwani alikuwa CCM lakini kwa Lipumba ni tofauti kwani ni msaliti.

Maalim Seif: CUF kwa sasa inaendeshwa kwa pesa za michango ya wanachama. Matajiri hawaji CUF kwani wakiwajua TRA watawasumbua.

Unamzungumziaje Rais Magufuli?
Pamoja na kuwa ni mtu anayepigania haki, asiyependa Rushwa na Ubadhilifu lakini kuna watu hata wafanye nini hawachukulii hatua. Kwa nafasi yake hapaswi kuwa na double standards.

Unadhani kuna uhuru wa vyombo vya habari?

Hakuna uhuru wa vyombo vya habari. Sheria ya Habari ni mbaya kwa wanahabari. Si vema Waziri kupewa uwezo wa kufungia chombo cha habari.
  • Teh! Teh! Teh!, Hiyo ni gia ya kutuambia kuwa anataka mazungumzo na CCM, na ambayo awali aliyakataa mwenyewe
  • Hata ajisemeshe vipi, kuhusu Zanzibar tulishamaliza kwa uchaguzi wa marudio.
 
Seif ni Muongo sana!

Kakaa na 'Wasaliti' wengi sana lakin anajifanya kasahau!

2003 NCCR Mageuzi chini ya James Mbatia waliwasaliti CUF Zanzibar kwa kuwawekea Pingamizi na CCM ikachukua Majimbo yote ya Pemba lakin anasema hakainna Msaliti

Chini ya Rais Amani Karume SMZ iliua Wapemba zaid ya thelathini kwny Maandamano ya kupinga Uchaguzi lakin 2010 walikaa chini Wakazungumza

Prof Lipumba kisha confirm kesho atakwenda Clouds kujibu Madai ya Maalim

Maalim Leo kajichanganya tena amekiri kuwa yeye ndie aliekwenda kushtaki kwa Kawawa na Nyerere kuhusu Mzee Jumbe kusema Znz kuna Mgawanyiko haina ya Wapemba na Waunguja hivyo aliunda Mabaraza ya Usuluhishi wapatane lakin baada ya kushtaki kwa Nyerere walitumwa Bregadia Moses Nnauye na Alfred Tandau na wakarudisha Majibu kuwa Zanzibar Hakuna Mgawanyiko lakin Huyu Huyu Seif ndio huwa anasema Mapinduzi ya Zanzibar yameleta Mgawamyiko Zanzibar mpaka leo

Jana anasema Alikuwa kwny Ziara isiyo rasmi ya Chama na ilianZia Kimara wakati kila Mtu anajua Ukizungumzia Kimara unazungumzia Chama gani

Kaulizwa Swali la Mtego kuhusu Uwepo wa Viongozi wanaoweza kuipeleka mbele CUF bila ya uwepo wake kaishia kutaja Wapemba wake peke yake bila hata ya kutaja Kiongozi mmoja kutoka Bara hata Mtatiro hayupo kwny orodha yake

Akategwa Tena na Masoud kuhusu Idadi ya Wanachama wa CUF Nchi nzima akataja ni laki mbili na nusu akimaanisha kwa Zanzibar peke yake mpaka akakumbushwa na Bara ndio akataja ni 1.5 Million

Huyu Babu apumzike Siasa alee Wajukuu!

Amekuwa Waziri wa Elimu 1977 wakati huo Rais Wetu Mpendwa Dkt John Magufuli yupo Kidato cha Pili lakin Leo ni Rais Jamaa bado anakimbiza Upepo
  • Licha ya kuwa muongo hilo zee ni linafiki na lichonganishi likubwa sana baina ya Wazanzibari na ndugu zao wa Tanzania bara
 
Mbona hawaku balance kama walivyojinasibu kwa Makonda? Au kwann hawakurushaga video ya Makonda afu kesho yake wamhoji Gwajima kama ambavyo watafanya kwa Lipumba kesho.?
 
ukae meza Moja na ccm ili nawe upate mgao kuliko mgao upitie kwa lipumba, hapo fafanua Maalim. tatizo tu hicho kitv nilishakidelete na kamwe sitakuja kukiangalia
 
Back
Top Bottom